Wednesday, 26 February 2014

KAZI YA MAOMBI YA REHEMA

Mwl: Mwinj & Mch. SONGWA, MM. KAZI
MAANDIKO: Ebr 4:16, Mith 3: 3 – 4, 1 Yhn 3:21-22.

YALIYOMO:
1. Utangulizi
2. Maana ya Rehema na Neema
3. Kazi ya Maombi ya Rehema na matokeo yake
4. Faida ya Maombi ya Rehema
5. Aina ya msaada upatikanao kwa Neema kwa njia ya Maombi ya Rehema

01. UTANGULIZI
Je, umewahi kukaa chini na kujiuliza maana ya maneno haya mawili maarufu sana; yaani Rehema na Neema?
Je, unajua Rehema hushughulika hasa na nini katika maisha ya mwamini? Hali kadhalika na Neema hushughulika na mambo gani katika maisha ya mwamini?
Basi; kwa kuifahamu zaidi fuatana nami katika somo hili. Na Mungu akubariki sana.

02. MAANA YA REHEMA NA NEEMA
I. REHEMA:
- Ni ile hali ya kutopata adhabu unayostahili kabisa kupewa kwa sababu ya uovu, dhambi au makosa yaliyofanywa nyuma.
- Ni msamaha wa mwisho wa Mungu uambatanao na kusitishwa kwa adhabu stahiki
- Ni kutopata unachostahili
- Ni msamaha

KUMBUKA: Kimsingi Maombi ya Rehema ni Toba ya kweli mbele za Mungu dhidi ya uovu, dhambi na makosa yaliyofanyika nyuma, Kut 20: 1 -4.

II. NEEMA:
- Ni kupewa usichostahili
- Ni hali kustahilishwa, kupendezwa, kuhurumiwa na Mungu (Favour and Spiritual Blessings of the Lord Jesus Christ.)
- Kuhesabiwa haki vure ( kazi ya msalaba)

03. KAZI YA MAOMBI YA REHEMA NA MATOKEO YAKE
I. Kazi ya maombi ya Rehema;
(a) Kufuta hati ya mashitaka; hali ya kuondoa uhalali wa shetani kututawala na kukutumikisha, Kol. 2 : 14
Pindi unaporudi kwa Yesu unapewa haki na uweza Yhn 1;12

(b) Kupata Ujasiri mbale za Mungu 1 Yhn 3: 21- 22, Mwanzo 3: 8 – 19.

Tabia za Mtu jasiri
Josh 1:1-9, Sam 17: 8-47, Amuzi 14:6, 19, 15:4, 13, 15, 16:3, 27
- Hana hofu ( Fearless person)
- Ana uhakika, anajiamini, shupavu, ana matumaini ( confident person)
- Ni shujaa, thabiti, jeuri (bold person)
-
Mambo yanayoondoa ujasiri ni; Isaya 59: 1-4
- Uovu, dhambi na makosa yetu.

Kumbuka: Kitu pekee kinachompa kiburi na jeuri shetani cha kututesa na kututawala ni ni uovu, dhambi na makosa yasiyotubiwa, Yhn 8: 34, 42-44
Hivyo Mungu anakusihi utubu ili akurejeshee ujasiri na mamlaka ya kumshinda aduui, Ezek 18: 21- 23.

(c ) Kutupa Kibali mbele za: Mith 3: 3- 4, Lk 2 : 52
- Mungu – Ushirika mzuri na Mungu
- Wanadamu – kusikilizwa, kutambuliwa, kufurahishwa na kuheshimiwa.

Kumbuka:
Mtu anapoteza kibali mbele za Mungu na wanadamu; katika ulimwengu wa roho anakuwa kama mtu aliyepakwa mavi usoni na anatoa harufu chafu ( uvundo). Hata kama mtu ana huduma nzuri , ana karama na vipawa vizuri akipoteza kibali tu, hatakubalika kamwe mpaka atengeneze na Mungu, Malaki 2:3.

Angalizo:
Uwe makini kulinda kibaki- ushirika mzuri na Mungu na wanadamu ili usije ukapakwa mavi usoni – ukapoteza kibali.

(d) Kutupa akili nzuri mbele za ; Mith 3:3-5, 24: 3-9, 1 Kor 15: 33- 34
- Mungu
- Wanadamu
Biblia inasema sana juu ya akili, kuwa Mungu ameruhusu tuzitumie akili lakini siyo kuzitegemea kwani akili zina mwisho wake.

Matunda ya akili nzuri ni; Mith 24: 3-6, 3: 13-20
- Hekima (nguvu), maarifa (elimu).
- Ufahamu (Ujuzi na ustadi)

Kumbuka: Urithi wa mwenye akili ni maarifa kwani ana busara, bali urithi wa mjinga (asiye na akili) ni upumbavu, Mith 14: 18


Jambo la msingi la kuelewa vizuri kati ya Rehema na Neema ni kwamba;
-Rehema kazi yake ni kushughulikia MSINGI wa maisha ya mtu, Zab 11:3, yaani mambo ya nyuma. Yanawezekana mengine huyakumbuki; haya ni pamoja na yote yaliyotendwa na watu wengine pamoja na yale uliyotenda mwenyewe.
-Mambo ya nyuma yana uwezo wa kukukwamisha mbele ya safari hata usiweze kuumaliza mwendo; yaani kuyatimiza malengo na makusudi ya Mungu katika maisha yako.
-Neema kazi yake ni kushughulikia JENGO (Maisha) – 1Kor 3:9- 15, na mambo yajayo Ebr 4: 16 (Tazama pia Yer 1:10, Math 13: 24-30, Math 15:13_)

04. FAIDA YA KUMWENDEA MUNGU KWA MAOMBI YA REHEMA

Ebr 4: 16 na Math 5: 7

Faida ni matunda mazuri ya kitu au jambo.

Zifuatazo ni baadhi ya faida:
(i) Tunapokea Rehema ( Msamaha) kwa yale tuliyoshindwa ( Help for our failures)
(ii) Tunapata Neema ya kutusaidia katika nyakati ngumu za uhitaji, 2 Kor 12 : 9- 10)

05. AINA YA MSAADA UPATIKANAO KWA NEEMA KWA NJIA YA MAOMBI YA REHEMA
Ebr 4: 16
Tunapata:
(i) Msaada ufaao ( appropriate help)
(ii) Msaada ujao kwa muda/ majira/ wakati sahihi kabisa wa Mungu ( Divine well-timed help)

Kumbuka: Toba ya kweli huleta Ufalme wa Mungu kwenye maisha ya mtu, Math 4 :17, 3: 2


UISHI MILELE
2Kor 13;14


IMEANDALIWA NA:
Mwl: Mwinj & Mch. SONGWA, MM. KAZI
SIMU: 0757-567899. 0789-567899. 0719-968160, 0779-597066
Email: songwa@yahoo.com ptrsongwak@gmail.com
TAG KONGOWE FOREST. DSM. P.O. Box 70983. DSM.

IBADA YA KWELI [THE TRUE WORSHIP]




TAG – KONGOWE FOREST P.O. BOX 70983 DAR ES SALAAM.


GLORY TO GLORY CENTRE – GGC – DAR.


Mwl: Mwinj. & Mch. Songwa .M. Kazi


SIMU: 0757 – 567899/ 0789 – 567899/ 0719 – 968160/ 0779 – 597066


Email: songwak@yahoo.com/ptrsongwak@gmail.com





MAANDIKO YA SOMO: Yohana 4:20 – 24





YALIYOMO:
Maana ya Ibada.
Aina za Ibada.
Misingi 2 ya Ibada inayokubalika.
Jinsi ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli.
Matokeo ya Ibada inayokubalika.
Sura [picha] ya Ibada inayokubalika.
Maandalizi ya Ibada inayokubalika.
Tofauti kati ya Ibada na Huduma.
Sifa za jumla za Mwabudu.
Msingi wa Ibada ya kweli [Inayokubalika].





Je, umewahi kujiuliza kwa nini unakuja Kanisani?


Leo watu wengi Makanisani hawaji kuabudu bali wanakuja kupokea – kutimiza haja zao tu.


Maana ya Ibada:
Ni heshima inayotolewa na Bwana mkubwa kwa lengo la kumfanya ajisikie vizuri.



Neno Ibada siyo takatifu, ila Yule unayemfanyia Ibada ndiye ataamua Ibada yako ni ya namna gani – yaani ni takatifu [(safi) au ovu chafu)]




Ibada ni kuanguka chini ya miguu ya Bwana na kumbusu miguu au mikono [Proskuneo – Kigiriki].



Tazama. Math 15:24 – 27, Yh 5:5 – 8, 9:6 – 7, 2Falme 5:1-19 n.k.





Ibada ni utii:


Ibada ni sadaka. [kutoa] Mdo 20:35b [Heri kutoa kuliko kupokea]


Ibada ikiwa kama sadaka inalenga maeneo makuu matatu yakutoa:-
Kujitoa mwenyewe [giving yourself] Rumi 12:1.
Kutoa mambo yaujazayo moyo [heart attitudes] 1Sam 1:9 – 15, 1kor 6:19.
Kutoa mali zako [your possession] kumb. 8:18. Jua kuwa wewe na vyote ulivyonavyo sio mali yako ni ya Mungu huna cha kujivunia.





Kumbuka: Mungu hakufanya na hatafanya muujiza kwako/kwangu kama hatutaonyesha roho ya utii (Ibada) kushuka chini ya miguu yake.


Kumbuka: Mungu ni Roho, hivyo inatupasa kumwabudu katika Roho na Kweli.


Kumbuka: Msingi wa utoaji (sadaka); Mungu haangilii ulichotoa anaangali ulichokibakisha. Soma Marko 12:41 – 44 na


Luka 21:1 – 4.





1. KUMWABUDU MUNGU: Yhn 4:23


Kuna aina kuu mbili (2) za Ibada:


i) Ibada inayokubalika mbele za Mungu


ii) Ibada isiyokubalika mbele za Mungu.





I} IBADA INAYOKUBALIKA MBELE ZA MUNGU


Misingi mikuu miwili (2) ya Ibada inayokubalika ni:-


a) Kumwabudu Mungu katika Roho – 23


b) Kumwabudu Mungu katika kweli - 23





Maelezo ya:-


a} Kumwabudu Mungu katika Roho – 23
Hii ni Ibada inayotoka ndani kwenda nje na siyo nje kwenda ndani.
Haiangaalii mazingira wala hali, shauku yake Mungu kwanza apokee sifa – haki yake kasha baadaye mambo binafsi, hivyo hapa Mungu ndiyo kipaumbele. Mdo 16:25.
Ibada hii inaongozwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya Mwamini. Tazama Rumi 1:9 -15; Zab 103:1; 51:15 - 17





Kumbuka:


Kama moyo wako hauko sawa Ibada yako haitakubalika mbele za Mungu. Na kama Ibada ni sadaka, basi sadaka yoyote iliyo bora lazima itoke kwa Mungu.





Mfano: Isaka alitoka kwa Mungu - Mwz 16:15-19, 22:1-2, 9, 19, Yesu alitoka Mungu Yhn 3:16 na Filipi 2:5 - 11





Hivyo basi Ibada inayoongozwa na Roho Mtakatifu itakuwa sadaka itokayo kwa Mungu mwenyewe maana Roho Mtakatifu ni Mungu mwenyewe. Yoh 4:24





Jinsi ya kumwabudu Mungu katika Roho (Method of Worship).


Njia pekee ya kumwabudu Mungu katika Roho ni:-


i) Kujaa Roho Mtakatifu na kumpa nafasi ya kuyatawala/kuyaongoza maisha yako yote. Rumi 8:14, Kor2:11 - 12, 12:13





ii) Kuelekeza mawazo yako yote kwa Mungu (Thoughts centered to God).


Ni ile hali ya kuweka fahamu na akili zako zote juu ya jambo moja. Zab 22:4, Kol 3:2.





iii) Kugundua na kutafakari juu ya Neno la Mungu (Meditating God’s Word)


Kutafakari ni ile hali ya kuweka mawazo yako yote juu ya kitu/jambo moja tu.


Hivyo, kutafakari juu ya Mungu unahitaji zaidi kuwa na Muda wa kutosha wa Kuomba na kusoma Neno. 1Kor 2:10,


Luka 10:38 - 42, Zab 27:4





Hivyo ili kupata ufunuo wa Neno la Mungu, unahitaji kuwa na ushirika wa karibu sana na Roho Mtakatifu.


2Kor 13:14, 1Kor 2:10 - 13.





b} Kumwabudu Mungu katika Kweli - 23


Hiii ni Ibada ambayo misingi yake imejengwa kwatika Neno la Mungu na siyo hisia na msukumo wa nje. (mbwembwe) zingine kama ujanja na uongo. Zab. 119:160, 142; 2kor 4:2, Rumi 1:18 - 19, 25, Yhn. 18:37 - 38; 17:17 - 18, Zab47:7





Kumbuka:


Usichanganye kweli ya Mungu na uongo (uovu).





Matokeo ya Ibada inayokubalika:


i) Mungu anatukuzwa - Zab. 50:23


ii) Waumini wanasafishwa - Zab. 24:3 - 4


iii) Kanisa linajengwa - Mdo. 5:28


iv) Waliopotea wanahubiriwa Injili. 1Kor. 14:23 - 25





Sura ya picha ya Ibada inayokubalika:


Ni manukato/harufu nzuri mbele ya Mungu. Kutoka 30:34 - 38, Yhn. 12: 3 - 8





Maandalizi ya Ibada inayokubalika mbele za Mungu:


Anza na maombi ya Rehema na utakaso mbele za Mungu ili upatane na Mungu ili unapokwenda mbele zake asione kitu kisicho safi (kichafu) akageuka na kukuacha. Kumb. 23:14
Tazama. Ebr 4:10 - 16, 10:19 - 22, Mithali. 3:3 - 4, 1Yhb. 3:21, Yak. 4:7, Zab 24:3-5, Lawi 16:1 -





Tofauti kati ya Ibada na Huduma:


Kuna tofauti kubwa kati ya Huduma na Ibada, kwa kifupi ni kwamba;-


Ibada ni ile inayotoka chini (kwetu) kwenda juu kwa (Mungu) kwa nguvu za Roho Mtakatifu kupitia njia ya Yesu wakati Huduma ni ile itokayo juu kwa (Mungu) kuja chini (kwetu) kwa njia ya Yesu na kwa nguvu za Roho Mtakatifu katika mfumo na karama za rohoni.


1Kor. 12:1 - 11





Hivyo Mungu atashuka kuhudumu yaani kukutana na mahitaji yetu pale tu atakapo kuwa ameipokea ibada yetu (amefurahishwa na ibada yetu).





Kumbuka:
Tatizo kubwa leo wakristo tupo kihuduma zaidi na siyo kiibada; tunaweza kufananisha na (kizazi cha Matha Luka 10:38-48).



Tunapaswa kujifunza kwa Mariam Zab 27:4 na Luka 10:38-42



Kwa hiyo fanya chochote uwezacho kufanya kitakacho mfanya Mungu ajisikie vizuri, maana sahau kupokea kitu kutoka kwa Mungu - BWANA kama Ibada yako haijamfurahisha.





Mungu tangu zamani alishuka kuhudumu, kuchukua au kupokea sadaka n.k. baada ya kupendezwa na ibada hiyo.


Sasa tafuta cha kufanya katika nyumba ya Mungu kitakachompelekea Mungu ajisikie vizuri na kukubariki na kukutendea mambo makuu ya kushangaza. Tazama Mwanzo 4:4 - Sadaka ya Habili.











II} IBADA ISIYOKUBALIKA MBELE ZA MUNGU.
Zifuatazo ni baadhi ya Ibada ambazo Mungu hazipokei kamwe japo walengwa watoa mbele za Mungu wa kweli Mpendwa ni jambo la kuogofya na kusikitisha sana kwenda mbele za Mungu kumwabudu kisha Ibada yako ikakataliwa. Rejea habari za wana wa Adam Habili na Kaini - Mwanzo 4:1-15.



Jambo linalotokea kwa mwamini pale Ibada inapokataliwa ni kuwa roho/moyo wenye chuki (Hatred), wivu (Jelous), kuhukumu (Judgementalism) na uchungu (bitterness) kwa wale wanafanikiwa, barikiwa, kuinuliwa kutumiwa na Mungu n.k.




Usiumize kichwa wala usipate shida na watu kama hao juwa tatizo lao ni kiwango/kimo chao cha Ibada mbele za Mungu bado kipo chini sana ya kiwango na hivyo usipambane nao kimwili washauri wainue viwango vyao vya ibada kwa kuomba, kusoma Neno la kushiriki katika ratiba za Ibada za Kanisa na huduma mbalimbali za kiroho.






Kumbuka:


Watu wengi wagomvi, wachochezi, wezi wa mafungu ya kumi, wasiotulia makanisani (wachanga wa kiroho) wanaosusa kufanya huduma hao wote viwango vyao vya Ibada na Ufahamu wa kweli ya Mungu viko chini ya kiwango. Malaki 3:8-11, Malaki 2:1-4, Zekaria 5:1-4.





ZIFUATAZO NI BAADHI TU YA IBADA ZISIZOKUBALIKA MBELE ZA MUNGU.





a} Ibada itolewayo kwa Miungu. (The Worship of False of God).


Miungu ni vitu vinavyochukua nafasi ya Mungu vyaweza kuwa mali, wazazi, shughuli n.k. (vitu vya dunia - Earhtly materials na sanamu za mfano wa vitu vya mbinguni - Heavenly things) na kumfanya Mungu kuwa wa baadaye. Kutoka 34:14 - Bwana ni Mungu mwenye wivu, Ayubu 31:24-28 usikwke tumaini kwenye vitu na Yoshua 24:20, Kumb 4:14-19, Mark 4:19.





b} Ibada itolewayo kwa Mungu wa kweli katika njia/mfumo mbaya. (The Worship of the true God in a wrong form).


Kutoka 32:1-28 Haruni - wana Israel na ndama ya kuyeyusha.


Mungu hatapokea Ibada itolewayo kwa miungu ya uongo hatapokea ibada itolewayo kwake kwa mfumo mbaya.





c} Ibada itolewayo kwa Mungu wa kweli kwa namna au kwa mtazamo wa mtu apendavyo yeye. ( The Worship of the


true God in a self - styled manners).



Hii ni roho ya mazoea - ilimtesa Samson - Amuni 16:20-21. Mdo 5:1-11 Anania na Safira hii ni kumshusha/kumpunguza Mungu na kumweka katika kiwango cha miungu.




Walawi 10:1-20 watoto wa Haruni, Nadadu na Abihu walikufa kwa sababu walitoa dhabihu wakiwa wamelewa mbele za Mungu tazama Lawi 10:9.




1Samweli 13:8-14 Habari za Mfalme Saul alipoingilia majukumu ya Nabii, Kuhani na Mwamuzi Samweli - ufalme wake haukudumu. 2Nyakati 26:16-21.




Habari Uza aliyekufa baada ya kulinyonyeshea mkono sanduku la Agano. 2Sam 6:1-9.




Habari ya Mafarisayo na Waandishi walivyokuwa wanafiki - Mnafiki ni rafiki adui. Math 15:1-9;23:23-28 (katika zaka na maombi).






d} Ibada itolewayo kwa Mungu wa kweli katika nia mbaya. (The Worship of the God with a wrong attitude)
Nia ni namna mtu anavyofikiria au mtu anavyohisi au ona kuhusu mtu mwingine.





Kumbuka:
Kama tukiabudu hali mioyo na hisia zetu haziko sawa au sahihi hiyo haitakubaliwa na Mungu.



Tazama mfano wa sadaka vipofu na vilema zilitolewa.

Malaki 1:6-14, 3:13-15, 4:1-6, Amos 5:21-22, Hosea 6:4-7, Isa 1:11-20, Mark 7:6





Kumbuka:
kiwango changu cha Ibada ndicho kitakacho amua hatima yangu uko vile ulivyo kwa sababu ya kiwango chako cha ibada.



Matatizo mengi leo hata kwenye ndoa ni kwa sababu viwango vya ibada viko chini. Hebu jaribu leo Mama/Baba, kumuheshimu au kumfurahisha mmeo/mkeo utashangaa tatizo lililodumu kwa miaka nenda rudi linatoweka bila hata kufunga na kuomba au kuombewa. Kol 3:18-19 na Efeso 5:22-29.




Hata mtoto ukiinua kiwango chako cha Ibada utashangaa namna utakavyopata kibali mbele ya wazazi wako. Kol 3:20. Pia hata vijana wengi kutokupata/kutokuoa au kuoelewa leo makanisani, ukifuatilia sana kiwango chao cha Ibada kipo chini, hebu kijana - askari wa Kristo nenda kaongeze kiwango chako cha Ibada utashangaa utakavyoa anza kutafutwa kila mtu atatamani kuwa karibu yako. Rejea kwa Yesu, popote alipo kwenda watu walimtafuta na kumfuata. Soma Luka 21:38 na kitabu cha Marko.






Kumbuka:
Tuliumbwa na kuokolewa kwa ajili ya Ibada - kumwabudu Mungu na kumtumikia.
Ebrania 12;28, Rumi 12:1, Efeso 1:3, Kutoka 10:24-29, Uf. 22:3.





Sifa za jumla za mwabudu - mtoa Ibada wa Kiroho na Kweli (True Worshiper).
Awe na imani juu ya Mungu. Hebr 11:6.




Aisha maisha mtakatifu (maisha safi) Zab 24:3-4, 1Kor 3;16, Math 5:8.






Kumbuka:
Msingi wa Ibada ya kweli inayokubalika ni USAFI. Zab 24:3-4 na Yoh 4;23.





Mungu akubariki kwa kusoma somo hili nina imani kuwa limebadilisha maisha yako nakuinua kiwango chako cha Ibada. Basi kama hivyo ndivyo; wasidie na wengine kuzijua kweli hizi ili tulijenge kanisa la Kristo. Kumbuka kupata maarifa na ujuzi na kisha usiutekeleze/kuutendea kazi huko sio kujifunza. Yak. 1:22 na Math 7:24-27








Uishi Milele


2Kor 13:14







SOMO: KIONGOZI BORA WA KIROHO [KIKRISTO]




MWL: MWINJ & MCH. SONGWA .MM. KAZI.


SIMU: 0757 – 567899/ 0789 – 567899/ 0719 – 968160/ 0779 – 597066


TAG – KONGOWE – FOREST P.O. BOX 70983 DAR ES SALAAM.


Email: songwak@yahoo.com. ptrsongwak@gmail.com





YALIYOMO:
Utangulizi.
Maana ya Uongozi.
Maana ya Kiongozi.
Tofauti ya kiongozi wa Kiroho na wa Ki - dunia.
Umuhimu wa Uongozi/Kiongozi.
Sura ya Uongozi/Kiongozi wa kiroho.
Maadili ya Kiongozi wa Kiroho.
Changamoto za Kiongozi/Uongozi.
Mafao (Thawabu), Gharama na Anasa za Uongozi.
Siri ya mafanikio ya Uongozi wa Kiroho.
Kiongozi mwenye maono na malengo na mipango.
Aina mbili ya Kiongozi.
Kiongozi anayefaa kuigwa na watu.
Misingi ya Kiongozi/Uongozi wa Kiroho.
Lugha ya Kiongozi.
Sifa za jumla za Kiongozi wa Kiroho.
Wajibu wa jumla wa Kiongozi wa Kiroho.





01. UTANGULIZI.


Je, Kiongozi anahitajika? Nini umuhimu wakuwa na Kiongozi?


Je, Unajua tofauti kati ya Uongozi na Utawala?


Je, Wewe ni kiongozi au Mtawala?



Popote unapoona kazi ya Mungu imesonga mbele na kufanya vizuri lazima kuna kiongozi aliyesimama kwenye nafasi yake vizuri.




Imekuwa ni tabia ya Mungu mara zote kumchagua mtu ili kuyafanikisha malengo na mipango yake.






Mfano: Mungu alimuandaa Ibrahimu na kumwita ili kuanzisha Taifa - Mwanzo 12: 1-2; Akamwandaa Yusufu ili kulihifadhi Taifa hilo - Mwanzo 45: 3 - 9, 50: 20 - 21. Akamwandaa Musa ili kulitoa Taifa hilo Utumwani - Kut.3:2-14. Akamwandaa Joshua kuliongoza Taifa hilo kuteka nyara, kupigana vita na kuliingiza Kanani - Yoshu 1: 1 - 9. Mungu alitumia wanaume na wanawake katika kufikia malengo yake kama vile Nabii Debora - Amuzi 4:4, Esta 7: 3 - 6 n.k.
Pia Mungu aliwaongoza na kuwaelekeza waamuzi na wafalme katika kulisimamia kundi lake (watu) wa Mungu, pia aliwatumia Manabii ili kuwaonya na kuwasahihisha watu wa Mungu; Na hatimaye alimtuma mwanaye wa pekee mpendwa Yesu Kristo kuja kufa na kufufuka kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu kutoka katika utumwa wa dhambi - Yoh. 3:16, Math. 1:21.



Yesu naye alipoondoka akamtuma Roho Mtakatifu ili atuongoze salama - Yoh. 14: 16,26, Rumi. 8:14




Jambo la pekee katika ufalme wa Mungu, mtu mmoja anaweza akaleta/akasababisha ushindi mkuu katika kanisa au Huduma. Hii ni ajabu Mungu anasema katika Ezek. 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakaye tengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.”






Kumbuka:
Hitaji kubwa la nyakati zote tangu vizazi na vizazi, katika watu wa kada zote, jamaa, Taifa, Mataifa, Taasisi na Mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza wengine, pia wenye uwezo na hekima katika kuwaunganisha watu ili kuwafanya kuwa wamoja katika kutumia karama, vipawa, talanta, huduma na rasilimali walizonazo kwa manufaa ya maendeleo yao. Pia waweze kufikia na kukamilisha jambo/malengo na mipango yao waliyokusudia.





Viongozi wanajua wanalopaswa kulifanya na wana uwezo wa kuwachukua watu mbele zaidi ya pale walipo sasa.





*MAANDIKO YA SOMO LA MSINGI*


Marko.10:45, 1Petr.2:21, Yoh.10:10 - 11





02. MAANA YA UONGOZI.
Uongozi ni hali/tendo la kuongoza.
Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani.





03. MAANA YA KIONGOZI: Mark.10:45, 1Tim.4;11 - 12, 1Petr.2:21.
Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo.



Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (shawishi) wengine wamfuate.




Ni mtu aliyepewa dhamana (aliyeaminiwa) na Mungu kuongoza watu wengine (kuwatumikia). Mfano: Yesu - Yoh.14:6; 10:2 - 4, Paulo - 1Kor.11:1; 4:16.




Ni mtumishi (mtumwa) wa wale anaowaongoza.

Mfano: Musa - Kut.10:25 - 26; 13:21 - 22, Yuda - Mw.46:28








Kumbuka:


Kiongozi wa Kiroho siyo mtawala (boss) bali ni mtumishi (mtumwa).


Kiongozi ni kielelezo (mfano) wa kupigiwa, kufuatwa na kuigwa na wengine - Unaosimama mbele yao kuwaongoza.





Hivyo maisha ya kiongozi lazima yawe kielelezo katika maeneo matano (5) yafuatayo:-
Katika Usemi: Chunga (angalia) sana matumizi ya ulimi (yale uyasemayo).


Yakobo 3:1 - 12.
Katika Mwenendo: (Tabia) - Maisha yako ya kila siku machoni pa watu.


Math.5:16, 1Petr.2:11 - 12, Fil.2:14- 16.
Katika Upendo: Kujitoa, kujali, kuhudumia na kuhurumia. Yoh.3:16,


Math.9:35 - 38.
Katika Imani: Maisha ya kumtegemea Mungu. Ebr.10:38; 11:1,6,


Hesabu.14:11, Yer.17:5 - 8, Rumi.1:17, Gal3:11.
Katika Usafi: Maisha Matakatifu - yenye ushuhuda mzuri mbele za watu.


Zb.16:3, Kumb.23:14, 1Kor.3:16 - 17, 1Petr.1:16.





04. TOFAUTI YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO NA WA KIDUNIA.


Uongozi wa Kiroho na ule wa kidunia unaweza ukafanana katika baadhi ya mambo Fulani tu, lakini ukatofautiana sana na kwa kiasi kikubwa katika mambo ya kimsingi.


Kwa mfano katika mambo yafuatayo:-





i) Hitaji na namna ya kumuandaa Kiongozi.
Mungu huandaa na kumweka Kiongozi. 1Sam.16:3,7 Ezek.16:1 - 5, 1Tim.3:1,15 Yer.3:15 Math.9:38.





ii) Nia ya ndani ya Kiongozi.
Swali la kimsingi la kujiuliza, Kwanini wewe ni Kiongozi? au kwanini unataka kuwa Kiongozi?
Zipo nia mbalimbali kama vile kutaka:- mamlaka, sifa, kuheshimiwa, utukufu, kutambulika, kiburi n.k.


*Hizo ni nia za Kiongozi wa Kidunia*
Pia mtu anaweza kuwa kiongozi kwa nia ya kutaka kuyafanya mapenzi ya Mungu. FIlipi.2:5, 13.


Kumbuka:
Uongozi wa kidunia unadhihirishwa katika nia binafsi katika kupata mafao yenye kumnufaisha yeye na familia yake, kupata marupurupu mazuri, heshima; bila kujali wengine kama wanaumia au la, hivyo watu wanapigania kuwa viongozi katika kutoa rushwa kwa nia ya cheo na siyo huduma itakayotolewa au utendaji.



Uongozi wa Kiroho, Mungu anasema “Msitende neno lolote kwa kushindana wala majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Fip.2:3 - 4.






iii) Kutaka mapenzi ya Mungu. Rum.12:2, Efe.5:17, 1Tim.3:1
Nia yake ya moyoni ndiyo itakayobainisha kama atakuwa wa Kiroho au wa Kidunia.





Kumbuka:
Kiongozi wa Kiroho, yeye ni kiungo au mpatanishi kati ya Mungu na watu anaowaongoza.



Mfano: Musa - Kutoka.19:9; 24:3, Yesu - Yoh.8:26 - 30, Paulo - 2Kor.5:18 - 20.






05. UMUHIMU WA UONGOZI/KIONGOZI.


Tumeona uongozi ni muhimu sana mbele za Mungu na kwa watu pia.





Uongozi ni kipawa (zawadi) ya Mungu kwa wanadamu ili wakae katika amani, utulivu na matumaini. Bila uongozi watu hukosa mwelekeo (dira) na amani, hivyo hufikia hatua ya kufarakana, kutawanyika, kukosa mwelekeo, kila mtu kwenda au kutenda lile analoona linamfaa yeye machoni pake. Rejea baada ya Yoshua kushindwa kuandaa kiongozi, pindi alipokufa wana wa Israel walipoteza mwelekeo kabisa, kila mwamuzi aliibuka na mfumo wake kwani hakuwepo kiongozi. Kwa sababu hiyo Mungu ameweka Uongozi ili watu wapate mwelekeo, amani na matumaini katika kuyatimiza mapenzi yake duniani. Tazama Amuzi. 21:25 watu walijiendea hovyo hovyo, Zek. 13:7 - Nitampiga Mchungaji. Hesabu. 27:15 - 23, Efeso. 4:11 - 13.





06. SURA YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO.


Yapo mambo mengi ya kuangalia au yanayotakiwa kuonekana ndani ya Uongozi wa Kiroho ila haya matatu ni ya msingi sana kutupa sura ya kiongozi wa kiroho:-





i) SURA YA UTUMISHI:


Mark. 10:45, Lk. 22:24 - 27, Math. 20:24 - 28, Yoh. 13:1 - 17 (mst 14, 17)
Je, wewe ni kiongozi wa aina gani?
Mimi ni Kiongozi ninayeongoza.
Mimi ni Mtumishi ninayetumika.
Mimi ni Kiongozi Mtumishi.
Mimi ni Mtumishi Kiongozi.



Mtumishi Kiongozi:



Hii ni falsafsa (msemo/imani) inayowasaidia watu kuwa na dhana ya utumishi; na baadaye kuweza kuongoza kwa nia ya kuwatumikia watu, shirika, kanisa, n.k.





Mtumishi kiongozi anaweza asiwe na cheo/nafasi yoyote kanisani na bado akawa tegemeo (nguzo) kwa kanisa au watu wengi na kutoka kwake watu wanaweza kupokea hazina njema.





Mchungaji wangu kiongozi Rev. Victor Tawete wa TAG Kongowe Forest siku moja alisema katika fafanuzi yake ya neno mtumishi kuwa “Kipimo cha mtumishi ni kiwango cha mtumishi (mhudumu) wa Hotelini, maarufu kama waiters hata kama akitumwa vipi hakwaziki na wala hakasiriki, akaongeza akisema mtumishi kiongozi ni Yule anayetumiwa na watu wengine kwa kadri wapendavyo wao.”





Neno la Mungu linaonyesha maneno ya msingi na yenye hekima katika utumishi kama ifuatavyo:-


Lk. 22:26 - 27, Math. 20:26 - 28, 1Petr. 5:2 - 3.
Tabia ya Mtumishi Kiongozi.
Mnyenyekevu - Math. 10:24, 2Tim. 2:25, 1Petr. 5:5 - 7.
Ana bidii - Si mvivu - Math. 24:45 - 47.
Ana uwezo wa kufundisha - 2Tim. 2:24.
Mvumilivu - 2Tim. 4:2.
Mtii - Efeso. 6:5 - 6, Tito. 2:9.
Anajitoa - 2Sam. 15:21.
Mwangalifu - 1Sam. 22:14.
Amejaa Roho Mtakatifu - Mdo. 2:16,18.
Anakubali Maonyo - Mhubiri. 4:13.








II) SURA YA UCHUNGAJI:

Zab. 23, Yoh. 10:11; 21:15 - 17, 1Petr. 5:2 - 3.



Kiini cha Uchungaji:

Neno Mchungaji lilitumika sawa na mchungaji wa kondoo, ng’ombe au mifugo mingine. Yer. 6:3, Math. 8:33



Mchungaji hukaa na kondoo na kazi yake muhimu ni kuwa na kondoo hizo.






Kumbuka:
Kondoo ndiyo wanampa kazi ya kuwa mchungaji, hivyo mchungaji ni mtumishi wa kondoo (watu).



Sifa ya Mchungaji:

Anawajua kondoo wake kwa majina - Yoh. 10:3, 14, 27. Sawa na Haruni juu ya wana wa Israel - Kut. 28:9, 10, 12, 29.



Yuko pamoja na kondoo au anapatikana na ni rahisi kuingilika Lk. 22:27.

Anatangulia mbele kuwaonyesha kondoo njia, mahali pa malisho, majani na maji.. Zab. 23:1 - 2.



Ni jasiri na yuko tayari kujitoa kwa ajili ya kondoo. Yoh. 10: 10 - 13.




Anawaongoza na kuwaelekeza kwa upole kwa fimbo ya kichungaji. Zab. 23:4, Ufu. 21:15.




Ili kutimiza wajibu wake kwa kondoo (washirika/kanisa):

Kiongozi wa sura ya mchungaji anapaswa kujua mambo makuu matatu,


nayo ni:-


i) Kwamba ameitwa na Mungu - Yh. 15:16.


ii) Kufahamu chanzo cha nguvu zake - Kol. 1:11, 29. Zek.4:6.


iii) Kufahamu mambo aliyoitiwa kufanya, na hata jinsi ya kuyapatia vipaumbele -


Yoh. 10:4.



Mambo hayo humfanya mchungaji kuwa na maono, malengo na mipango mizuri katika uongozi (kazi), huduma yake. - Kol. 1:10, Efes. 4:1.




Mchungaji anapaswa kuhakikisha kuwa kundi lake:-

Linaongezeka kiidadi - Mdo. 2:47, 41: 6 - 7.
Linakuwa kiroho - Mdo. 2:42, 2Kor. 2:14, Kol. 1:10.
Linamwabudu Mungu katika Roho na kweli - Yoh. 4:24, 2Kor. 4:24, 2Kor. 4:2.
Linahifadhi umoja wa roho na ushirika katika mwili wa Kristo - Fil. 1:27, Efe. 4:1 - 6.
Linashuhudia ulimwengu habari njema na kuwaleta watu kwa Kristo (Uinjilisti) - Mdo. 5:42; 6:7, Math. 20:18 - 20.
Linapata ulinzi, usalama na amani - Mdo. 20:28 – 31



Tahadhari ya Mchungaji (kiongozi) kama kuhani wa Mungu ni kuona kuwa:-

Asiwe sababisho la kundi kutawanyika katika uongozi wake. Yer.23:1 - 2, Ezek.34:2 - 5, 10.



Hapotoshi mafundisho ya kweli ya Mungu; yaani hafundishi kwa nia ya kudanganya kundi kwa manufaa yake binafsi. Ezek. 22:26, 30, Tito. 2:7 - 8, Ezek. 13:1 - 7, Isa. 10:1- 3, Yer. 14:14, Isa. 30:10, Yer. 23:21 - 22, 2thes. 2:9 - 12.




Anatoa malisho kwa kundi kama unavyokusudia na kwa wakati unaokubalika. Yer. 23:22, Math.24:45 - 46, 2Tim. 2:15, 2Tim.4:5.






Kumbuka:


Kwa kuyafanikisha haya mchungaji (kiongozi) lazima azingatie yafuatayo:-
Maombi na (b).Kusoma neno la Mungu na kulitafakari kila wakati. Math. 17:20 - 21, Yoh. 15:7, Fil. 4:16, 1Thes. 5:17, Kol. 3:16, Yoh. 17:14 - 17.





III. SURA YA UWAKILI.
Math. 25:14, 1Kor. 4:1 - 2.


Wakili: Ni mtu yeyote anayepewa uwezo na mtu mwingine ili kusimamia mambo yake.


Wakili: Ni mtu anyemtetea mtu mwingine mahakamani.
Katika Agano jipya wakili ni mtu aliyeaminiwa na bwana wake; na hivyo alipewa mafao na mamlaka na pia alikuwa na wajibu na uwajibikaji kwa kazi yake. Lk. 12:42 - 43.





Wajibu wa Wakili ulikuwa ni:-
Kuangalia vipawa katika maisha ya wale anaowaongoza ili avitumie vizuri na kuzalisha. 2Tim. 1:14, 1Tim. 1:18 - 20.





b) Kuhesabu rasilimali zote alizonazo, kama vile watu, fedha, vifaa na kwa neema ya


Mungu kuweza kupanga na kuvitumia ipasavyo.





c) Kuwa mkweli (honesty) - mwenye msimamo mwema mwadilifu (integrity) na


muwazi (transparency) - Yoh. 8:12.



Kuwa mwaminifu (faithful) na mwenye kupandishwa daraja kwa sababu ya



uaminifu wake. - Math. 25:21, 1Kor.4:1 - 2, Math. 24:45 - 47.





07. MAADILI YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO.
Maadili ni tabia njema ya mtu au mwenendo mwema (mzuri) wa mtu.
Tabia - Ni mazoea ya hali Fulani au vitendo fulani.
Maadili ni jambo linaloweza kutenganisha sifa za kiongozi katika mwonekano wake kati ya uongozi wa Kiroho na wale wa kidunia.
Maadili yapo hasa kuonyesha msimamo katika usafi wa maisha na haki.


1Kor. 10:23, 6:12.





Swali la kujiuliza;
Unajisikiaje kwa yale unayoyafanya mbele za Mungu na wanadamu?.





Je, ni sawa au si sawa?
1Tim. 3:2 - 12.


Neno la Mungu linaeleza maadili ya msingi kwa kiongozi wa Kiroho ya kuwa anapaswa awe mtu wa:-


Kutolaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, na busara, mtaratibu, mkarimu, mwenyekujua kufundisha, si mlevi, si mpiga watu, si mtu wa majadiliano, si mpenda fedha, mwenye kusimamia nyumba yake, si mchanga kiroho, mwenye ushuhuda mzuri nje, si mwenye kauli mbili, asiyetamani fedha ya aibu. Tito. 1:6 - 7.





Kumbuka:
Maadili yanatusaidia kuishi maisha ya mfano au kielelezo. Tazama


Tito. 1:8 - 9, 2Thes. 3:9, 1Tim. 4:12, 1Sam. 12: 2 - 5.



Unayoyafanya yatageuza watu zaidi ya yale unayoyasema.




Unavyoishi itasaidia kukazia mafundisho yako au pia kuyaondoa kabisa mioyoni mwa watu wanaokutazama.



Kumbuka:
Watu hujifunza zaidi kwa kuona, kisha kwa kusikia na kwa kiasi kidogo kwa yale mengineyo.



Maadili bora (mema) ni uamuzi na misimamo inayoweza kumfanya mtu binafsi au jamii iweze kuishi maisha ya haki, utaratibu na usafi.






Hebu tuangalie mfano wa watu (viongozi) hawa wawili:-


a) Sauli:
Yeye aliitwa na Mungu kuwa mfalme, alipakwa mafuta na kutumiwa na Mungu; Lakini:- 1Sam. 13:13 - 14
Alikuwa mtu wa kutenda bila kufikiri, aliweza kutoa sadaka kinyume na utaratibu wa Mungu.
Alikuwa mtu wa kutumia mabavu (ubabe - nguvu), kiburi kutotii na kupenda umaarufu. 1Sam. 15:12 - 26.
Na mwisho wa yote aliishia kuanguka na kukataliwa na Mungu. Tatizo lake alijiwekea maadili mabaya, ambayo hayakumpa Mungu utukufu.


1Sam. 15:10 - 11.





b) Nehemia:
Katika Neh. 5:14 - 19 hapa Nehemia anaonyesha msimamo wa haki, kama maadili (tabia) yake binafsi.
Alikusudia kufanya yaliyo mema na ya haki Mst.14
Alijitenga na watu walio wadhalimu (waovu) Mst.15
Alijitoa na kukaza macho yake kwenye kazi ya kuujenga ukuta - Mst.16
Nehemia alikuwa na uwezo wa kuwavuta wengine (nguvu ya ushawishi).
Alitoa mali zake kusaidia wengine - Mst.17
Alitanguliza maslahi ya wengine kwanza, badala ya faida yake - Mst.17 - 18.
Alionyesha kuwajibika kwa Mungu akimpa utukufu - Mst.19


Nehemia. 12:40 - 43.





Kukosa maadili mema kunajidhihirisha katika mambo yafuatayo:-


i) Maisha ya uasi kwa kiongozi kama vile wana wa Israel:
1Kor. 10:1 - 5.
Kutamani mabaya - 1Yoh. 2:15 - 17.
Kuabudu sanamu na shughuli nyingi - Mark. 4:19, Kut. 20:4 - 6.
Uasherati - Gal. 5:19.
Mawazo potovu.
Uhusiano mbaya (ugomvi) kati ya mke na mume (wanandoa).
Kukosa hekima katika kushauri/kushuriana.
Kumjaribu Bwana - Lk. 4:12
Manung’uniko - Hesabu. 14:26 - 27
Kiburi - Majivuno (kujiona wewe bora kuliko wengine) - Mith. 22:10.





Kumbuka:


Anatazamiwa kiongozi ya kuwa:-
“Alivyo kwa nje na ndivyo anavyotakiwa awe kwa ndani.”
“Vile anavyokuwa madhabahuni/mbele za watu anatakiwa awe pia mbele za familia yake.”





ii) Maisha mabaya katika fedha:
Kupenda fedha kuliko Mungu - 1Tim6:6 - 10.
Kutumia vibaya fedha za kanisa - Fil. 4:11 - 12.
Udanganyifu katika matumizi - Mith. 15:27, Rumi. 13:8.
Kutotoa fungu la kumi (Zaka) 10% ya mapato yako - Mal. 3:8 - 9, Ebr. 7:5 - 10, Zek. 5:1- 4.
Uzembe wa kutolipa madeni - Zab. 37:21, Mith.22:7


Kumbuka:
Hali hii inapozoeleka kwa kiongozi inasababisha hali ya kutokuaminika na kuonewa shaka.


iii) Matatizo katika ndoa:
Matatizo haya yanaweza kusababishwa na:-





a) Unafiki:
Nje kuonekana tofauti na hali halisi ya ndani.
Kuvaa sura isiyo yako.
Kuficha au kufanya siri shida na matatizo ya kindoa - Math. 23:27 - 28.





b) Kutokutatua matatizo madogo madogo ya ndani; na hivyo huzaa matatizo


makubwa - Lk. 16:10.





c) Kujilinganisha na watu wengine (ndoa nyingine):
2Kor. 10:12


Mwanandoa yeyote anayejilinganisha na mtu mwingine hana akili kabisa - zezeta.


Kumbuka: Tofauti zetu zinamfurahisha Mungu, siri ya ndoa bora ni msingi wake.





d) Dharau/Kiburi - 2Tim. 3:1 - 4.


e) Mawasiliano mabovu - Amos. 3:3





Kumbuka:
Adui hatakubali na hafurahi kuona mnaishi hivyo anachofanya ni kuwachafulia mawasiliano, msimpe nafasi. Efes. 4:27


f) Kipato/Fedha kidogo:


hili nalo huweza kuleta tatizo katika ndoa nyingi, hivyo kama mwanandoa jifunze kuridhika na uwezo wa mwenzi wako huku mkiweka mipango na malengo pamoja ili kuinua kiwango cha fedha na uchumi katika familia. Fil. 4:11 - 13.





g) Tabia za asili za mwenzi wako - Mith 30:11 - 14.


Hivyo ni vizuri wanandoa ukamjua mwenzako vizuri hasa juu ya tabia zake za asili - ndani, wakati wa uchumba huwezi kuziona tabia za ndani bali za nje.





h) Viwango vya tendo la ndoa
Mith. 5:15 - 19, Wimbo. 4:12 utoshelevu.





Swali la kujiuliza:
Je, unaujasiri wa kuhubiri mbele ya mkeo au mumeo na pia watoto wako? Kama unakosa ujasiri mbele yao basi, kunamambo yanayohitajika kupata ufumbuzi.


j) Kuacha kutunza familia kwa kisingizio cha kutingwa na huduma - Lazima


kuwe na uwiano, japo ni muhimu sana kumsikiliza na Roho Mtakatifu


kuliko kutii wanadamu -
1Tim. 5:8, Mdo. 5:29.





iv) Kuharibu huduma yako; kwa:-
Kupotosha neno la Mungu, kulighushi na bila ya kutumia kwa halali neno la kweli.
2Kor. 4:1 - 2; 2:17, 2Tim. 2:15.
Kuwatumia watu kwa kujinufaisha yeye binafsi badala ya kuwajenga na kuwaimarisha katika ufalme wa Mungu.





*Faida ya maisha na maadili mema ya Kiroho*
Ili uwe kiongozi, lazima uwe na wafuasi. Kuwa na wafuasi lazima wakuamini. Hivyo maadili bora ni ya lazima kwani yanakuwezesha wewe kiongozi katika mambo yafuatayo:-
Kurithisha (influence) tabia yako kwa wale unaowaongoza. Math. 26:73, 1Tim. 4:12.
Kutokuwa mtu wa kubadilika kama (kinyonga/popo).





Swali la kujiuliza;
Je, wewe ni yeye Yule kila wakati?
Je, jambo gani unafanya ambalo hutaki watu walijue?
Je, hii ndiyo tabia yako? 1Tim. 3:8.





Kumbuka:
Tabia yako isiyobadilika inagusa mioyo ya watu - Ebr. 13:7
Dhamiria kuwa mkweli na muwazi, usitafute kuonekana mzuri, bali uwe mzuri. Yer. 7:3 - 4.
Tabia huweza kujengwa na kubomolewa katika mambo madogo, hivyo dhamiria kuwa mwaminifu katika yaliyo madogo na utakuwa mwaminifu dhidi ya mambo yaliyo makubwa.
Unaweza ukabadili matendo yako ili yafuatane na kanuni za maadili mema au unaweza ukabadili kanuni za maadili zifuatane na matendo yako. Uchaguzi ni wako.
Dhamiria kuwa na nia ya kutumika kwa unyenyekevu, watu watakufuata wakijua nia na lengo lako ni kuwatumikia.





08. CHANGAMOTO ZA UONGOZI/KIONGOZI.
Hitaji kubwa la kanisa ni kupata viongozi bora wa kiroho watakaoweza kukabiliana na changamoto zilizopo nyakati hizi za mwisho katika kumwakilisha Kristo. Je, wewe ni miongoni mwao? - 1Tim. 3:1 - 7.





Swali: Utafanya nini wewe binafsi ili kuboresha uongozi wako?





Changamoto nyingine za kiongozi ni:-
Kiwango duni (cha chini) cha elimu na ufahamu sahihi wa neno la Mungu na mambo mengine - Mith. 3:13; 4:13.
Maisha yasiyo na ushuhuda mzuri. Math. 5:13 - 16
Kushindwa kufikia malengo/maono. Lk. 14:28 - 32.





09. MAFAO (FAIDA) NA THAWABU, GHARAMA NA ANASA ZA UONGOZI/KIONGOZI BORA WA KIROHO.
Uongozi una mafao/thawabu, gharama na anasa zake. Anasa ni pamoja na vikwazo vilivyomo.





I) {a} Mafao (Faida) & Thawabu ya Uongozi:-
1Thes. 5:12 - 13, Ebr. 13:17, 1Petr. 5:2 - 4, 1Kor. 9:10.
Heshima katika jamii - (Social Status).
Kutambuliwa na kueleweka - (Recognitation & Position).
Mapato (Material gain).
Mamlaka (Power & Authority).
Kuwa na mvuto kwa watu (Influence).
Mafao ya Kiroho (Spiritual Benefits).
Taji ya utukufu (Glorious Crown) Dan. 12:3 na 1Kor. 15:41.
Kupata kibali kwa Mungu na kwa wanadamu (God’s favour) - Mith. 3:3 - 4.





{b} Kuongoza vizuri mafao/faida ya uongozi:
Hesabu 27:12 - 23.
Ni jambo la msingi na lakuzingatiwa sana kwa kila kiongozi aliyepata kibali cha kuongoza kuyafanya haya:-
Uuone uongozi kama dhamana.
Uwe na nia ya Utumishi.
Jifunze kutofautisha kati ya mambo yako binafsi na cheo.





Kumbuka:
Panga maisha ambayo unaweza kuishi bila cheo.
Wekeza kwa ajili ya siku za mbele.
Uwe tayari kumpisha mwingine kuchukua cheo au nafasi yako.





Kumbuka:
Kuandaa Kiongozi/Viongozi (mrithi/warithi) watakaoendeleza mbio za uongozi hata wakati ambao hautakuwepo.





Mfano: Eliya, kabla ya kuondoka alimwandaa Elisha. 1Falme. 19:15 - 21.
Musa alimwandaa Joshua. Hesabu . 27:12 - 33.
Paulo alimwandaa Timotheo - 2Timotheo. 2:1 - 3.
Mwamini Mungu katika nafasi uliyonayo. Yosh. 1:6 - 9.


II) {a} Gharama za Uongozi.
Math. 5:11 - 12, Yoh. 10:11, Lk. 15:4, Yoh. 15:3, 1Sam. 17:35 - 37.
Kujitoa muhanga kwa ajili ya wengine (kondoo) - (Personal sacrifice).
Mateso ya kibinafsi - Kutokana na hisia mbalimbali.
Kukataliwa, kukatishwa tamaa, kuchekwa, kuzomewa, kulaumiwa, kudhalilishwa.
Matatizo ya ndoa na familia (kutengana kimajukumu)
kusingiziwa, upweke, shutuma, chuki, kusingiziwa, kusemwa, kuudhiwa.
Kuingiliwa katika maisha kwa mambo binafsi.
Kuwa tayari dhidi ya majaribu yatokanayo na fedha, zinaa (wanawake/wanaume) na utukufu (sifa) na matumizi mabaya ya madaraka n.k. 1Petr. 4:14; 2:20, Zab. 89:50 - 51.





{b} Kukabiliana na Gharama za uongozi.
Mjue sana Mungu na kumpenda - Fil. 3:8 - 10, Ayu. 22:21.
Jiandae kukabiliana na gharama hizo - Fil. 1:27 - 29.
Tumia muda wako vizuri kwa mambo yote, yaani uwe na kiasi.


Kol. 4:5, Efes. 5:15 - 16.
Uwe tayari kuwajibika.
Uwe mtu wa maombi, ili kumshirikisha Mungu mambo yote na kumtegemea.


Zab. 37:2 - 7, 23.
Jaa neno la Mungu - Kol. 3:16.
Jaa Roho Mtakatifu - Efes. 5:18.
Inua kiwango chako cha Ibada - Yoh. 4:23 - 24.
Kuishi maisha safi - Matakatifu yenye ushuhuda mzuri. Math. 5:13 - 16.





III) {a} Anasa au majaribu (vikwazo) vya uongozi:


Anasa ni mambo ya starehe yasiyo ya lazima.
Uongozi huambatana na anasa zake ambazo ni mitego na majaribu kwa kiongozi.





Baadhi ya majaribu hayo ni:-
Kujiona umefika juu ya kilele (kiburi) - Isa. 14:13 - 14, Mith. 29:23.
Kushindwa kuwa na maono - Mith. 29:18.
Kuacha kuwa mfano wa kuigwa.
Kutumia madaraka/Uongozi kwa faida binafsi.
Kukataa kujipima mwenyewe - Gal. 6:4 - 5.
Kuridhika na utendaji usioridhisha.
Kutumia vibaya madaraka/uongozi kwa watu unaowaongoza.
Zinaa/Uzinzi/Uasherati.
Kujisifu na kujiinua (sifa) - Fil. 2:3, 14:16.
Wivu.
Kutokujali familia.
Kukosa motisha na kuahirisha mambo.
Kujisikia huwezi na hufai (kujidharau na kujikataa) - Hesabu. 13:32 - 33.
Kupoteza dira ya uzima wa milele.
Fedha - 1Tim. 6:10. na yanayofanana na hayo.





{b} Namna ya kukabiliana na Anasa, mitego na majaribu ya Uongozi:


Soma maandiko haya:- 2Tim. 4:15 - 16, 1Thes. 4:1; 5:17 - 18, Fil. $:6 - 7. Hivyo ni lazima:-
Kukaa katika maadili mema ya Kikristo.
Kudumu na kutii neno la Mungu.
Kudumu katika maombi - Mith. 16:3, Lk. 18:1 -
Kuhusisha mambo yako kwa walio karibu nawe, watu au timu yako ya Uongozi kwa ushauri. Mith. 20:18, Mith. 15:22.





10. SIRI YA MAFANIKIO YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO:
Pamoja na kuwa na maadili bora mambo yafuatyo ni muhimu sana kwa kiongozi ili aweze kufanikiwa:-


i) Kumwamini na kumpenda Mungu - Yoh. 14:1, 12, 21, 23.


ii) Kufanya mapenzi ya Mungu - Math. 7:21, Efes. 5:10, Yoh. 5:24.


iii) Maombi - Lk. 18:1, 1Tim. 2:1, Lk. 6:12, Mark. 1:35 - 39, Ebr5:7 - 10, Ezr. 8:21 - 23.


iv) Kuwa na mipango mizuri - Lk. 14:28 - 32, 1Tim. 3:15.


v) Kujali rasilimali ulizonazo pamoja na muda na watu - Kut. 10:24 - 26, 8, 9, Lk. 22:35 - 36, Efe. 5:15 - 16.


vi) Mahusiano bora na wengine wanaokuzunguka - Ebr. 12:14 - 15, Yoh. 13:34 - 35..


vii) Usiridhike na ulichonacho tamani kujifunza toka kwa wengine - Mith. 2:3 - 6, Mith. 12:9 -





11. KIONGOZI MWENYE MAONO NA MALENGO:
Mithali 29:18.


Ipo tofauti kubwa kati ya Maono na Malengo





(A) MAONO NA MALENGO:


MAONO:
Ni ule uwezo wa kupata picha ndoto/dira/ufunuo ya mambo ya siku za mbele; ambapo MALENGO: Ni ile namna ya kuyatekeleza hayo maono uliyoyaona au uliyoyapata.
Ni kufanya safari toka kwa unayoyaona sasa kwa yasiyofahamika na kuyaona kama yapo katika uhalisia.


Watu wengi wanakwama kwani wanadhani kitu cha muhimu ni fedha, hapana cha kwanza ni kuwa na maono pesa ije iingie kwenye hayo maono. Pesa bila maono itapukutika yote. Rejea kwa Yusufu aliingia Misri kama mtumwa, hana kitu, lakini alikuja kuwa mtawala kwa sababu alikuwa na maono.





Mfano:
Nuhu aliona mapema gharika juu ya uso wa nchi akawaonya watu wake. Mwa. 6:13 - 22.
Yusufu aliona miaka saba ya njaa kabla ya kutokea. Mwa. 41:28 - 30.
Musa aliona nchi ya ahadi - Kut. 3:3 - 9.
Nehemia aliona Yerusalemu mpya - Neh. 1:2 - 6, Neh. 2:3 - 5..
Paulo aliona Makedonia inahitaji injili Mdo. 16: 9 - 10.





Swali:


Je, wewe unaona maono gani juu ya:-


{a} Kanisa? (b).Familia yako? n.k.





Kumbuka:


Mtu mwenye maono siku zote hufuatwa na kutafutwa na watu, bali mtu asiye na maono siku zote huwa mtu wa kufuata na kutafuta watu. Soma Mwanzo. 45: 3 - 10; 50:20 - 21.


(B) BAADA YA KUONA MAONO:


Ni lazima mambo yafuatayo yafanyike ili maono yawe mambo au kitu halisi na wala sio ndoto za kupita tu.
Kuhamasisha watu; Ili kuyatimiza mambo uliyoyaona. Mfano, Musa alihitaji kuwaona wazee wa Israel kwanza - Mwa. 3:16 - 18, 4:29 - 31. Hivyohivyo na Nehemia pia - Neh. 2:17 - 18.
Kuweka malengo: Yaani mipango ya utekelezaji ili kuyafanikisha maono lengwa/ husika.





Kumbuka:
Pasipo maono watu hujiendea - hupuyanga hovyohovyo na mwisho hupotea na kuangamia; Na pasipo malengo na mipango mizuri watu watashindwa kuyafikia maono, na hawawezi kuhamasika tena kuendelea mbele kuyatekeleza.



Hatimaye kila mtu atafanya anavyoona inafaa machoni pake mwenyewe. Amuzi. 21:25.






(C) MSINGI WA BIBLIA KUHUSU KUWEKA MALENGO:
Yesu alitoa mfano wa mjenzi wa mnara na mfalme aendaye vitani. Lk. 14:28 - 32.
Paulo alitoa mfano wa mwanariadha, mpiganaji ngumi, mkulima, mwanamichezo na Askari - 2Tim. 2:3 - 10, 1Kor. 9:24 - 26, Fil. 4:14, 2Tim. 4:7.
Mjenzi katika kuweka malengo inamlazimu kuchora ramani, kukusanya vifaa na rasilimali zingine, kisha kuanza kujenga hatua kwa hatua.
Mpiganaji kabla ya vita (pambano) hujiandaa, huandaa majeshi, vifaa, silaha na njia (mbinu) za kuendelea na hivyo hujipanga kikamilifu kabla ya yote, kwa nia ya kupigana.





Kumbuka:
Mpango wa Mungu wa wokovu ulikuwa na malengo na mipango yake ya utekelezaji.
Hivyo Mungu aliandaa mtu mmoja ambaye ni Ibrahimu, Baba wa Imani.
Kisha Taifa la Israel kuwepo.
Manabii/Yesu kuzaliwa awe mkombozi wa ulimwengu.
Mitume/Roho Mtakatifu/Kanisa/ Hatimaye wokovu wa milele (Uzima wa MIlele).





(D) FAIDA YA KUWEKA MALENGO NA MIPANGO:


i) Huwezesha kuwa na mwelekeo mzuri wa mambo au kazi katika maisha.


Kumbuka:
Watu wote wasio na malengo hawafiki popote.
Malengo na mipango hufanya maisha yawe ya maana na huweka mwongozo wa maisha. “Kama hujui unakokwenda, njia yoyote itakufikisha huko usikokujua.”


Hivyo kukosa malengo na mipango huo ni upofu, na shimoni lazima utatumbukia tu - Math. 15:14





Kumbuka:


“Ukilenga hewa utafanikiwa kupiga shabaha hiyo, na hakuna anayelenga hewa akaikosa.”





ii) Huhamasisha mambo kufanyika:
Viongozi wengi waliofaulu vizuri wanakiri kuwa walihamasika na malengo waliyokuwa nayo, na kujiona wakitembea kuelekea katika malengo hayo.
Ni malengo yanayowaelekeza ni wapi wawekeze na kutoa vipaumbele katika mali na rasilimali walizonazo na pia nguvu zao.


iii) Humfanya mtu kuwa na Tabia (shauku) ya kutaka kuona matokeo.
Malengo na mipango humfanya kiongozi awe na hamu/ shauku ya kuona matokeo ya kazi anayoifanya na maendeleo yake yalivyo.
Malengo yanamfanya mtu kuweka mkazo katika matokeo, badala ya shughuli zinazofanyika.





Malengo na mipango humsaidia kiongozi
Kupima utendaji na shughuli (huduma) yake.
Kujua umekwenda umbali gani? (napiga hatua au hapana)
Kuwajibika.
Kutathimini kazi mara kwa mara na kuboresha utendaji wake.


Gal 6:4 -5


Kumbuka:
Viongozi waliofaulu ni watu ambao wana malengo kwa siku za mbele. Si watu wa kushughulikia matukio tu au watu na mambo yaliyopita.



Huwa hawasubiri mambo yaotokee na ndipo wafanye kitu, bali ni watu wanaojitahidi kutimiza mambo, kwa sababu:-



i) Wana maono yaliyo wazi.


ii) Hujiwekea mipango na ratiba ya kutimiza maono hayo.


iii) Wanawajibika katika kufuatilia malengo waliyojiwekea.


vi) Huvumilia wakati maono, malengo na mipango inapokutana na vikwazo


mbalimbali na kutotimiza malengo aliyokusudia.


v) Hupata ufumbuzi na kubuni njia ya kuendelea mbele si kurudi nyuma na kukata


tamaa.





12. AINA YA VIONGOZI/UONGOZI.


Kuna viongozi wa aina nyingi, leo tuangalie mbili ambao ni:
Wale wanasababisha mambo kutokea na
Wale wanaosubiri mambo yatokee.





I} sifa za viongozi wanaosababisha mambo yatokee.
Wana mtazamo wa mbele (wana ndoto, maono, malengo, mipango) Mith. 29:18, Mwanzo 37:5-11.
Wako tayari kupanga mipango, na kuona jinsi gani watakavyoyatimiza malengo/maono hayo. Mwanzo 41:1 – 44


(Mst. 25 – 40)
Wanaweka mikakati ya kuzuia matatizo yatakayoweza kutokea. Mwz 41:33 – 36.
Hawakati tamaa na pia ni hodari na jasiri. Hesabu 14;6 – 9’13:30





II} sifa za viongozi wanaosubiri mambo yatokee.
Hawafanyi chochote/hawajishughulishi mpaka mambo yatokee.
Hutumia muda mwingi kushughulikia matukio. Hesabu 13:31 -33
Ni wazima moto na hutumia muda mwingi kuzima moto bila kujiuliza chanzo cha huo moto kutokea. Math 9:32 – 33.





Kumbuka:
Tofauti kubwa kati ya viongozi wa aina mbili hii ni Uwezo katika malengo na kujishughulisha na mipango pia mikakati mbalimbali katika kutimiza maono yaliyopo.


Kumbuka:


Maono, malengo na mipango lazima iwe Smart (safi), yaani iwe na sifa hizi:-


Spirit led & specific - Uongozi wa Roho Mtakatifu na yenye shabaha (yaliyo wazi – bayana).
Measurable – kupimika/yenye kutathiminika.
Attainable – yenye kufikika.
Realistic – yawe halisi
Time targeted – muda maalum
Soma Lk. 4.:18 – 22, 1Tm. 4:7, 1Kor. 9:24 – 26





Maono/mipango/malengo yanaweza kushindikana kufikiwa kutokana na sababu zifuatazo:-
Hayakuwa na shabaha (bayana) maalumu.
Hayapimiki.
Hayafikiki kirahisi.
Hayako halisi kibinadamu.
Hayakutengewa muda maalumu, yangekuwa na muda yangeweza kuhimizwa na kukamilishwa haraka na hivyo kufurahia matokeo yake.





Kumbuka:


Maono yako yafafanuliwe kwa maneno yako, maneno yako yazae matendo na tabia, malengo, mipango na mikakati.





Hatimaye yataonekana matokeo kamili (halisi) kutokana na mawazo uliyonayo> bila hivyo mawazo/maono uliyonayo yatabaki kuwa ndoto tena za mchana.



Hivyo kiongozi wa kiroho lazima kuwa na mtazamo wa ki Mungu, kama vile Mungu mwenye Enzi alivyo na maono thabiti tangu mwanzo hadi mwisho wa kazi yake katika ulimwengu huu na ule ujao.




Mipango na mikakati yake ya wokovu imekuwa na ushirikishwaji wa mwanadamu na kwa uwazi kabisa. Rumi 8:28.




Uongozi wa kiroho unabeba sura ya Mungu mwenyewe kwa wana wa Mungu wanaotegemea. Mith. 16:4, Rumi 8:14, Yhn. 15:6, Isa. 14:24, Math. 28:20






13. KIONGOZI ANAYEFAA KUIGWA NA WATU WENGINE.


Zifuatazo ni baadhi ya sifa/vigezo apasavyo kiongozi kuwa navyo ili watu wengine waweze kuiga kutoka kwake.



Watu huvutiwa na kumfuata kiongozi aliye na:-






I} Maono.
Kiongozi asiye na maono hafai kuwa kiongozi. Mungu humtumia mtu mwenye maono na mipango safi. Mfano Musa, Joshua n.k.



Hivyo kiongozi lazima ujue unakwenda wapi na Mungu anataka nifanye nini? Mith. 29:18



II} Mfano/Kielelezo: 1Tim 4:11 – 12, 2Kor. 3:2 -3


Mtume Paulo hakusita kuwaeleza watu kuwa wamfuate/wamuige yeye anavyofanya. 1Kor. 11:1, Fil. 3:17, Fil. 4:9, 2Thes. 3:7, Lk. 14:25.





Kumbuka:


Kuacha/kushindwa kuongoza kwa mfano mwema ndio kuzaliwa hadithi za kale, utasikia mtu anasema, enzi zetu, wakati, miaka ile tulifanya hiki na kile, lakini leo hawezi, hilo tayari ni tatizo, umeshindwa kuwa kielelezo kizuri.





III} Uadilifu: 1Sam 16:7 –


Uadilifu ni suala linalohusika na moyo wa mtu mwenyewe (tabia) yake.


1Sam. 16:7, Zab. 78:72





Kumbuka:
Unapopoteza uadilifu umepoteza uthamani na ubora (kibali) cha uongozi wako.



Uadilifu unajengwa kupitia; kufanya (kutenda) na kutekeleza ahadi na kujitoa kikamilifu.






IV} Neno la Mungu: Ebr. 4:12, 2Tim 13:17, Mdo 6;2, Ebr 13:7, Kol. 3:16, Yh 1:1 – 14.
Viongozi ni wasomi wa neno (Leaders are Readers) kwa sababu, Mtumishi wa Mungu hutegemea neno la Mungu, kumuongoza Zab. 119:105 na kumpa nguvu (chakula)
Math 4:4, Ay 23:12.
Je unafanya nini ili kujilisha neno?
Unafanya nini katika kuhakikisha wengine wanakula (pata) neno la Mungu?





V} Maombi: mdo. 6:4, Lk. 5:16.
Kama kiongozi lazima ujitoe kikamilifu katika maombi na kulihudumia neno.
Mara zote mwanadamu hutafuta njia zilizo bora zaidi.
Mungu naye anatafuta mtu (kiongozi) bora aliyeshujaa na hodari katika maombi.
Mfano Joshua akiwa vitani Kut. 17.





VI} kiongozi aliyejaa roho mtakatifu:


Mdo 6:3, Yhn. 15:5, 2kor. 3:5 – 6, 2kor 13:14, Kol.1:1 – 29.
Sisi (viongozi) bila roho mtakatifu hutuwezi kufanya chochote.





Kumbuka:
Popote palipo na kiongozi aliyejaa Roho Mtakatifu elewa kuwa nyuma yake yupo Mungu 2kor 3:5 – 6.





VII} Mwenye Bidii na Kazi: 1Thes. 5:12 – 13, kut. 2:15
Kiongozi bora, Mtumishi lazima awe na bidii ya kazi za mikono na huduma ili watu wamkubali. Rumi. 12:8





VIII} Mwenye Imani: Ebr 13:7, 11:1,6, Ebr. 10:38, Rumi 1:17.
Mwanafalsafa mmoja alisema “Ni bora kuwa na simba mmoja anayewaongoza kondoo elfu moja, kuliko kondoo mmoja kuongoza simba elfu moja.”



Kiongozi bora lazima awajibike kuwaongoza watu katika kumwamini Mungu na kumtegemea yeye (Mungu).



IX} Anayekua/Ongezeka (Mwenye Kujifunza) Yh. 8:31 – 36.


Kiongozi hayuko kamili ila mara zote yupo kwenye mchakato wa kujifunza mambo mapya katika maisha yake ya Imani.





Kumbuka:
Kiongozi aachapo kujifunza na kukua ndipo mwisho wake wa kuongoza hufika.





X} Maisha Safi ya Nyumbani: 1tim. 4:12 -16.
Mtu mmoja alisema, “ikiwa haifai nyumbani, usiiuze nje.”
Ukishindwa kusimamia nyumba yako, yaani mke/mume na watoto tayari umeshindwa kuwa kiongozi bora wa kiroho ( ki – kristo).





14. Misingi ya Kiongozi/Uongozi wa Kiroho.
Misingi ni nguzo ambazo kwazo kiongozi wamejengwa au anajengwa ili kufaa katika uongozi:






a} Kujitoa kwa
Kristo (Bwana – Mungu) – 2Kor 8:5
Watu – 9yhn 3:16





b} Utii: mwz. 12:1 – 4


Neno utii limeunganishwa na Bwana wa majeshi. Hii lugha ya kijeshi wajibu wa askari ni kutii kutekeleza amri kwanza na maelezo baadae Efo. 6:1- 2.





c} Uaminifu: 1kor. 4:1 – 2.


Kipimo cha Kiongozi ni Uaminifu Katika
Maagano.
Mahudhurio.
Muda.
Matokeo.
Ibada n.k.





d} Tabia za Kiroho/Nidhamu za Kiroho: Mdo 6:4
Maombi
Kusoma na kutafakari neno.
Ibada
Matokeo
Utumishi (Huduma)





Kumbuka:
Nguvu zetu katika huduma inategemea muda ninaokaa mbele za Mungu, kuomba na kutafakari neno lake.





e} Uwajibikaji: Mark 6:7, 30


unapokuwa kiongozi kuna maneno ya:-
Kuagiza.
Kutumwa (kuagizwa jambo)
Amri (hakuna kuhoji ni kutekeleza tu).


Kumbuka:
Ni lazima kutoa taarifa kwa mkuu wako ( Mchungaji)
Lazima uwe mtu wa mawasiliano.





f} Kuambatana: 1Sam. 18:1, 1Kor. 1:10, Math. 12:30, Ruth. 1.14 – 18.
Kuambatana ni kushikana na viongozi wenzako ili kutompa nafasi ibilisi (Adui) shetani kutushinda. Efe. 4:27.



Kutokuwa kigeugeu Mith 26:21.






Misingi ya kuambatana: 1kor. 1:10
Kunena mamoja.
Kutokuwa na faraka – matengano
Kuwa na nia moja.
Kuwa na shauri moja.



Siri ya kufikia hatima yako njema salama katika uongozi ni lazima ujifunze kuambata na wenzako vizuri, bila hivyo hutafika mbali (itakuwa kama mbio za panya sakafuni).




Nikinukuu maneno ya makamu Askofu Mkuu wa TAG Dr Magnus Mhiche alisema siku moja kuwa “ukitaka kwenda mbali nenda mwenyewe (peke yako), lakini ukitaka kwenda mbali zaidi jifunze kwenda (kuambatana) na wengine. Mfano: Gehazi alishindwa kufikia hatima yake akiwa na nabii Elisha baada ya kujitenga kushindwa kuambatana naye. 2Falme 5:20 – 27.




Pia Akani aliuwawa kwa kupigwa mawe maana hakuweza kuambatana na Joshua. Yosh. 7:9 – 25.






Kumbuka:
Ili ufike (mwisho) hatima yako lazima ujifunze kuambatana na wenzako maana wao ni walinzi wako.



Dawa/tiba ya mtu asiyependa kuambatana na wenzake ni kumtupa nje kumwondoa. Mith 22:10, Yosh. 7:1 – 25 kwani bila kufanya hivyo wote mtapigwa na adui wala hamtaweza kusimama tena.






g} Kupokea Maonyo: Mhubiri 4:13


Kiongozi bora wa kiroho lazima ajifunze kupokea maonyo/awe tayari kuonywa na kusahihishwa pale atakapo kengeuka/kosea.





H} Kuwa Balozi Wako (Mchungaji)
Jifunze kumtaja vizuri au kumnena vema kiongozi/mchungaji wako (Mkuu wa kituo) mbele ya watu pia jaribu kunukuu na kurejea mafundisho yake ukionyesha jinsi yalivyokusaidia na waimarishe watu kutokana na mafundisho yake na maono ya Kanisa hasa pale upatapo nafasi kusimama madhabahuni au katika idara yoyote na kipindi chochote Kanisani na siyo kumpinga (kumponda) na kuanzisha kitu kipya.





15. Lugha ya Kiongozi/Uongozi.
Lugha ni njia ya mawasiliano. Na ili adui awaweze na kuwashinda ni lazima kwanza aharibu miundo mbinu yenu ya mawasiliano.



Lugha pekee ya kiongozi ni KUAMBATANA. Tazama Ruth. 1:14 – 18, Amos. 3:3 na 1Sam 18:1.






16. Sifa za Jumla za Kiongozi/Uongozi wa Kiroho.


Kiongozi wa kiroho lazima awe na:-
Uwezo wa kuongoza
Mcha mungu
Mkweli
Achukie mapato ya udhalimu (utapeli) yasiyo halali (rushwa).
Mtu mwema/mwadilifu.
Amaanishe anachosema na aseme anacho maanisha.
Ajae roho mtakatifu.
Awe mvumilivu
Awe na maono (Mith. 29:78)
Apende ibada
Awe mtunza siri.
Awe mbunifu Mw 30:25 – 43, 2:15
Awe na hekima.
Awe mtu wa kujitoa
Asiwe mtu wa udhuru
Awe mnyenyekevu 1Pt 5:6, Math 8:21 – 22, 1Flm 19:20.
Awe mcheshi
Aishi maisha ya uanafunzi. Yhn. 8:31 – 36.
Anayekubali changamoto na kufanya uamuzi.
Awe amezaliwa mara ya pili. Yh. 3:3 – 8.
Awe na huruma. Lk. 7:12 – 13, Math. 9: 35 – 38.
Awe mtu mzima katika imani, siyo mchanga. 1Tim.3:6
Anayekubali ushauri. Kut. 18:13 – 27.
Awe na ufahamu sahihi wa neno la Mungu na mambo mengine Mith. 2:3 – 6. Soma Pia: Kut. 18:21 – 24, Mdo 6:3, Rumi 12:6, Mith 11:30, 2Nyakati 1:11 – 12, 1Tim 3:1 – 13, 1Falme 3:5 – 28.





17. Wajibu wa Jumla wa Kiongozi wa Kiroho.
Mdo 20:1 – 38, Yhn 10:11 – 15.
Wajibu ni majukumu (kazi) apaswayo kiongozi kuyafanya kwa nguvu zake zote ili kuyatimiza malengo yake.





Baadhi ya majukumu/wajibu wake ni :-


i} Kujitunza nafsi yake: 1Thes 5:23


Nafsi imebeba:-


a} Akili


b} Makusudi (nia)


c} Hisia


Mith. 4:23, 1Kor 15:33 – 34





Hivyo kama kiongozi lazima uitawale nafsi yako mbele ya hao unaowaongoza.





ii} Kulitunza Kundi


Ni wajibu wa kiongozi kulilinda, kulichunga na kulihakikishia usalama kundi ninaloliongoza dhidi ya:-


a} Mbwamwitu wakali: Watumishi waharibifu ambao kondoo siyo wito wao.


b} Imani potofu: Mafundisho ya uongo (Mashetani).





Kumbuka:
Hili litawezekana pale tu kiongozi atajitoa kwa kufundisha watu wake Elimu sahihi ya Imani (Neno la Mungu) – (Sound Doctrine).



Tunayapinga mafundisho ya uongo kwa kufundisha kweli ya Mungu. Yuda 1:3 – 6, Yhu 8:31 – 36, Hosea 4:6, Mith. 11:9 na Mith. 21:16






Kumbuka:


Kanisa linaangamizwa kwa kukosa maarifa, Elimu sahihi ya neno la Mungu. Hosea 4:6, Mith. 21:16.





Hali kadhalika Kanisa linapona kwa maarifa. Mith 11:9, Yhn 8:31 – 36.





Kumbuka:
Kanisa linajengwa/imarishwa na kuponywa kwa mafundisho, mafafanuzi ya neno la Mungu. Za 119:130 na wala siyo Mahubiri, kukemea maombezi.





Kumbuka:
Shetani haogopi mahubiri wala maombezi au makemeo bali anaogopa ufahamu unaomjua Mungu. Ay.22:21, Lk. 4:1 – 14.





Hitimisho:
Mungu haangalii uliipataje nafasi hiyo ya uongozi, yeye anaangalia kusudi lake la hiyo nafasi linatimia kikamilifu.



Elewa kuwa Roho Mtakatifu ndiye aliyehusika kuwatumia hao waliokuchagua au aliyekuteua katika nafasi hiyo ya uongozi uliopo.






Hivyo sasa, kuwa huwajibiki kwa mtu (mwanadamu) bali kwa Mungu moja kwa moja. Mdo. 20:28.





Elewa, kuwa kutokutimiza wajibu wako kama kiongozi haumkomoi mtu bali unatafuta ugomvi na Mungu aliyekuwa kuwa mwangalizi, kiongozi na msimamizi wa kundi lake.





Zingatia:


Itakuwa heri kwako, Bwana akikukuta ukidumu katika kuwahudumia watumwa, watu wake kwa Uadilifu na Uaminifu wote na kwa unyenyekevu kabisa; atakuweka kuwa juu ya vitu vyake vyote na usipofanya hivyo atakukatakata vipande vipande na kukutupilia mbali. Math. 24:45 – 51.














Uishi Milele.


2Kor 13:14











SOMO: MALANGO/MILANGO YA KUZIMU.



MWL. EV. & PT. SONGWA .MM. KAZI – TAG – KONGOWE FOREST P.O. BOX 70983 DAR ES SALAAM.


Simu: 0757 – 567899/0789– 567899/0719 – 968160/0779 – 597066.


Email: songwak@yahoo.com. ptrsongwak@gmail.com






Maandiko ya somo: Mathayo 16:13 – 19






YALIYOMO:


1. Utangulizi.


2. Maana ya mlango.


3. Kazi ya mlango.


4. Mgawanyo wa mlango katika sura Majeshi katika ulimwengu wa Roho.


5. Kazi ya jeshi lolote.


6. Mambo yanayofungua malango ya kuzimu dhidi ya kanisa.


7. Njia ya kuyadhibiti haya malango ya kuzimu.






1. UTANGULIZI:


v Je, unayajua malango/milango ya kuzimu na kuzimu yenyewe? Kumbuka, ufahamu sahihi juu ya jambo lolote unalofanya au unalokabiliana nalo ni wa muhimu sana ili kufanikiwa vizuri.






v Acha kufanya kitu bila kuwa na ufahamu juu yake, au usipigane vita bila kujua adui yako vizuri; uwezo wake, silaha zake, mbinu zake na mawasilianao yake; lasivyo utaumia na kushindwa siku zote.






Kumbuka: Ufahamu hapa umelinganishwa na mwamba (Rock).






v Kwa nini Yesu alisema vita ya Kanisa ni dhidi ya milango ya kuzimu na siyo shetani? Fuatana nami katika somo hili.






2. MAANA YA MLANGO.


v Kwa mkutadha huu, mlango anaweza kuwa mtu au kitu chochote. Ila kwa somo hili mlango hapa ni mtu. Mfano: Adamu wa kwanza alikuwa mlango wa dhambi kuingia duniani na kuleta mauti kwa kila mwanadamu (Rumi 5:12) Adamu wa pili Yesu amekuwa mlango wa wokovu na uzima wa milele kwa kila amwaminie Yhn 10:7 – 10.






Kumbuka: Mungu hawezi kufanya jambo lolote duniani bila kupata mlango hali kadhalika hata shetani hivyo hivyo.






v Tazama mwanzo 18:17 habari za Ibrahim Kutoka 32:11, habari ya Musa, pia tazamaa Lk 22:3-6 habari yuda aliingiwa na roho ya shetani na kumsaliti Yesu. Ili shetani aingie ndani yako anahitaji mfano kumb. 28:7






3. KAZI YA MLANGO.


Kazi kubwa ya mlango ni kupitisha (kuingiza) na kutoa vitu.


Swali je, Mimi kama mlango naingiza nini na kutoa nini katika Kanisa/huduma/idara/familia/jamii?


Je, unapitisha (unaingiza) na kutoa mambo mema/mazuri katika Kanisa lako? Hapo ndipo utaelewa wewe ni lango la Mungu (Yesu) au la kuzimu kwani watu humchora shetani kuwa anasura mbaya anatisha, elewa leo kuwa shetani hayuko kama vile anavyochorwa, kwani hakuna ambaye angekubali kuwa na jitu linalotisha, wangemkimbia, hivyo shetani yuko vizuri, anasura nzuri ila kazi na matokeo yake ni mabaya sana na inatisha.






Kumbuka:


Wewe kama ni mchonganishi, mgomvi mwenye wivu, mwenye fitina na hila na tabia nyingi nyingine zinafanana nahizo zinawakilisha ufalme wa kuzimu (giza). Pia tunaposema Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo tunamaanisha haya (hawa) ni malango ya Mungu duniani yaliyopitisha vitu vizuri Tazama. Mwz. 18:17, (Ibrahim) Kutoka 32:11 (Musa).






Tazama Yoabu alikuwa mlango wa magonjwa katika ukoo wake 2Sam. 3: 27 – 29 Math. 12:43 – 45.






4. MGAWANYIKO WA MALANGO YA KUZIMU KATIKA SURA YA MAJESHI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.






Kama unavyona majeshi ya kawaida katika nchi ndivyo katika ulimwengu wa roho adui nae anajipanga vizuri tazama Efeso 6:12 katika kila nchi kuna jeshi la:-


a) Anga Dan. 10:12 - Wanajipanga kuzuia majibu.


b) Nchi kavu Kut. 22:18 - Wachawi, waganga n.k.


c) Baharini Mk. 4:34 -5:1 – Mapepo/Majini (Kuleta) Vurugu/Machafuko


Math. 12:43 – 45






Kumbuka: Kazi ya jeshi kulinda (ulinzi) dhidi ya uvamizi, Hivyo kama kanisa tukilala tu adui anatumaliza, soma


Math 13:24 – 30






5. KAZI YA JESHI LOLOTE.


v Kazi/wajibu wa jeshi ni kulinda nchi ili isivamiwe na adui. Efeso 6:10 -18.






v Ni marufuku kwa mlinzi kulala, anatakiwa awe macho siku zote, kosa akilala tu adui hatafanya kosa. Math. 13:24-30






6. MAMBO YANAYOFUNGUA MALANGO NA KUYAPA MALANGO YA KUZIMU NGUVU DHIDI YA KANISA.






I} UOVU, DHAMBI NA MAKOSA (Isaya 59:1 – 4, 1 Yhn 3:4, Math 1:21 Rumi 3:23, 6:23, Rumi 8:1 –


v Uovu: Ni mavuno ya maovu ya watu wengine au tabia ya mtu kuzoelea kufanya


(kutenda) dhambi.






v Dhambi: Ni uasi, kuupinga utawala unao tawala kwa halali, 1Yhn 3:4, Isaya 14:12 – 17.


v Makosa: Ni mambo tufanyayo bila kujua ni kosa kutokujua jambo ni kosa. Lawi 5:17






II} LAANA: Mith 26:1 – 2, Gal. 3:13, Mwz. 3:17


Laana ni kuzuizi kisicho onekana na chenye nguvu kimsingi laana ni tatizo la kiroho.






Kumbuka:


Msingi wa laana ni matamko (maneno) Mith 6:2. Hivyo uwe mwangalifu sana juu ya maneno unayo:-


a) Jitamkia


b) Unayotamkia wengine


c) Unayotamkiwa na wengine.


Maneno hayo yanaweza kuwa kizuizi katika ulimwengu wa roho na hata kukukwamisha katika mambo yako.






III} MAKUHANI KUICHA KWELI YA MUNGU. (Hosea 4:6)


v Leo hii watumishi wengi wanalighoshi (wanaongeza maji, chumvi) na kulilazimisha neno kusema lisivyopaswa kusemwa ili kukidhi mahitaji na matamanio ya moyo wao. (personal latest) tazama 1Petro 2:1 – 5.






IV} MFUMO MBAYA WA IBADA (KUABUDU): Math 10:8


v Mfano maombi ya fedha, mbaya zaidi yanatolewa kwa kulingana na kiwango cha fedha. Hii mimi nasema biashara haramu madhababuni.






v Viongozi (makuhani husika) pamoja na wanaopewa huduma hiyo wote ni wahuni ni malango ya kuzimu kwa ajili ya kulidhofisha Kanisa la Mungu, lakini habari njema ni kwamba Mwalimu na Bwana Yesu alikwisha tangulia kusema kuwa hakuna milango ya kuzimu itakayoweza kulishinda Kanisa lake.






v Bila kulisahau wimbi kubwa la waimbaji wa nyimbo za injili; ukiangalia kwa undani ni kama wao na wachungaji wao wanakubaliana wafanye biashara ili pengine wagawane baada ya huduma husika kuisha. Nijambo la kusikitisha sana kuona mtumishi anatanguliza pesa mbele huduma baadae, hakuna fedha, hakuna huduma (lipa kwanza, upate huduma) imeshakuwa kana kwamba hizo pesa waliziwekeza, hii ni roho ya ushetani (kuzimu) hayupo Mungu hapo, hata kama kinachoimbwa kinamsema na kumtaja Mungu.






v Mbaya zaidi hata wakifanya uzinduzi matamasha ya sifa na kuabudu uzinduzi wa kazi (CD, DVD) zao ni vituko na vioja tupu. Mimi nakumbuka vizuri, Mungu alipotupa watoto tulikwenda Kanisani na sadaka ya shukrani mbele za Mungu kwa kutupa uzao (zawadi ya Mtoto), sivyo Kanisa litupe sisi sadaka ya shukrani. Sasa leo ni kinyume baada ya waimbaji hawa kutoa sadaka hiyo ya shukrani, kuonyesha shetani amepofusha hata makuhani (viongozi – wachungaji) wanaweka viingilio tena kwa madaraja na viti maalumu, huu ni utapeli na wizi wa kiroho, hata kama ulikuwa hujui leo fahamu hivyo kuwa hivyo ndivyo ilivyo na hivyo ndinyo unavyotambuliwa na Mungu. Biblia inasema siku ya mwisho wengi watalia sana wakieleza walichokifanya kwa jina la Yesu, naye Yesu atawajibu na kuwaambia tokeni hapa ninyi mbuzi siwajui Math 25:11 – 46.






USHAURI WANGU: Naelewa mnayo mahitaji mbalimbali waeleze watu mbona watakuchangia kuliko kuwaibia kwa jina la Yesu, eti kwa kisingizio cha gharama za kurekodi studio, hivi mpendwa hata haya/aibu huna, wakati ulipoenda studio ulituaga kuwa tutakulipa?, sisi sote mwajiri wetu ni Mungu. Nenda kahudumu bila kutazamia malipo na Mungu aonaye sirini atakujaza na utashangaa, kwani Mungu anajishughulisha sana na mambo yetu 1Petro 5:7.






V} USINGIZI WA KIROHO: Math 13:24 – 30


Kuwa mzembe na mzito juu ya mambo ya Mungu (Ibada) humpa adui nafasi (Efo 4:27) ya kupanda magugu mipaka (mambo tusiyoyahitaji) maishani mwetu.


VI} KUZOELEA MAMBO YA MUNGU: Amuzi 16 – 20, 2Pet 1:9


Hali ya kuwa mwenyeji na mjuzi na kuonyesha kuridhika na kutosheka na kile ulicho nacho, hivyo ukajiona unaweza kufanya chochote bila kuulizwa. Rejea kwa rafiki yetu Samsoni matokeo ya roho ya mazoea ni:-


Ø Upofu wa kiroho


Ø Uziwi wa kiroho


Ø Mfungwa wa kiroho


Ø Mtumwa wa koroho






VII} UGOMVI (MIGOGORO) KATI YA NDUGU NA NDUGU NDANI YA NYUMBA YA MUNGU (KANISANI) Kut 2:11 – 14.


v Umewahi kujiuliza, msemo huu (methali hii) isemayo fahali wawili wagombanapo au vita vya Panzi furaha kwa Kunguru.






v Ndivyo ilivyo shetani akishapata nafasi maishani mwetu anapanda mbegu magugu ya magomvi. Hivyo tunapigana sisi kwa sisi yeye humrahisishia sana kazi kutumaliza kiulaini kabisa. Ni sawa na swala wanapo pigana porini simba hatapata wakati mgumu au kazi/shida kumkamata mmoja wapo.






VIII} IBADA YA MIUNGU: Lk 10:38 – 42, Mark 4:19 Kutoka 20:4, ya Yer 17:5 – 8.


Mfano: Sanamu, watu, shughuki nyingi.


Kumbuka: Mtu au kitu chochote kinachochukua nafasi ya Mungu kinaitwa sanamu au Mungu. Hivyo uwe makini sana usije ukawa mlango wa kuzimu na kudhofisha kazi ya Mungu.






IX} WIZI WA FUNGU LA KUMI: Mal 3:8 – 11, Zek 5:1-


v Elewa kuwa wizi ni tabia ya shetani soma Yoh 10:10. Hivyo uwe mwangalifu usije ukaingia kwenye mtego wa kumwibia Mungu. Maana usipotoa fungu la kumi vita hivyo hupigani na shetani utakuwa unapambana moja kwa moja na Mungu, na hakuna aliyeshindana na Mungu akashinda. Badilika kisha chukua hatua, Amen.






7. NJIA YA KUYADHIBITI MALANGO YA KUZIMU.






I} KUWA NA UFAHAMU SAHIHI WA KWELI YA MUNGU


Yhn 8:31 – 37, Josh 7:14, Mith 11:9;21:16


Bila yakuwa na ufahamu sahihi wa neno la Mungu itakuwa ni vigumu sana kuyajua malango utaendelea kuteseka, mpaka utakapogundua lango gani limefunguliwa, kumbuka mchawi wa kwanza ya huduma/maisha yako ni wewe mwenyewe, hivyo kabla ya kumtafuta aliyesababisha tatizo jiulize wewe mwenyewe unamchango gani katika tatizo hilo. Yesu katika huduma yake hakufanya jambo bila ya kujua nini chanzo cha tatizo hilo Math 9:32 – 33.










II} KUSAMEHE (FORGIVENESS) NA KUOMBA MSAMAHA. Math 5:7, 6:9 – 14 Mark 11:25


v Hii ni njia pekee yenye nguvu kummaliza adui katika maisha yako unapokosea omba msamaha na unapokosewa samehe ni eneo tata sana na gumu kibinadamu lakini kwa ajili ya usalama na kuwekwa huru hakuna namna lazima nijifunze kusamehe kwa gharama zozote.


v Ipo hivi, japo wewe ndiyo umekosewa na ungetegemea aliyekukosea aje akuombe msamaha lakini haoni haja ya kufanya hivyo ana roho ya kifarisayo (kiburi) cha kujihesabia haki, sasa wewe kwa kuwa ndiye unayeumia kwa kitendo au vitendo anavyo/alivyo kufanyia mfano matusi, dhuluma, usengenyaji, uongo, uzushi kachukua vitu vyako. Unachopaswa kufanya ni kusamehe. Bila kufanya hivyo ni sawa na kukoroga sumu na kuinywa mwenyewe na itakudhuru peke yako, mwenzako anakula maisha.






v Kumbuka: msingi wa mimi kusamehewa na Mungu ni kuwasamehe wengine walio nikosea. Hivyo msamaha wangu umeshikiliwa na Mungu atauachia tu pale nitakapo mwachia huyu aliyenikosea. Mark 11:25.






v Elewa kwamba unaposamehe unafungua mlango wa Mungu kukupigania na kukurejeshea haki zako.






III} KUOMBA TOBA NA REHEMA.


Lawi 16:1-, Ebr 4:16, Yk 4:17, Yhn 3:21 – 22, Mith 3:3 – 4


Maombi ya toba yanarejesha ushirika uliopotea na maombi ya rehema yanashughulika na msingi wa maisha yako kuruhusu neema ya Mungu kukutetea.






Matokeo ya toba na maombi ya rehema.


a) Kibali.


b) Ujasiri.


c) Akili nzuri (ufahamu).






Kumbuka: Dhambi/uovu/makosa huondoa ujasiri wa kwenda mbele za Mungu, ila toba ya kweli na maombi ya rehema yanarejesha ujasiri na kibali.






Ukimalizana na Mungu, sasa unauwezo wa kumshughulikia adui, lakini usithubutu kumpiga shetani wakati wewe na Mungu maadui utaumia.






IV} VAA SILAHA ZOTE ZA MUNGU.


Ef 6:10 – 18, Kol 3:16, Lk 44: 1- 8, 1Kor 2:10 - , 1Yh 2:20






v Unavaa silaha zote za Mungu tayari kwa vita ya kuyashughulikia hayo malango ya kuzimu.






v Jitambue/jifahamu kuwa wewe ni mfalme/mtawala na neno la mfalme lina Nguvu yaani neno lake ndiyo sheria, ndiyo katiba, halipingwi Mh. 8:4.






Kumbuka: Kujaa i} Neno Kol 3:16


ii} Roho Mtakatifu 1Kor 2:10 – 14










UISHI MILELE.


2Kor 13:14