♻ *SOMO*: *_KANUNI ZA KUENDESHA UCHUMBA_*
BY PASTOR SONGWA KAZI
WhatsApp 0719968160.
⏹Fuatana nami kwa utulivu sana juu ya mada au Somo zuri hili.
🕎 *Utangulizi:*
✍🏻Yawezekana kabisa wewe na mwenzako-yaani mchumba wako , mnaweza kuwa na sifa nyingi kama wachumba.
Huenda mkijitazama na hata watu wengine wakiwaona, hakuna anayetilia mashaka kwamba mnasifa na mnaonekana tayari kwa ndoa.
Lakini kama dereva yeyote aliye na sifa anavyopaswa kuzingatia sheria, vigezo na taratibu zote za udereva, mnapaswa kuzingatia kanuni za uendeshaji uchumba.
Zipo kanuni nyingi, lakini nimeziteua kanuni hizi chache naziona zimebeba uzito usiopungua busara, hekima na maarifa ya kiungu.
✝KANUNI; ni njia au ule utaratibu wa kufanya jambo fulani ili likupe matokeo chanya.
*Kumbuka*: Kanuni haidanganyi , yeyote anayeitumia itampa matokeo yaleyale.
🙆♂Ukipindua Kanuni inakuadhibu.
♻UCHUMBA NI KIVULI CHA NDOA♻
Kile mtakifanya kwenye uchumba ndicho mtakacho kiishi kwenye ndoa.
🤔🤔🤔
Hebu tuziangalie kanuni hizi kwa hatua:
1⃣ *_MRUHUSINI MUNGU AWE MJENZI WA MKUU WA UCHUMBA WENU._*
(Zaburi 127:1)
✝Psalms 127:1
[1](A Song of degrees for Solomon.) Except the LORD build the house, they labour in vain that build it: except the LORD keep the city, the watchman waketh but in vain.
*BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.* BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
👆👆Hii ni kwa sababu mke au mume sahihi anatoka kwa Bwana.
*Mithali 19:14*
2⃣ *_MSHIRIKISHE KWANZA MCHUNGAJI WAKO KABLA YA WATU WENGINE_*
(Waefeso 6:1-3)
✝Ephesians 6:1
[1]Children, obey your parents in the Lord: for this is right.
*Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.*
✝ (Wagalatia 6:6)
✍🏻Galatians 6:6
[6]Let him that is taught in the word communicate unto him that teacheth in all good things.
*Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.*
🙏🙏Uchumba wenu ukipata baraka za mchungaji wako sasa upo huru kupiga hatua ya tatu.
3⃣ *WASHIRIKISHE WAZAZI AU WALEZI WAKO*
( Waefeso 6:2-3)
✝Ephesians 6:2-3
[2]Honour thy father and mother; (which is the first commandment with promise;)
*Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,*
[3]That it may be well with thee, and thou mayest live long on the earth.
Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
4⃣ *_WEKENI UCHUMBA WENU WAZI MBELE ZA WATU WANAOWAPENDA_*
( Mwanzo 4:9)
✝Genesis 4:9
[9]And the LORD said unto Cain, Where is Abel thy brother? And he said, I know not: Am I my brother's keeper?
*BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?*
✍🏻Tambua wazi kuwa watu wanaowapenda ni walinzi wakuaminika kwa ndoto zenu na rafiki zenu.
Kumbuka: *Uchumba siyo siri*
❤Msiwaweke mbali nanyi watu wanaowatakia mema maishani mwenu❤ maana hao ni walinzi wenu wa kuwa angalia ( waangalizi) msiwafiche jambo kabisa.
🤔Wanaweza kuwasaidia kuyaona mambo msiyoyaona.
5⃣ *_JICHANGANYENI NA JAMII KATIKA SHUGHULI ZA JAMII_*
( Mwanzo 24:19-21)
✝Genesis 24:19-21
[19]And when she had done giving him drink, she said, I will draw water for thy camels also, until they have done drinking.
*Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa.*
[20]And she hasted, and emptied her pitcher into the trough, and ran again unto the well to draw water, and drew for all his camels.
Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote.
[21]And the man wondering at her held his peace, to wit whether the LORD had made his journey prosperous or not.
*Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kwamba BWANA ameifanikisha safari yake ama sivyo.*
✍🏻Usijitenge na kuwa kivyakovyako utapata taabu sana.
Hakikisha unashiriki katika shughuli za jamii kama vile sherehe, misiba, michango ya maendeleo , ushuhudiaji, michezo na utumishi mbalimbali n.k.
*Kumbuka;* unapowatumikia wengine, unajianika -yaani unajitambulisha ulivyo. Rebeka hakujua kuwa alikuwa anajianika au kujitangaza kwa mshenga wake kwa kuwanywesha wale ngamia.
♻ *Utapata fursa ya kumjua mchumba wako vizuri kupitia kutumika*
6⃣ *_LINDENI MAJINA YENU YASIINGIE MADOA_*
( Mithali 22:1
Proverbs 22:1
[1]A good name is rather to be chosen than great riches, and loving favour rather than silver and gold.
*Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema*
*fedha na dhahabu.*
🤔Wekeni mipaka kati yenu, msijiachie kama mizigo ya kununi.
🤔Kuna chumba kingine ni kero utadhani MTU na mke wake wa ndoa mpaka kichwa kinauma, sokoni wote, kisimani/bombani wote, chooni wote, chumbani wote, wanafuatana kama kumbikumbi.
♻Presha ya nini 🤷♂🤷♂🤷♂ tulizana mfunge ndoa. Maana mwisho wake wengi huishia kufanya zinaa. Tafadhali sana wekeni mipaka.
7⃣ _*MSIWASHE MOTO WA MAPENZI MSIO WEZA KUUZIMA*_
( Wimbo uliobora 2:7)
✝Song of Solomon 2:7
[7]I charge you, O ye daughters of Jerusalem, by the roes, and by the hinds of the field, that ye stir not up, nor awake my love, till he please.
*Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.*
🤔🤔Wekeni mbali mazungumzo mabaya ya kimapenzi-mahaba, msifanye michezo ya kimapenzi kama kutomasana, kupigana mabusu na kunyonyana chuchu, ndini na kushikana shikana , picha za ngono, kufanya hivyo ni sawa tu umefanya zinaa,
kwani biblia inasema amtazamae mwanamke kwa kumtamani tayari amekwisha zini naye moyoni wake sembuse michezo ya kimapenzi. Acha Mara moja ni hatari kubwa.
*Tubu anza upya.*
8⃣ *_FUNGUKENI MIOYO NA ONGEENI KWA UWAZI BILA KUFICHANA_*
( Mithali 17:28)
( Waefeso 4:25)
✝ Proverbs 17:28
[28]Even a fool, when he holdeth his peace, is counted wise: and he that shutteth his lips is esteemed a man of understanding.
*Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.*
😁😁 *Ongea ili mwenzako apime kiwango cha upambavu wako*
✝Ephesians 4:25
[25]Wherefore putting away lying, speak every man truth with his neighbour: for we are members one of another.
*Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.*
😁😁Kadri mnavyoongea ndiyo unapojua kiwango cha uongozi na ukweli wa mchumba wako.
♻ *kuweni wazi*
9⃣ *_MALIZENI TOFAUTI ZENU KISTAARABU MARA ZITOKEAPO_*
( Waefeso 4:26)
✝Ephesians 4:26
[26]Be ye angry, and sin not: let not the sun go down upon your wrath:
*Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;*
🕎Kumbuka , mchumba siyo Yesu kwamba yupo kamili ,IPO siku mtavurugana , na kuchefuana kabisa. Kipindi kama hicho tafuteni NJIA ya kutatua maisha yaendelee mbele.
🔟 *_CHAGUENI WANANDOA WALIOWATUNGULIA WATAKAO LEA UCHUMBA WENU_MLIO HURU KWAO_*
( MENTOR)
( Mithali 11:14)
✝Proverbs 11:14
[14]Where no counsel is, the people fall: but in the multitude of counsellors there is safety.
*Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.*
♻Hakuna haja ya kubahatisha pakukanyaga kama wapo watu waliowatangulia .
Ushauri: someni Vitabu, silikizeni CD na DVD na huzulieni semina na makongamano ya MAHUSIANO na ndoa ili kuongeza ujuzi na maarifa.
1⃣1⃣ *_KILA MMOJA AJIFUNZE KUONGEA LUGHA YA UPENDO YA MWENZAKE_*
( Yohana 13:34, Wagalatia 6:2)
✝John 13:34
[34]A new commandment I give unto you, That ye love one another; as I have loved you, that ye also love one another.
*Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.*
✝✝✝
Galatians 6:2
[2]Bear ye one another's burdens, and so fulfil the law of Christ.
*Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.*
❤❤Siyo rahisi kuongea lugha moja , muulize anapenda nini.
*Aina ya lugha*
⏹ Lugha ya maneno ya kujali.
⏹Lugha ya kupeana Zawadi.
⏹ Lugha ya kusaidiana.
⏹Lugha ya kutumia muda mwafaka pamoja.
⏹Lugha ya mguso wa Upendo.
1⃣2⃣ *_INGIA KATIKA UHUSIANO WA UCHUMBA KAMA UPO TAYARI KWA NDOA_*
( Mhubiri 3:1)
✝Ecclesiastes 3:1
[1]To every thing there is a season, and a time to every purpose under the heaven:
*Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.*
🕎Kama huna mpango na ndoa acha kabisa Fanya unachofanya wakati ukifika utachoka mwenyewe.
( Wimbo bora 3:5)
✝Song of Solomon 3:5
[5]I charge you, O ye daughters of Jerusalem, by the roes, and by the hinds of the field, that ye stir not up, nor awake my love, till he please.
*Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. Bwana Arusi na Kundi lake Wakaribia*
♻ *HITIMISHO*
✍🏻Angalizo:
Kuingia katika MAHUSIANO na mtu yeyote kwa sababu amekuvutia kimwili lakini huoni anafaa katika maagano ya milele ya ndoa si Salama kabisa.
🤔🤔 *usicheze na mkondo wa mapenzi unaopita kwa kasi ; utajitambua baada ya kunywa maji*😁
Ubarikiwe Sana kwa kusoma Somo hili la Kanuni 12 za KUENDESHA UCHUMBA.
By Pastor SONGWA KAZI
MWL na Mshauri wa maswala ya MAHUSIANO.
Simu : 0757-567-899
Good
ReplyDelete