NJIA SAHIHI YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA
BWANA.
{Tiba Ya Vijana. }
v
TOLEO LA TATU {3} - (c )
DESEMBA, 2016.
Yaliyomo:
SHUKURANI
KUHUSU MWANDISHI -TA WASIFU
UTANGULIZI
1. CHANZO CHA NDOA NA KUSUDI LA NDOA
2.MISINGI BORA YA MAHUSIANO.
3 NJIA YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA BWANA
4. SABABU ZAINAZOFANYA KIJANA ACHELEWE KUOA AU KUOLEWA
5. MADHARA YA ZINAA AU NGONO KABLA YA NDOA.
6. MAMBO YA KUYAELEWA KATIKA MAHUSIANO.
7. UTAJUAJE KUWA HUYU NI CHAGUO LAKO ?
8. MAMBO YANAYO VUNJA MAHUSIANO.
9. MAMBO YANAYO JENGA MAHUSIANO.
10. MAMBO YAKUZINGATIA
ILI KUIMALIZA SAFARI YAMAHUSIANO SALAMA NA KWA USHINDI MKUU
11. MAOMBI
. MAANDIKO YA MSINGI YA SOMO.
Mwanzo 1:26-28, Mwanzo 2:7,15,18-25 , Mithali 19:14 na Mithali 18:22
I. SHUKURANI.
·
Kipekee kabisa na mshukuru sana Mungu wangu BWANA Yesu Kristo aliye
niita kwa wito mtakatifu kwakuniokoa na kunitenga kwa ajili ya utumishi katika
ufalme wake.
·
Pili; ninazo shukurani zangu
nyingi kwa baba na rafiki; Mchungaji wangu kiongozi Askofu Victor A. Tawete na family yake kwa ushauri ,
kwakunitia moyo, kuniombea na kwa mafundisho yake yamenijenga sana.
·
Tatu; namshukuru Yesu wangu kwa kunipa mke mwenye busara Miriam
Songwa Kazi na wanangu Meshach, Prince na Amani kwa maombi na uvumulivu wao
kwangu pindi walipo nikosa nikiwa katika maandalizi ya kazi hii njema unayo
isoma.
·
Nne; nina washukuru wazazi wangu ndugu na jamaa zangu wote wanao
niombea.
·
Tano; nina washukuru kipee rafiki zangu kipenzi na watenda kazi
pamoja nami katika kazi ya Injili ya ufalme wa Mungu; wana Life Changing Ministry
international [ LCM ]na wachungaji wote rafiki zangu kwa maombi yao na ushauri
wao. Mungu awabariki sana.
II. KUHUSU MWANDISHI.
II. KUHUSU MWANDISHI.
·
TAWASIFU:
Nimezaliwa huko Bunda –Mara mnano mwaka 1980 ni kiwa Mtoto wa kumi na wa mwisho katika familia. Niliokoka mwaka 1999.
ELIMU:
Nina Cheti-[Certificate] chaTheolojia- Elimu kuhusu Mungu- Theology In Bible kutoka African Leadership Inernational-AL.
Kwa sasa ninachukua Shahada [digrii] katika Uongozi, Utawala na Huduma-[ Bachelor In Administration, Management and Ministry-BA In Min] kutoka katika Chuo Cha Kimataifa cha T-NET INTERNATIONAL.
HUDUMA.
Ø
Tangu mwaka 2004 mpaka sasa nimekuwa nikiandaa makongamano ,
semina na mikutano ya Injili ya matengenezo
na uamusho, ili kuijenga na kuinua misingi ya vizazi vingi; nikilijenga kanisa nakulipa nyenzo kanisa la
vijana katika maeneo nyeti ya mahusiano
yaliyo sahaulika sana na utumishi katika ufalme wa Mungu .Isaya 58:12-14 na
Zaburi 11:3, nikishirikiana na huduna na makanisa rafiki. Pia nimekuwa nikifanya huduma za Umisheni-Umishenari,
Uinjilisti na Ualimu katika maeneo mbalimbali ya Vijijini na Mijini ndani ya
nchi na nje nchi; kwa kujitoa-kidhabihu kwa gharama zangu mwenyewe pamoja na wapenzi wa Injili , wapendao kwenda pamoja
nami hutoa vitu vyao ili kuwafikia watu wenye kiu na njaa ya haki na Injili; bila kutazamia malipo, kwani tumepewa
bure tutoe bure-Math.10:8, nikihubiri na kufundisha Kweli ya Neno hai
la Mungu [Sound Doctrine ] na kufanyika baraka kuu kila eneo nililofika
kihuduma kwa kulijenga kwa kuwaandaa waamini kuwa wanafunzi watendakazi na
wazalishaji wazuri katika shamba la
Bwana ; na kuwaongoza watu wengi kumjua na kumwamini BWANA YESU na wengine
wengi kufunguliwa na kuwekwa huru kutoka kwenye vifungo na magereza ya utumwa
wa nguvu za giza.
Ø
Ni Kiongozi na Mkurugenzi Mkuu [ Director General] wa Huduma ya Life Changing Ministry International-LCM; yenye malengo ya kuleta MATENGENEZO na UAMUSHO, ili kuinua Misingi ya Vizazi vingi na kuwaandaa ili kumzalia Bwana matunda kwa kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa Yesu na hivyo kuukamilisha Utume Mkuu ambao ndio Amri au Agizo kuu la Kanisa. Mathayo 28:18-20.
Ni Kiongozi na Mkurugenzi Mkuu [ Director General] wa Huduma ya Life Changing Ministry International-LCM; yenye malengo ya kuleta MATENGENEZO na UAMUSHO, ili kuinua Misingi ya Vizazi vingi na kuwaandaa ili kumzalia Bwana matunda kwa kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa Yesu na hivyo kuukamilisha Utume Mkuu ambao ndio Amri au Agizo kuu la Kanisa. Mathayo 28:18-20.
Ø
Kwa sasa ni Mchungaji Msaidizi Kanisa la GLORY TO GLORY CHRISTIAN CENTRE- GGCC TAG FOREST KONGOWE chini ya ASKOFU wangu mpendwa Rev. Victor Tawete.
Kwa sasa ni Mchungaji Msaidizi Kanisa la GLORY TO GLORY CHRISTIAN CENTRE- GGCC TAG FOREST KONGOWE chini ya ASKOFU wangu mpendwa Rev. Victor Tawete.
Ø
Nilifunga ndoa Agosti 26, 2007 na Miriam; na Mungu ametubarikia watoto watatu wa kiume, Meshach, Prince na Amani. Bwana Yesu awabariki wote.
III. UTANGULIZI:
Nilifunga ndoa Agosti 26, 2007 na Miriam; na Mungu ametubarikia watoto watatu wa kiume, Meshach, Prince na Amani. Bwana Yesu awabariki wote.
III. UTANGULIZI:
·
Baada ya mtu kiokoka ,
jambo pekee la muhimu atakalo paswa kufanya uchaguzi na maamuzi sahihi ya nani
wa kuoa au kuolewa naye.
·
Uamuzi huu ni wamuhimu sana , na ikitokea umekosea itayagharimu
maisha yako na kukuletea mateso ya muda mrefu katika maisha yako; na ikitokea
umefanya uchaguzuzi na maamuzi mazuri ya mwenzi wa maisha utafurahia maisha yako.
·
Ndoa mbaya inaweza kuathiri maeneo mengine ya maisha
·
Leo kuna baadhi ya wanandoa wanajutia maamuzi yao, wanatamani
warudie ujana ili waanz e mchakato upya
wa mahusiano kwa kufanya maamuzi sahihi.
·
.Je, wewe ni miongoni mwa vijana walio na maono au ndoto yakuwa siku moja uta oa ama kuolewa ?
.Je, wewe ni miongoni mwa vijana walio na maono au ndoto yakuwa siku moja uta oa ama kuolewa ?
Na kama jibu lako ni ndiyo; basi kitabu hiki kitakufaa sana
kukupa nuru na kukuongezea hatua zaidi ili uanze na kumaliza salama na vizuri
safari au mbio za mahusiano ulizonazo au unazotazamia kuwa nazo siku za usoni.
·
Kama wewe ni kijana tulia usipaparikie kuingia kwenye ndoa; kwa
msingi wa:-
ü
Hofu ya umri
ü
Tamaa na kuwafurahisha watu
ü
Shinikizo la wazazi au familia
ü
Rafiki zako wameolewa
·
Kwa watu wawili kuishi pamoja kwa amani na furaha ni lazima wawe
wamekubaliana kiroho, kimwili na kiakili kwa kila kitu. Mfano; tembo hawezi
kuoa kipepeo wala ng’ombe kuoana na samaki; swali watakutania wapi? Hivyo
mwamini utaolewa na mtu aliye amini. 2Korintho6:14
·
Shetani ameweka mtego wake kwenye familia , kwani anajua wazi
kila mtu lazima awe na familia anayo toka. Kwani akifanikiwa kuwaweka watu wawili kwa jinsi
isivyo sawsawa atakuwa amefanikisha mpango wake wa kuharibu jamii na mataifa.
·
Watu wawili wasiyo sahihi wakiunda familia wata zaa watoto
ambayo ni mzigo na tatizo kwa jamii.
·
Jiulize maswali haya:
ü
Nini unataka kwa mwanamke?
ü
Nini unataka kwa mwaume?
KUMBUKA:
·
Ndoa, siyo unataka nini, bali ni juu ya nani unamhitaji; ukiwa
na ufahamu huu uwe bora wakati huohuo nawe unawafanya wenzako kuwa bora.
·
Ndoa ni kumpata msaidizi wa maisha; ndiyo maana sasa unapaswa
kujua mapema sababu kuoa au kuolewa.
.Pia hata kama umeoa au kuolewa ama umekwisha mpata umpendae na mnatazamia kufunga pingu za maisha yaani kufunga ndoa hivi karibuni bado kitabu hiki kitakuwa cha msaada sana kwako pia; ili kukisaidia kizazi hiki kinachokabiliwa na changamoto nyingi za kila namna ili kisipotee na kisifanye makosa kwa kukosa maarifa. Hosea 4:6; kama wengine waliofanya makosa na wakaumia; hata sasa wanalia,wanajuta kwani walijiingiza kwenye wimbi hili la mahusiano bila kuwa na maarifa na ufahamu wakutosha; wakaumizwa na leo wana majeraha na wengi wao hawajui watatoka vipi kwenye maumivu na uchungu huo. Mithali 18:14…… nani awezeye kuistahimili roho iliyo vunjika?
.Pia hata kama umeoa au kuolewa ama umekwisha mpata umpendae na mnatazamia kufunga pingu za maisha yaani kufunga ndoa hivi karibuni bado kitabu hiki kitakuwa cha msaada sana kwako pia; ili kukisaidia kizazi hiki kinachokabiliwa na changamoto nyingi za kila namna ili kisipotee na kisifanye makosa kwa kukosa maarifa. Hosea 4:6; kama wengine waliofanya makosa na wakaumia; hata sasa wanalia,wanajuta kwani walijiingiza kwenye wimbi hili la mahusiano bila kuwa na maarifa na ufahamu wakutosha; wakaumizwa na leo wana majeraha na wengi wao hawajui watatoka vipi kwenye maumivu na uchungu huo. Mithali 18:14…… nani awezeye kuistahimili roho iliyo vunjika?
Biblia inasema katika Hosea 4:6 kuwa, ‘ Watu wangu wanaangamizwa kwakukosa maarifa….’Hivyo hakuna sababu ya kuangamia kwa kukosa maarifa na Mungu hataki kabisa wewe au kizazi chetu na kile kijacho kiangamizwe eti kwakukosa maarifa, ndio maana sasa kinakuja kitabu hiki ili kutupa maarifa, nyenzo na nuru katika maeneo fulanifulani ya mahusiano.
.Hivyo kitabu hiki ni silaha iliyo mkononi na nyezo tosha yakumsaidia kijana kutokufanya makosa yanayoweza kuepukika yatokanayo na makosa ya kukosa maarifa yaani ufahamu juu ya mahusiano. Elewa kuwa UFAHAMU NI NGUVU.
.Kitabu hiki kinamfaa kila mtu mwenye ndoto au maono ya kwamba ipo siku moja atakuwa mke au mume wa mtu; Kwa msingi huo kitabu hiki kinafaa kusomwa na mtu yeyote Yule hasa vijana, wanafunzi, wanandoa , watumishi na viongozi wote ili tusifanye makosa wakati utakapo wadia au fika wa kuoa au kuolewa.
.Hakikisha mtumishi mwenzangu unayo nakala hii kwenye makitaba yako ili kukisaidia kizazi chetu kwenye eneo la mahusiano.
KUMBUKA:
Kuoa au kuolewa yaani NDOA ni mpango wa asili wa Mungu kwetu sisi watoto wake. Tazama Mwanzo 1:26-28 hasa mstari wa 27-28 inasema, ‘ Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke, aliwaumba. Mungu akawabarikia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
KUMBUKA:
Siyo vema kabisa na wala haijakaaa vizuri kwa vijana wenye umri na sifa za kuoa ama kuolewa hawajitambui yaani hawajaoa na kuolewa wapo wapo tu . Mwanzo 2:18; Bwana Mungu akasema , si vema huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Nini tunajifunza hapa? Ni kuwa Mungu ndiye BWANA wa historia na mwasisi wa taasisi hii ya NDOA, hivyo ni mpango mkakati wa Mungu kabisa kwa vijana kuoa na kuolewa.
Mithali 18:22 inasema, “ Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.” Kwa lugha nyepesi Mungu ndiye anae toa kibali cha watu kuoa na kuolewa hii ni kutuonesha jinsi alivyo makini [serious] na swala la ndoa. Tazama pia Mithali 19:14; ina sema kuwa, “ Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
.Sasa karibu tuangalie kwa pamoja hazina iliyopo kwenye somo hili na Mungu wangu akutane na haja ya moyo wako katika jina la Yesu, Amen.
SURA
YA KWANZA:
CHANZO NA KUSUDI LA NDOA.
.Chanzo ndoa kuwepo sio wazo wala mpango wa mtu au kikundi Fulani cha dini bali ni mpango mkamilifu wa Mungu mwenyewe; Na Mungu ndiye aliye fungisha ndoa ya kwanza; Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia , Mungu akasema, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
Kulithibitisha hili Mungu mwenyewe kupitia mtunzi wa Mithali 19:14 anasema; “…….mke mwenye busara mtu hupewa na BWANA” wala sio mtu, wazazi au marafiki.
.KUSUDI ; ni ile sababu iliyopelekea jambo au kitu fulani kuwepo. Tangu mwanzo Mungu aliweka wazi kusudi la NDOA katika kitabu cha Mwanzo 1:28, alipo wabarikia Adamu na Eva, akasema, “ Zaeni Mkaongezeke…..”Hivyo moja ya kusudi la Ndoa ni:-
[i] Kuendeleza uzao-kizazi [ uumbaji] wa kiroho na kimwili; kwa maana ya kwamba Mungu asingeendelea kufinyanga tope siku zote bali aliweka mfumo ndani ya mwadamu kuendeleza kizazi.
[ii] Ushirika na kusaidiana majukumu endelevu, kwani Adamu alionekana kuwa yuko mpweke ndipo Mungu akasema si vyema huyo mtu – Adamu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Mwanzo 2:18 na Mithali 19:14, anapo sema, “ Mke mwenye busara ( wise, understanding and prudent wife) huyu ni aina ya mke atakaye weza kuwa na uwezo wa kulielewa kusudi la Mungu ndani ya mume na kuwa sehemu ya kulifanikisha, kuliendeleza na kulikamilisha; kinyume chake utakapokosea kumpata mke au mume mwenye busara na hekima atakuwa mwiba [kikwazo] mbavuni mwako na atatumika kikamilifu kukukwamisha kwenye utumishi na hata katika ndoto au maono na mipango ya maisha uliyo nayo. Kwani haoni kama unavyo ona.
KUMBUKA:
Ø Kuna aina kama
tatu za mke au mume nao ni:
1. Mke/mume wa kupewa na BWANA
2. Mke/mume wakupewa na wazazi,ndugu au marafiki
3. Mke/mume wakujipatia mwenyewe
Mke au mume atakae kufaa kati ya hao watatu na kulikamilisha kusudi la Mungu maishani mwako ni yule atokaye kwa BWANA peke yake.- Mithali 19:14.
SURA YA PILI :
MISINGI
BORA YA MAHUSIANO.
Kama misingi
ikiharibika , Mwenye haki atafanya nini? Zaburi 11:3
Heshima , ubora na
uthabiti wa nyumba yeyote siyo rangi au matofali bali ni msingi imara. Historia
zetu zimefungwa na misingi yetu ya nyuma iliyo tubeba; kwa msingi huo misingi
yetu ndiyo itakayo amua hatima yetu. Basi, elewa wazi kuwa , utakapo kosea
msingi wa jambo lolote jua kuwa hatima yako itakuwa ngumu na mbaya sana.
Mjenzi yeyote mwenye
akili au hekima hujenga nyumba yake kwenye mwamba imara [ msingi ] Mathayo 7:24.
Na mara aonapo
kunashida kwenye msingi, huubomoa na kuuvunja kasha huujenga na kuuimarisha. Yeremia 1:10.
·
Ni heri na bora zaidi
uchumba uliovunjika kuliko kuwa na ndoa isiyo na furaha na amani.
·
Wakati wa uchumba
ndiyo wakati pekee wa kuweka misingi imara na bora ya ndoa yenu. Kumbuka msingi
mtakao uweka ndiyo utakao toa picha na dira na ku amua mwuwe na ndoa ya namna
gani.
·
Kamwe usifanye tendo
la ndoa kabla ya ndoa , utakuwa umevuruga na kuharibu sana misingi yako ya
ndoa.
v
Msingi mkuu na bora wa mahusiano ni:
1. BWANA
YESU -1Petero 2:6-8 Yesu
ndiye jiwe kuu la pembeni.
Ni jambo la maana sana kumheshimu Mungu kwenye
mahusiano yenu. Jambo lolote la ki-Mungu lazima lianze na Mungu na kumalizika
na Mungu. Mithali 16:1-4, mkabidhi BWANA
kazi zako , Na mawazo yako yatathibitika. Mathayo 6:33 – Bali utafuteni kwanza
ufalme wa wake- Mungu na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa. Mithali 19:14 ……… mke mwenye busara mtu hupewa na BWANA.
Misingi mingine bora ya mahusiano ni:-
1.1 Kuanza na madhabahu / wachungaji.
Hakikisha safari yako ya mahusiano ni rasmi na
mchungaji wako awe anajua mwanzo mwisho wa jambo lenu; na siyo unamshirikisha
wakati tayari jambo limekwisha kuota mizizi na mmekwisha malizana wenyewe;
haijakaa vizuri kabisa kumficha mchungaji wako. Kitendo tu cha mchungaji kujua
swala lenu la mahusiano ni usalama kwenu na uponyaji, kwania atakuombea na
kukushauri.
1.2 Wekeni mahusiano yenu wazi; hakuna haja ya
kufichaficha kama jambo ni la ki-Munngu acha watu wajue mapenzi yenu. Kwani ni jambo la heri.
Epuka kufanya na kuendesha uchumba bubu [
uchumba usio rasmi ]; unakuta vijana wapo kanisanai wana miezi au miaka kadhaa
wakiendesha uchumba bila uongozi kujua;
haifai kwani ni hii kwa hasara ya nafsi yako.
USHUHUDA
WANGU BINAFSI.
Mara tu ya mke wangu
leo kunipa jibu la ndiyo, nilikuwa na tembea na picha zake kwaninilitamani kila
mtu ajue kuwa nina mchumba nimpendaye kutoka kwa BWANA. Sikutaka kuwa siri.
SURA YA TATU:
NJIA
SAHIHI YA KUMPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA BWANA.
NJIA- Ni mwongozo au
dira [direction] inayo mwongoza mtu kufika au kumaliza mwendo au safari yake
vizuri bila kupotea. Hivyo kumbuka ; Kila njia ina masharti yake yaani taratibu
au kanuni kwa hiyo yakupasa kuyafuata vema ili usikwame au kupata ajari na
kupotea njiani.
KUMBUKA:
Kama hujui unakokwenda, njia yoyote itakufikisha huko usikokujua. Ni sawa na kulenga hewa utafanikiwa kupiga shabaha hiyo, na hakuna anaye lenga hewa akaikosa.
Mathayo 15:14 ina zungumza kwa habari ya kiongozi kipofu akimwongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni. Hivyo lengo la Njia hizi ni ili usije ukatumbukia shimoni, kwa kuwa kipofu bali uone sawasawa; uwe na ufahamu wakutosha juu ya mahusiano.
§
Njia pekee ya kanisa yaani mwongozo wetu ni NENO la MUNGU kwani ndio lenye nuru yakutuongoza ili kukupata mke au mume sahihi umpendaye kutoka kwa BWANA.
Njia pekee ya kanisa yaani mwongozo wetu ni NENO la MUNGU kwani ndio lenye nuru yakutuongoza ili kukupata mke au mume sahihi umpendaye kutoka kwa BWANA.
Zifuatazo ni baadhi tu ya Njia hizo za kumpata mke au mume atokaye kwa BWANA tu:
i. Utafute kwanza Ufalme wa Mungu:
Mathayo 6:33
·
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote
mtazidishiwa.
Hii ndiyo njia pekee kuu kuliko zote uwezazo mtu kutumia ili
kumpata mwenza aliye chaguo la sahihi la Mungu kwake. Hili lipo wazi kabisa ;
vyote yunavyo vitaka na kuvihitaji vimo
ndani ya ufalme wa Mungu. Maana yake sasa ni kwamba ikitokea mtu amepishana na
kanuni na vigezo vya ufalme wa Mungu lazima upishane na majibu yake kutoka kwa
Bwana Yesu; Mungu mkuu.
Majibu na miujiza yetu imefungamanishwa na ufalme, na ufalme
ndiyo kitu pekee kilicho mfanya Yesu aje duniani kutuokoa na kuturejeshea
ufalme; Mathayo 3:17, Tokea wkati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni
; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Ufalme wa Mungu ndiyo kila kitu kwetu. Ndani
ya huo ufalme yumo mke na mume wako na vyote unavyo vitamani maishani mwako.
KUMBUKA:
Unahitaji kuutafuta
kwanza ufalme wa Mungu na haki yake ili kumpata mke / mume ataokaye kwa Bwana. Mithali 19:14, ….mke mwenye busara mtu
hupewa na BWANA. Ukiukosa ufalme
utapa mke au mume lakini siyo mwenye busara bali mpumbavu; na unajua tena kuwa
mke mpambavu huivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Mithali 14:1
ii. Usitafute mke au mume:
Kitabu cha Mwanzo 2:7,15,18-25 kinatupa picha
kamili juu ya mchakato mzima wa kumpata umpendae. Hapa tunaona wazi Mungu ndiye
aliye husika kwa asilimia zote wakumtafutia Adamu mke au mwenzi wa kufanana
nae. Katika sura na mistari hii tunaona Mungu anampa Adamu wajibu wa kuilima na
kuitunza bustani ya Edeni. Na popote palipo na wajibu lazima pawe na haki hali
kadhalika na kinyume chake vivyo hivyo. Na kwa msingi huo hatumwoni Adamu
akihangaika kutafuta mke huku na kule kama wengine wafanyavyo hivi leo, ana
hama kanisa moja hadi jingine kutafuta mchumba , anachumbia huyu mara yule
vurugu tupu, lakini hapa Adamu alitulia na kujikita kwenye wajibu [kazi] yake ya kuilima na kuitunza bustani ya Edeni na
ndipo Mungu mwenyewe akaona si vema
Adamu aendelee kuwa peke yake; akamfanyia na akampa mke ; Eva wa kufanana naye.
Hivyo wajibu wako kama mwana wa Mungu ni kuwa mtu wa ibada na kuwekeza kwenye ufamle wa Mungu kwa viwango vya juu pamoja na kutumika nyumbani mwa Bwana kwa kadri ya nguvu alizokujalia Mungu, kama alivyo fanya Adamu, mpaka akamshawishi Mungu kufanyia mke wa kufanana naye.
KUMBUKA:
Hakuna mtu anayependa kuoa au kuolea na mtu mvivu / mlegevu au mzembe na asiyejituma au kuwajibika vema.
Hivyo wewe jikite kikamilifu katika kumwabudu Mungu na kumtumikia kwa nguvu zako zote na kwa nia safi kabisa katika kanisa lako; na swala la mke au mume mwachie Mungu alishughulikie; cha muhimu kwako mtangazie Mungu nia yako , yaani mwambie haja ya moyo wako yakuwa una maono au ndoto za kuoa au kuolewa kwani ukinyamaza, leo vijana wanasema inakula kwako maana yake; utapata hasara mwenyewe. Kwanini nimesema hivyo; ni kwa sababu wapo vijana wengi nimekutana nao hujifanya kuwa ni wakiroho sana na hulipuuza swala hili la kuoa na kuolewa na utakapo jaribu kuongea nao juu ya jambo hili huondoka hata wasikusikilize kwani wana kuona mtu wa mwilini na umepoa kiroho; chakushangaza unakuta hao hao mwisho wa siku unasikia kapola au kampa binti wa watu mimba au binti kafanya uasherati na kijana Fulani au mara mwingine katoa mimba mwingine mjamzito au mara huyu kaacha wokovu. Usilipuuze swala nyeti kama hili la mahusiano, funguka sema na Mchungaji wako sasa uwe wazi, eleweka na tangaza nia yako.
USHUHUDA:
·
Nikiwa katika moja ya semina ya mahusiano juu ya Misingi ya bora
ya Mahusiano katika moja ya mkoa katika
nchi ya Tanzania; vijana wawili wakike na wakiume walikuwa wakicheka sana kwa
kejeli na wala hawakuwa makini kipindi chote cha mafundisho, kwani waliona
nikama nawapotezea muda wao na mbele zao nilionekana kama mtu niliyekosa cha
kufundisha. Baada ya kulitambua hilo, niliwaambia kwa sauti kuu kuwa; kama
watayapuuza haya niyafundishayo leo, kitakuja kipindi ambacho mtayakumbuka na
kuyatafuta lakini mtakuwa mmekwisha chelewa kabisa na wala hayatakuwa na msaada
kwenu badala yake yata wahukumu. Inatia huruma ; muda mrefu haukupita kabla
vijana hwa wote wawili kkujikuta kila mmoja kwa wakati wake wakianguka kwenye
zinaa na binti kupata uja uzito. Na kwa bahati nzuri nilienda kuhudumu katika
kanisa lao walipo sikia nakwenda hawakuwa tena na ujasiri wakuonana na mimi
kama ilivyokuwa zamani. Nakuombea isiwe hivyo kwako.
KUMBUKA:
Mungu hujishughulisha sana na mambo yetu,
hasa pale tunapo jitoa kikamilifu kwake, 2Petro5:7
iii. jipate kwanza wewe mwenyewe vizuri.
Hii ina maana kabla ya kumpata mwenzi wa maisha au umpendae anza kwanza kujipata wewe mwenyewe, yaani ni ule uwezo wakujitambua au kujielewa vizuri kuwa wewe ni mke au mume wa mtu hata kabla ya kumpata umpendae.
Hii ina maana kabla ya kumpata mwenzi wa maisha au umpendae anza kwanza kujipata wewe mwenyewe, yaani ni ule uwezo wakujitambua au kujielewa vizuri kuwa wewe ni mke au mume wa mtu hata kabla ya kumpata umpendae.
Hivyo sasa ; kitendo cha kujipata mwenyewe ni ile hali au uwezo wa mtu KIJITAMBUA, kujiweza mwenyewe ili usije ukawa mzigo huko uendako. Mwanzo 2:15-25 hapa tunaona Adamu anapewa majukumu na Mungu ya kuilima na kuitunza bustani ya Edeni kama kipimo cha kuya kabili majukumu ya familia. Sio unakuta muoaji na mwolewa wote hawajitambui; akili haja komaa, viungo havijakomaa na hajaandaliwa kuya kabil maisha ya ndoa. Hebu tujifunze kwa watu wamataifa ; utakuta baadhi ya makabila huwa peleka binti zao unyagoni na wavulana hupelekwa jandoni ili kufundwa kuwezeshwa na kupewa nyenzo ili kuya kabili maisha ya ndoa yatakapo fika majira yake. Ndiyo maana Yesu alisema haki yetu isipo zidi ya waandishi na mafarisayo hatuwezi kuurithi ufamle wa Mungu. Sasa vijana hawa wasiyo andaliwa vema , ikitokea wanaanza maisha ya ndoa na wakapata changamoto, au watoto ; utakuta mtoto analia , mama analia na baba naye analia hakuna hata mmoja wakumsaidia mwingine;kwani vichwa vidogo, na ndio maana tumeshuhudia matukio yakinyama katika nchi yetu na hata mataifa mengine ya watoto wachanga kutelekezwa na wengine kutupwa majalalani na hata wengine kutumbukizwa chooni, kuvunjika kwa ndoa , wana ndoa kupigana , hii inaonesha wazi kuwa aliingia kwenye mahusiano akiwa hajitambui na hajui nini kitatokea mbele ya safari. Hili ni tatizo kubwa kwa kanisa la kuwa na msingi mbovu wa ndoa.
Kwa hiyo kwako wewe unaye kisoma kitabu hiki
isikutokee kabisa. Kwani ndoa ikipona kanisa limepona. Adui naye anajua
chochote kitakacho zaliwa kwenyemsingi mzuri wa kifamle kita haribu ufamle wake
., hivyo anawavuruga vijana mapema katika eneo la mahusiano ili apate mlango
wakupitishia mipango yake ya uharibifu. Unakuta vijana wengi leo wamekamatwa na
roho ya zinaa. Tuta anagalaia mbele zaidi madhara ya kufanya ngono kabla ya
ndoa.
KUMBUKA:
Tatizo kubwa la wachumba au wanandoa watarajiwa na wanandoa na kimo, yaani kiwango chao cha ufahamu juu ya tasisi [kitengo] hiki ni kidogo sana.
ANGALIZO:
Kijana; Waone mabinti wote kuwa wazuri lakini usiwabinafsishe wote,bali wako ni mmoja tu.
Mabinti; Waone vijana wote kuwa wazuri lakini usiwabinafsishe wote,bali wako yupo mmoja tu .
Hili tutaliangalia zaidi huko mbele kwenye kipengele cha “ Utamtambuaje aliye chaguo lako.”
Elewa kuwa;
Wanaume wote ni waume lakini sio wote ni waume zako, hali kadhalika wanawake wote ni wake lakini sio wote wake zako.
Tembea ukijua wazi wewe ni mke au mume wa mtu au wewe ni jibu la mtu.
iv. Maombi na Shukurani.
Luka 18: 1-8 ;
Akawaambia mfano, ya kwamba
imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa.
Ni lazima kuomba kabla ya kuchagua nani wakumwoa, hii
itakusaidia kupata mwongozo wa ki-Mungu juu ya mtu sahihi wakuishi naye. Mwanzo
2:18, Mungu anamjua mtu aliye bora kwa ajili yako, ni hekima pekee ya kutafuta
mapenzi ya Mungu.
Ni rahisi kuyajua mapenzi ya Mungu kama tendo la ndoa au ngono
hajahusishwa. Pindi tu ngono au tendo la ndoa likahusishwa katika mahusiano
yenu na hapo hapo mnataka kuyajua mapenzi ya Mungu atawakatilia mbali kabisa
kwa kuwa pofusha na kamwe hamtaweza kuyajua mapenzi ya Mungu. Hii ni kwa sababu
mmevunja kanuni na sharia yake ya HAKUNA
kufanya TENDO LA NDOA kabla ya ndoa.
Kama mmewahi kufanya tendo la ndoa wakati ninyi ni wachumba ;
fanyeni yafuatayo haraka sana:-
§ Ombeni toba ya kweli
mbele za Mungu na;
§ Na kaeni mbali na kusitisha
uchumba wenu kwa muda ili kuutafuta uso wa Mungu. Lengo ndoa yako isiwe kuzimu
hapa duniani bali ndoa yako iheshimiwe kwa utukufu wa Jina la Yesu kristo.
KUMBUKA:
Bora na heri uchumba
mbovu ulio vunjika kuliko kulea ndoa jipu isiyo na amani na furaha.
Ndoa siyo tukio bali
ni maisha; hivyo usifanye mchezo na kuleta masihara au utani kabisa.
Ni vizuri kujiuliza kwanza , kwa nini tunaomba?
ü
Tunaomba kwa ili kumtiisha na kutawala Yule anaye shikilia vitu
vyetu. Kwani yote tunayo yahitajia Adamu aliyauza kwa shetani.
Neno linaweka wazi katika Wafilipi 4:4-7 kwamba tusijisumbue kwa jambo au neno lolote ; maana yake likiwemo hata hilo swala lako la kumpata umpendae, Biblia inasema, “Bali katika kila jambo kwa kusali na kuomba na kushukuru haja zako, [yaani mahitaji yako] zijulikane na Mungu.”
Ni katika wakati wa maombi tunapo mjulisha Mungu haja zetu. Vijana wengi leo hawafanyi maombi kabla ya kumpata mwenzi wa maisha bali wanaomba baada ya kuwa wamekwisha kuona, hili tayari ni tatizo ni sawa na mtu anaye jitekenya mwenyewe na kisha kuanza kucheka.
Hupaswi kuanza mahusiano kabla ya kufanya maombi.Tuomba ili tupewe kuona sawasawa na mapenzi ya Mungu [ kuanza na Mungu].
Maombi ni ishara ya kuhitaji msaada kwa Mungu na imani ni kupokea kwa shukurani uliyoomba mbele za Mungu.
Ukiisha mwona umpendae huhitaji kuanza kuomba kwa Mungu bali ni kwenda kwa Mchungaji wako ili akupe mwongozo na sura kamili ya mchakato mzima wa kufanikisha safari yako ya ndoa. Mara utasikia mwingine akisema nataka nihakikishe kama ni kweli Mungu au ni shetani. Kama una ushirika mzuri na Roho mtakatifu huhitaji kwenda kuomba ili kupata uhakika wengi wao kutaka uhakika shetani amewamalizia huko huko. Kama una Roho Mtakatifu siyo kazi ngumu kuyajua yaliyo mapenzi ya Mungu.
ANGALIZO :
Kuna mambo ya kuomba na yapo mambo mengine ya wajibu, yanakutaka kuwajibika; maombi siyo mbadala wa mambo ya wajibu wako. [ Prayer is not a substitute for your Responsibilities].
·
Usilifanye jambo la kimwili kuwa la kiroho , kwani utakuwa
unasema uongo wa kiroho kwa kulazimisha biblia kusema kitu ambacho haisemi.
v. Jitoe vema na kikamilifu kwa ajili ya utumishi.
Neno liko wazi katika Mwanzo 2:15; 29:1-30. Adamu alijitoa vema kuilima na kuitunza bustani ya Edeni ambapo Mungu alimweka na kumpa kazi; hata ikamshawishi Mungu kumtafutia msaidizi wa kufanana naye. Lakini pia tunamwona mtumishi wa Mungu Yakobo anatumika kwa miaka mingine saba zaidi na kuwa miaka kumi na nne ili tu ampate Raheli msichana aliye mpenda, na mjomba wake Labani tunaona anamtoa Raheli na kumpa Yakobo awe mkewe.
Binti isibweteke tu yaani usikae kwa hasara; mkao wa kuhurumiwa hurumiwa waoaji nao wanaangalia kichwa cha mtu [ufahamu wake na uwajibikaji]; fanya kazi , jishughulishe kwa bidii ili ulete heshima kwenye ndoa yako. Usikalie kupaka rangi kucha na hina na kujipodoa [kujiremba] badala ya kujishughulisha; sio kwamba kujipamba ni vibaya ni jambo zuri sana ila kazi kwanza kisha vipodozi ndio vinafuata.
Mwanamke anafananishwa na merikebu iliyo jaa shehena-mali; Mithali 31:10-31 na huamka mapema ilikutafuta mali,chakula n.k. kwa ajili ya familia yake.
Endelea kuwa mwaminifu katika Ibada na huduma [utumishi] na Mungu aonaye sirini na aijuae haja ya moyo wako atakutendea mema.
SURA YA NNE:
SABABU
ZAINAZOFANYA KIJANA ACHELEW E KUOA AU KUOLEWA.
Zipo sababu nyingi zinazo pelekea kijana wa kike au wa kiume kuchelewa kumpata mwenzi wa maisha yake; sababu hizi zipo katika makundi makuu matatu kama yafuatavyo:-
A/. Vifungo Vya Sababu Binafsi B/. Vifungo Vya
Sababu Za Mila, Desturi na Utamaduni na
C/. Vifungo Vya Sababu Za Kiroho
KUMBUKA:
Kifungo ni hali ya mtu kuwekwa katika hali ya
utumwa wa kitu Fulani ; lakini pia
kifungo kinaweza kuwa kitu chochote kinacho mfunga au kumzuia mtu na kumfanya kushindwa kufanya
jambo alitakalo. [ kuwekwa kizuizini / kunyimwa au kunyang’anywa uhuru wako ]
A. Vifungo Vya Sababu Binafsi:
Hizi ni sababu za mtu
binafsi na vifungo vya kujitakia
mwenyewe, kimsingi sababu hizi zimejengwa juu ya mchanga [ vitu ] na siyo
mwamba [ Yesu ].
Ifuatayo ni baadhi tu
ya mifano ya Vifungo Vya sababu binafsi:
i . Wengi huwa wamekwisha fanya maamuzi ya nani ataishi naye .
i . Wengi huwa wamekwisha fanya maamuzi ya nani ataishi naye .
Pamoja na kuwa tayari ana maamuzi yake juu ya mtu wa kuishi naye bado anaenda kumdhihaki Mungu kwa kumwomba ampe mke au mume sahihi wa kuishi naye. Kwa sababu hiyo inakuwa ni vigumu kwao kumpata mtu wa mapenzi ya Mungu na pia inamuwia kazi Mungu kukupa au kukuonyesha mke au mume wa kusudi lake kwani tayari umekwisha kufanya maamuzi ndani ya nafsi yako, hivyo kitu pekee atakacho kifanya Mungu hapo ni kunyamaza tu; utamwomba wala hata jibu utamwita kwa machozi wala hata kusikia. Mithali 16:1-5
ii . Kuwa na vigezo binafsi;
Vijana wengi sana katika swala la kuoa wana vigezo vingi ambavyo wameviweka juu ya mke au mume atakaye ishi naye. Ni vema kuwa na vigezo; mfano mwingine anataka mwenye mwanya, mfupi, mrefu, mweupe, mweusi, awe kabila Fulani, msomi, mfugaji,mkulima, mnene, mwenye gari, mwenye nyumba, aliye nizidi elimu, bikra, mwenye makalio makubwa, mwembamba, n.k .Wengine hudai ili waowe lazima kwanza ajenge nyumba au apate kiasi fulani cha fedha; Pamoja na hayo uwe tayari kuyaruhusu mapenzi ya Mungu; kwani Mungu ndiye anaye kupa mke au mume. Hivyo wengi hujikuta muda wa Mungu kwa wao kuoa au kuolewa umepita kwani hawakuwa tayari kumsikiliza Mungu bali wao ndio walitaka Mungu awasikilize hii ni hatari sana. Tutaliangalia jambo hili kwa kina mbele kidogo.
·
Namna ya funguliwa vifungo vya sababu binafsi ni mtu mwenyewe
kukubali kugeuzwa kufanywa upya nia yake . kuchukua hatua za makusudi kuachana
na tabia za dunia za mwilini. Ambazo hutoweka mara. Lakini mapenzi ya
Mungu yana dumu milele. Tujifunze kwa mwalimu wetu Yesu , ukweli Yesu alitanza mapema hisia zake za
kutokuwa tayari kufa msalabani kwa kukataa kukinywea kikombe cha mateso aliomba
hivyo mara tatu akasema lakini si kama
nitakavyo bali mapenzi yako yatimizwe. Na yalipotimizwa mapenzi ya Mungu
yakasababisha furaha na amani kwa ulimwengu wote. Ndani ya mapenzi ya Mungu
kuna amani , hakia na furaha katika Roho Mtakatifu vinatawala. Mathayo 26:36-47
Wala msiifuatishe
namana ya dunia hii; balimgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika
mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:2
iii. ugonjwa au
udhaifu wa mwili [ tatizo la kiafya ].
Kijana kama unatatizo
la kiafya eleza mapema ili upate msaada haraka. Hakuna linaloshindikana kwa
Mungu, kwake yeye amwaminie.
·
Nilisikia ushuhuda wa binti mmoja aliye olewa na kumbe hakuwa na
sehemu za siri , jambo hili lilileta mtafaruku mkuwa kwa mwanaume ikabidi aende
kutoa taarifa kwa mchungaji kuwa mwenzake hana vitendea kazi yaani sehemu za
siri, kijana alifanya hivyo ili
afunguliwe kuanza mchakato upya. .
·
Lakini pia hata kwa vijana wakiume wengine wana matatizo ya
kiafya , anaogopa kusema mapema ili apate msaada haraka , sasa mtu kama huyu
unaweza kushangaa umri unaenda hana mpango wa kuoa unadhani pengine anataka
kijipanaga kama ilivyo kwa vijana wengi hutumia kauli hiyo ya kujipanga ili
kumaliza mjadala huo, kumbe wengine siyo kujipanga bali wagonjwa kabisa [ kale
kaugonjwa kakushindwa kutoa huduma ya tendo la ndoa ] , ushauri hebu funguka
kijana usife na tai shingoni Yesu anaponya.
B/. Vifungo Vya Sababu Za Mila, Desturi na Utamaduni:
Hivi ni moja ya
vifungo vinayo litesa kanisa na vijana wengi leo. Utakuta kijana ana amriwa na
kuongozwa na mila za ukoo wake au kabila lake. Hii ni hatari sana. Elewa kuwa mke
hatolewi na kabila au ukoo bali na Bwana.
USHUHUDA:
Nikiwa moja ya mikoa
ya Tanzania nikiwa nafundisha somo la mahusianao hasa kipengele hiki cha sababu
za vijana kuchelewa kuoa au kuolewa, nilimwona kijana mmoja ameshika shavu huku
akiniangalia kwa huruma akiashiria kuwa yupo kwenye kifungo na hajui atoke vipi.
Wakati wa maswali na majibu ; akauliza kuwa, je , afanyeje kwani mila za kabila
lao na wazazi wake wana taka aoe binti wa kabila Fulani na ole wake asifanye
hivyo hatapewa mahari ya kuolea na pia atatengwa na ukoo, hajui afanyeje yuko
katikati ya bahari.
·
Jibu lilikuwa rahisi sana, Mithali 19:14, Bwana ndiye atoaye mke
na siyo kabila, ukoo wala wazazi. Kumbuka mke huyo hatakwenda kuishi na kabila
lako wala wazazi wako na hauoi kabila bali mke. Nikamwambia piga teke mila na
desturi za kipagani msikilize Mungu ; na kingine kinacho oa, siyo mahari bali
ni wewe. Kijana alifurahi sana kupita maelezo; baada ya muda si mrefu
alinipigia simu akinijuza kuwa Bwana amemtokea amepata mchumba mara tu ya
kufunguliwa na mafundisho kwenye semina ile.
Haleluya , sifa kwa Yesu.
C/. Vifungo Vya Sababu Za Kiroho:
i/. Sababu ya kujitamkia maneno ya kinyume [
negative words].
Biblia imeweka wazi kila jambo; nabii bora wa maisha yako ni wewe mwenyewe hivyo uwe makini sana juu ya kile unacho kisema juu yako na wengine kwani maneno yanaumba kwa sababu maneno yote ni roho; Yoh. 6:63. Pia Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazo ya midomo yake.Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. Mithali 18:20-21; Mithali 6:2. Bado Neno linasema wazi kuwa; Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo- Mithali 23:7.Mfano wale wapelelezi 12 waliotumwa na Musa kuipeleleza Kanani 10 wakaja na taarifa mbaya wakisema wao ni wasawa na mapanzi sawasawa na ukiri wao hawakuingia Kanani –Hesabu13:32-33; lakini Yoshua na Kalebu walikataa kuwa mapanzi kwani walimwamini Mungu wao na ndio pekee walioiingia Kanani sawasawa na ukiri wao. Hesabu 14:30.
Eneo hili la kukiri kushindwa, limewakwamisha watu wengi bila wao kujua tatizo ni nini; hasa akina dada wengi ndio wahanga wa eneo hili; hii ni kwa sababu mbalimbali kama vile kubakwa, majeraha katika nafsi ya kuachwa au kukataliwa na mchumba au wachumba hata kufikia hatua ya kujitamkia maneno magumu kwa kusema hawataki kuolewa tena au kuoa. Sasa unapita muda wanataka kuolewa au kuoa wanaanza kumuomba Mungu ili awape mume au mke wakati huo wana sahau kwamba kuna kipindi cha nyuma walikwisha kutamka maneno yakujifunga nafsi- Hesabu 30:2-16 na shetani kama mwindaji ameyashikilia katika ulimwengu wa roho; hivyo ni lazima uende mbele za Mungu kwa kuomba toba na rehema ili upate kibali na kisha kuyafuta hayo maneno kwa damu ya Yesu ili kumwondolea shetani uhalali wa kukushikilia, kwani bila kufanya hivyo itakuwa ni shughuli pevu kupenya hapo.
KUMBUKA:
Hutaishi zaidi ya kile unacho kisema, maneno uyasemayo ndiyo
huwa ramani ya maisha yako. Angalia sana na uwe mwanagalifu juu ya kile kinywa
chako kina kiri.
ii.
Uovu, Dhambi na Makosa:
……….Lakini maovu yenu
yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu , na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia. Isaya
59:1-2
Uovu ; ni ile tabia ya
kuzoelea kufanya dhambi. Kimsingi uovu ni mavuno ya makosa, dhambi au uasi uliyo fanywa na watu wengine kabla
yetu na sasa hawapo tena.
Baba
zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. Maombolezo
5:7
Kama kuna dhambi kijana umefanya na bado haujaitubia inaweza kuwa ni kikwazo cha kukuchelewesha kwenda kwenye hatima yako njema na kujikuta umri unakwenda, wala hushituki unaona ni hali ya kawaida.
Kama kuna dhambi kijana umefanya na bado haujaitubia inaweza kuwa ni kikwazo cha kukuchelewesha kwenda kwenye hatima yako njema na kujikuta umri unakwenda, wala hushituki unaona ni hali ya kawaida.
Neno la Mungu lipo wazi linasema, “ Afichaye dhambi zake
hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atasamehewa na kupata rehema.
Mithali 28:13.
Dhambi humwondolea mtu kibali mbele za Mungu; dhambi humfanya
mtu kuwa adui wa Mungu; dhambi humtoa Mungu ndani ya mtu na kujikuta unaishi
maisha ya uasi ,yaani ya kupingana na Neno la Mungu na mapenzi yake makamalifu . 1Yohana
3:4…… dhambi ni uasi.
KUMBUKA:
KUMBUKA:
Kama kuna jambo na silaha pekee anayoitumia shetani kutuzuia kwenda kwenye mema yetu na kumpa adui uhalali wa kutumiliki; ni dhambi isiyo tubiwa. Toba ya kweli hurejesha kibali kilicho potea na ujasiri; kwani dhambi huondoa kibali mbele za Mungu; mtu akitenda dhambi kwenye ulimwengu wa roho anakuwa kama amepakwa mavi, unajua wazi kuwa hakuna mtu anaye furahia harufu ya mavi, kadhalika na Mungu naye haifurahii dhambi. Mfano wapo watu wanao toa mimba au kuwatupa watoto walio wazaa ; watu kama hao nao kupata mke au mume huwa inakuwa kazi kweli kweli. Hivyo nenda mbele za Mungu ukatengeneze ili upatane kwanza na Mungu. Yakobo 4:7 na Mitali 3:1-4
iii. Sababu za kipepo.
Katika kipengele hiki tutaongelea mambo mawili hivi;
·
Jambo la kwanza ; yawezekana wazazi au ndugu wamekwisha mtoa
huyo kijana kwa mizimu yao ya ukoo kama dhabihu kwa sababu ya mila zao.
·
Jambo la pili; yawezekana alipatikana kwa njia za kipepo au
za kishirikina [ waganga]. Na hapa nimekutana na kesi kama hizi nyingi kwenye utumishi wangu. Akina dada wengi
ambao wazazi wao au wao wenyenye waliwahai kujihusisha na maswala ya mila kama
vile kushiriki kwenye sherehe za matambiko na kwenda kwa waganga na hata
wengine wakapewa majina maalumu ya kiukoo nakujikuta kwenye wakati mgumu
wakuolewa na mapepo na kuharibiwa hatima zao. Siri moja ni hii yapo mapepo
mengine yanapo kuwa yamemwoa binti hayako tayari kukuruhusu kuolewa au
kushiriki na mwingine , tendo la ndoa; hivyo lazima yalete upinzani mkali pale
utakapo taka kuolewa ili tu usiolewe au kuoa hasa kama hayo mapepo yamekwisha
kufanya na yana endelea kufanya tendo la ndoa na wewe. Lakini habari njema ni
kwamba hakuna linalo shindikana kwa Mungu; Kwake yote yana wezekana Marko 9:23
na kila pando asilo lipanda Baba lazima ling’olewe Math.15:13, Yer.1:10
USHUHUDA:
Nimekutana na mabinti wengi niliyo fanya nao maombi ili kuzizibiti hizo roho za kuingiliwa kimwili na mapepo na Mungu amewafungua wengine tayari wana familia na watoto. Japo awali binti mmoja aliniijia akisema kuwa akisumbuliwa na ndoto mbaya za makaburini analishwa nyama na kubakwa na mapepo usiku; na kila kijana anapokuja kwa lengo la kutaka kumwoa ana mchukia na kumfukuza bila lidhaa yake baada ya kitendo hicho anajutia sana ; kumbe hakujua kuwa yale mapepo ndiyo yaliyokuwa kikwazo cha yeye kuwachukia vijana na kutokuwa tayari kuolewa, lakini baada ya maombi alifunguliwa na sasa yuko huru na ameolewa na ana watoto.
Mwingine huyu yeye alipewa jina la ukoo likiambatana na ibada ya kuchinja mbuzi kama sehemu ya tambiko la kupitisha roho za ukoo ndani yake naye alipata mateso ya kuingiliwa kimwili na mapepo na ndoto za kuongea na wafu na alikimbiwa na wachumba bila kujua sababu za msingi; Binti huyu hakujua kwa nini yanamfika haya mpaka alipotambulishwa kwa Yesu. Mara nyingi mabinti wanaoingiliwa kimwili na mapepo haya huachiwa halufu mbaya inayo waondolea kibali mbele za watu. Ila pamoja na yote hayo yupo Yesu mwenye uwezo wa kurejesha kibali cha ki-Mungu kwako tena. Huyu binti yuko huru sasa kwa jina la Yesu.
vi. Kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati.
Mhubiri 3:1- Anasema, “ kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu.” Swala la kutafuta mke au mume lina majira yake kama wewe ni mwanafunzi nakusihi soma sana tena kwa bidii wakati ukufika wa wewe kuoa au kuolewa itakuwa kama ilivyo pangwa na Mungu ; nimeeleza huko mwanzo kuwa usiyachochee mapenzi wala usi ya amushe mpaka yatakapo ona vema yenyewe . Hivyo usihangaike kutafuta mke au mume utateseka bure endelea na wajibu wako kwa bidii sana kama ni huduma, hudumu sana na kama ni kazi fanya kwa bidii na kama ni kusoma soma sana na Mungu atakutendea mema.
v/. Hofu ya maisha:
Wapo vijana wengi
wanaogopa kuchukua hatua ya kuoa kwa hofu ya kesho; kwamba ataishi vipi, atakula
nini, atatoa wapi mahari n.k. Yote nikutata kuiga maisha ya mtu Fulani. Hii inachangiwa na kukosa maarifa sahaihi ya
misingi bora ya mahusiano.
Hofu ni moja ya silaha
za shetani anayo itumia sana kwa kuwaogofya wana wa Mungu ili wasichukue hatua.
Hofu ni
kama chumba cha giza kinacho mjengea mtu
hali ya mtazamo hasi juu ya jambo Fulani kuona haiwezekani.
Biblia inasema, Kwa
kuwa hamkupokea tena Roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea Roho ya kufanywa wana, ambayo
kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Warumi 8:15
SURA YA TANO:
MADHARA
YA ZINAA AU NGONO KABLA YA NDOA.
Zinaa; ni tamaa mbaya ya kufanya tendo la
ndoa.
Miongoni mwa dhambi za
uchafu na zinazo mkasirisha Mungu zilizo beba uovu na nguvu ya mapatilizo ni
dhambi ya uchawi, uuaji na zinaa.
Wapo wangine husema
kuwa tufanye dhambi kisha tutatubu tu. Kabla ya kutenda dhambi au kuwaza toba , angalia gharama ya dhambi
kufanyika .
Bilblia inasemaje kuhusu
dhambi hiyo na toba yake.
KUMBUKA:
Kwa maana mshahara wa
dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni
uzima wa milele katika kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 6:23
Upo ushahidi wa
kibiblia na kibinadamu juu ya nguvu ya dhambi ya zinaa, hasara zake na matokeo
yake katika maisha ya mtu.
Nguvu ya dhambi na
hasara zake katika maisha ya kiroho na
kimwili ndiyo ilisababisha hata makanisa nawachungaji kuweka sharia na
utaratibu mkali wa kutoa adhabu ya kusimamishwa huduma, kutengwa kwa kipindi
fulani au kufukukwa kwenye ushirika watu wanao ingia kwenye shimo la dhambi hii
ya zinaa.
Zifuatazo ni baadhi tu
ya madhara ya zinaa au ngono nje ya ndoa:
1. Zinaa inaua [
nafsi ]utu wa ndani:
Zinaa inajeruhi utu wa
ndani [ nafsi ]
Roho ya mtu
itastahimili uddhaifu wake; Bali roho ilivunjika nani awezaye kuistahimili?
Mithali 18:14.
Lakini pia mtume Paulo
kwa
1Wakorintho 6:18; Anasema,
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye
afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Mtu azinie na mwanamke
hana akili kabisa, afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi yake na atapata
jeraha za kunjiwa heshima; wala fedheha yake haitafutika. Mithali 6:32-33
KUMBUKA:
Dhambi zote zinaweza
kufutika isipokuwa ya zinaa.
2. Zinaa humvunjia
mtu heshima:
Zinaa humwondolea mtu
heshima yake mbele ya jamii husika, hivyo humfanya kudharauliwa na kila mtu. …………..atapata
jeraha za kunjiwa heshima; wala fedheha yake haitafutika. Mithali 6:32-33
3. Zinaa
hufedhehesha:
Mtu afanyaye zinaa
hujidharirisha na kupata aibu au fedheha kwenye jamii inayo mzunguka. ………wala
fedheha yake haitafutika. Mithali 6:32-33
4. Zinaa inafuta
maono na ndoto za mtu:
Zinaa humfanya mtu
apoteze mwelekeo [ vision ]wa maisha yakena kushindwa kutimiza ndoto za maisha
yake.Ikawa
baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu , akamwambia, lala name. Mwanzo 39:7
Ndiyo maana Yusufu kwa kulijua hilo alikataa
kulala na mke wa bwana wake, akisema; Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi,
wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe umkewe. Nifanyeje ubaya
huu mkubwa nikamkose Mungu? Mwanzo 39:9
5. Zinaa humwondolea mtu ujasiri wa kuikemea dhambi:
Mtu afanyapo zinaa
hukosa ule ujasiri mbele za Mungu na wanadamu tena , kwani tayari kunashida
imeingia ndani yake. Hivyo moyo wake unajaa hukumu. 1Yohana 3:21-22, Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; na lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kutenda
yampendezayo machoni pake.
6: Muunganiko wa
nafsi:
Tendo la zinaa ni
agano; hivyo huwaunganisha nafsi [ akili, hisia, utashi, fikra au dhana na ufahamu ] za
watu wawili na kuwa mwili mmoja. Ndiyo maana sasa unaweza kukuta mtu
ameokoka lakini kabla ya kuokoka alikuwa na mpenzi wake aliyekuwa akifanya naye
zinaa, utashangaa wengine hata baada ya kuokoka kama atakuwa hajafunguliwa
vifungo vya nafsi ni vigumu kuacha huwa wanaendelea na maisha yao ya duniani ya
zinaa. Hii ni kwa sababu kunamuunganiko wa nafsi mbili hizi; ni mpaka
afunguliwe maagano na vifungo vya nafsi.
1Wakorintho 6:16; Au
hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja
7. Zinaa hukiingiza
kizazi chako kwenye vifungo:
Leo
kuna watu wengi wanapata mateso ambayo kimsingi wao siyo wahusika kabisa, bali
wamejikuta wamo kwenye mazingira magumu na hawajui wanatokaje. Hii yote ni kwa
sababu ya misingi iliyo wabeba ilikuwa mibovu.
Baba zetu walitenda
dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. Maombolezo 5:7 . Tazama pia Zaburi
51:5, Daudi anasema; Tazama , mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu
alinichukua mimba hatiyani.
Wasomaji wazuri wa
Biblia utakuja kugundua kua anguko la mfalme Daudi ya kuzini na mke wa Uria
2Samweli11:1-5; 12:9,13,14 utakuja
kugundua kuwa alikuwa akitembele misingi
mibovu ilikuwa bado haijashughulikiwa ya bibi yake ni Rahabu Yule kahaba , Mathayo
1:1-17. Ndiyo sasa Mfalme Daudi anagundua kuwa misingi iliyombeba haiku salama
kabisa na ananza kuishughulikia kwa toba ya kumaanisha kabisa , soma Zaburi 51
yote.
8. Zinaa huambukiza
magonjwa :
Wapo watu leo wanalia
maana afya zao ni mgogoro, hii ni kutokana namaambukizi ya magonjwa yatokanayo na kufanya zinaa na mtu mwenye maambukizi. Mfano wa
magonjwa haya ni UKIMWI, KASWENDE, GONOREA, FANGASI n.k
9. Zinaa ni mlango
wa mapepo kwa mtu:
Kwakua zinaa ni tendo
linalo unganisha watu wawili kiakili,kihisia, kiroho na kimwili ; basi upo
uwezekano mkubwa sana wa mmoja aliye na roho chafu kumwingia mwingine kama vile
tu mtu anavyo weza kupata maambukizi ya magonjwa ; hata mapepo vivyo hivyo.
SURA YA SITA:
MAMBO
YA KUYAELEWA KATIKA MAHUSIANO.
i. Maisha au hali ya mwenzi wako lazima ikuguse ; bila kujali hali,mazingira,mali,elimu,ukoo,kabila n.k
i. Maisha au hali ya mwenzi wako lazima ikuguse ; bila kujali hali,mazingira,mali,elimu,ukoo,kabila n.k
ii. Usimwoe au usiolewe na mtu kwa kumtamani ; kwani ukimtamani binti au kijana lazima utaanguka naye au utazini [utatenda dhambi tu]
iii. Ukimpenda mwenzi wako utamjali, utamuheshimu na kumthamini kwa viwango vya juu; na wala hutasikiliza maneno ya kukuvunja moyo ya watesi au walioshindwa watakayo sema dhidi ya umpendae. Wahenga au wazee wetu walisema, “Akipenda chongo huita kengeza.” Neno nalo linasema, “Upendo hustili wingi wa dhambi.”Maana yake ukimpenda mtu hutayaona madhaifu,makosa na mapungufu yake. Hivyo pendo ni kama kifuniko. Tazama 1Petro 4:8 na 1Kor.13:1-10
iv. Ukiwa mtu wa kuangalia au kuchunguza sana lazima utabagua ; utakuwa mbaguzi [selective];
Kuangalia ni ule uwezo wa kutambua mambo ya ndani [siri] Kama Adamu angeona hali ya ndani ya Eva au Hawa asinge mkubali, maana angeona anguko.[Mambo ya siri ni ya Bwana na yaliyo wazi hayo ni yetu Kumb.29:29]
v. Ukiwa mtu wa kutazama; nilazima utapenda na kujali [ kutazama kunashughulika na mambo ya nje ambayo ndio tumejaliwa kuyaona.
vi. Mahusiano yanaanza Kwa kutazamana. Rejea Mwanzo 2:18-23.
vii. Hakuna kupenda bila gharama. Kupenda ni kutoa [kupenda kunaambatana na kutoa ] Mfano; Mungu alimtoa Mwanae kuwa sadaka ya ulimwengu kuokolewa; hii inafunua nguvu ya upendo. Tazama Yoh.3:16 nasi tunapaswa kujitoa kwa ajili ya wengine .1Yoh.3:16 na Mwanzo 29:1-30 inaonyesha jinsi Yakobo alivyotumika kwa miaka kumi nne ili kumpata Raheli kama nilivyo eleza hapo mwanzo. Utakuwa tayari wewe kuumia ili umpendae ajisikie vizuri [afurahi]. Kwa mfano utakuwa tayari kutembea kwa miguu au kushinda njaa ili umpendae apande gari au ale chakula. n.k.
viii. Tujenge mahusiano ili tupate akili ya kujuana vizuri. Nilazima umjue vizuri mtu unae fanya nae mahusiano. Kumbuka kipindi cha uchumba ndicho cha kuchimba msingi na kufanya matengenezo ya nguvu sana; ndicho kipindi cha kushughulikia kila aina ya tabia mbovu pengine katika ukoo au mtu binafsi.
ix. Kuna msemo usemao, “Ukimkosa umpendae basi jitahidi kumpenda utakaye mpata.”Maana yake kama wewe unavaa kiatu namba saba ukaenda dukani ukakiona kiatu kingine kizuri ila chenyewe ni namba tatu na ukaamua kujichukulia kwa raha [furaha] zako ukweli kitakubana kisawasawa na kitakutoa sugu na hata kitakufanya kutembea kwako kuwe kwa namna isiyo ya kawaida mpaka utakapo zoea; Hayo ndio baadhi ya maisha ya wanandoa waliopeana wenyewe na sio Bwana, ushauri wangu kwako lidhika na vumilia kwani uliyataka mwenyewe mpaka kifo kitakapo watenga.
x. Weka mipaka [kiasi] katika mahusiano yenu ili msije mkampa ibilisi [shetani] nafasi yakuwatega na kuiharibu misingi kwa kuwa angusha dhambini na kulitukanisha kanisa kwa jamii inayolizunguka; kwa maana sisi ni barua iliyowazi tunasomwa na kila mtu hivyo somekeni vizuri mbele ya mataifa.
xi. Usiwe na mazoea pamoja na mazungumzo [maongezi] yasiyo mpa Mungu utukufu. Biblia inasema, “………Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema; yaani mwenendo wa maisha unakuwa mbovu na mchafu. 1Kor.15:33; Hivyo kijana jiheshimu, jua wewe ni mtumishi wa Mungu na usikae kihasara hasara.
xii. Kijana ukikataliwa na binti au binti ikatokea umektaliwa na kijana basi usimchukie huyo kijana na kumwona mpagani au amepoa kiroho bali wewe mshukuru Mungu kwani amekuponya na tatizo, msiba, janga au mzigo; Zaidi ya yote mpende kama ndugu katika Bwana na kumwombea ili Mungu amkutanishe na jibu lake sahihi, nawe uende ukainue kiwango chako cha Ibada na Utumishi uta mshangaa Mungu atakavyo kutokea na kukujibu kwa moto. Hii ni ajabu utakuta kijana anakuchukua hatua ya kuhama hata kanisa au hata pengine mtaa au mji ati kisa amekataliwa na binti au na mvulana, huo ni utoto ukue sasa upone sasa kwa jina la Yesu.
USHUHUDA:
Ni ushuhuda wa binti mmoja aliye zimia baada ya kuwa kijana amemkataa mbele ya mchungaji wake. Nilimwuliza kulikoni mpaka kupoteza fahamu? Akanijibu akiwa anamshutumu yule kijana akisema, “Yule kijana hajaokoka bali ni mjumbe au wakala [agent] wa shetani anajifanya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu, sikutegemea kuwa angenikataa mbele ya mchungaji wake! Mimi nilimwambia kuwa nimeota ndoto ,nimeona amenishika mkono ananipeleka shimoni [ kuzimu] naona alijisikia vibaya japo mimi sikuwa na maana ya kumwacha bali tuendelee kuikataa hali hiyo; kumbe mwenzangu alichukia na tulipofika kwa mchungaji wake ili kuthibitisha pendo letu kwake; hivyo alipoulizwa kama ananipenda kweli na yupo tayari kunioa, alikataa kabisa kitendo kile kikanisababishia mshituko na kuzimia kwa takribani saa moja hivi.”
Nami nilimweleza ukweli wote kuwa yule kijana hakua wakala [ agent ] wa shetani bali yeye yaani binti ndiye mwenye tatizo kwani hakuwa na ufahamu wakutambua yupi ni chaguo lake sahihi. Hivyo nikamwambia amshukuru Mungu kwani amemponya na matatizo mazito ambayo yangemtesa maisha yake yote ya ndoa. Sasa binti wa watu anasonga mbele kwa amani tele na mipango yake; na huyu kijana naye tayari amekwisha kuoa anaendelea mbele na maisha yake kwa amani nyingi kabisa.
Hivyo na kushauri tulizana usije ukatuletea balaa la kuzimia na kutupa kazi ya kupepea na pengine usiinuke; mwenzako yeye aliinuka, tuna mambo mengi ya utumishi na siyo kazi ya kuwapepea watu wasiotaka kujifunza .
xiii. Kijana uliyeokoka usijaribu kumtongoza binti ; na wewe binti usikubali kutongozeka, ukikubali nawe unamatatizo makubwa.
Kutongoza ni kujaribu
kumshawishi binti au kijana akubaliane na jambo asilolitaka kulifanya ili alifanye.
Wewe eleza ukweli wako wote wa maisha usijipachike vyeo , nafasi na majina makubwa [mazito] yanayo kukataa mwisho wake ni aibu na fedheha utakapo umbuliwa kwa ukweli kujulikana.
Wapagani ndio wanaotongoza [danganya] ili tu wakubaliwe ombi lao.
Hata leo mabinti nao wana watongoza wavulana [wana washawishi] kwa namna mbali mbali mfano kwa wananavyoonekana [ mitindo ya uvaaji wa kuacha na kuonyesha sehemu nyeti], mali au fedha n.k; Leo kuna msemo wa vijana usemao, “unanitega” ukimanisha kumshawishi mtu kufanya kitu asichokuwa amekitarajia.
Onyo : Binti wa Yesu vaa vizuri kwa na adabu na heshima zote, jistiri upendeze . Msiwatege vijana kwa mavazi yako ya kikahaba yenyekuonyesha maungo au sehemu nyeti za mwili. Mihtali 7:7-27
Na wewe kijana unayetegwa na ukategeka una matatizo mazito unahitaji msaada wa Mungu wa kufunguliwa ufahamu na kugeuzwa akili zako na kufanywa upya nia yako na Bwana na unapaswa kufanya jitihada za makusudi za kuikwepa hiyo mitego kwani ipo wazi.
Rejea kwa rafiki yetu Yusufu ; mtumishi kijana aliye timua mbio mbele ya mke wa bwana wake Potifa
Mwanzo 39:7-12
xiii. Usioe kwa kumhurumia binti au Usiolewe kwa kumhurumia kijana; tafadhali sana usije ukamkubali mtu kwa kigezo cha kumhurumia; eti kwa madai ya kumpunguzia matatizo au kuondoa kero za kukufuatilia kila mara. Kumbuka hatuoi au kuolewa kwa kigezo cha kuhurumiana bali bali kwa kupendana kidhati na kwa mapenzi ya Mungu.
xiv. Ni vema kuweka vigezo kwa mtu ambaye ungependa awe mwenzi wa maisha yako; mfano ungetaka awe asiye soma,msomi, mrefu, mfupi, mweupe, mweusi, mrefu, mfupi, masikini, tajiri, mwembamba, mnene-bonge, mwenye kitambi n.k. Lakini uwe tayari kuyaruhusu mapenzi makamilifu ya Mungu kuchukua nafasi ya kwanza kwani Mungu kamwe hata kuangusha [hata ku- let down] yeye anamjua vizuri mke au mume atakaye kufaa. Mfano Yesu hakuwa tayari kwenda kufa msalabani lakini katika maombi yake aliyaruhusu mapenzi ya Mungu na mapenzi ya Mungu yakatimizwa yakufa msalabani na kusababisha ukombozi mkuu kwa ulimwengu mzima. Mathayo 26:39-44.
xv. Mke hatuonyeshwi kwenye ndoto bali tunaona waziwazi kabisa kama ilivyokuwa kwa Adamu. Mwanzo 2:19-25; Japo Mungu anaweza kufanya mambo yote , anaweza kukuonyesha kama itabidi au pia akaamua kusema kwa sauti na wewe juu ya huyo umpendae. Ila unapaswa kuwa makini sana kuliko kawaida kwenye eneo la kuonyeshwa na kusema kwa sauti kwani wapo mabinti wengi wameumizwa sana kwa kudanganywa na vijana kuwa ameonyeshwa au Bwana wa majeshi amesema nae juu yake. Zipo sauti nyingi zinazo weza kusema na mtu; mfano sauti ya Mungu, sauti ya Dhamiri na sauti ya Shetani.
USHUHUDA :
Rafiki yangu mmoja aliyedai kuwa Mungu alisema naye kwa sauti zaidi ya mara tatu juu ya binti Fulani nami nikmwambia kwakumtania kuwa hilo ni sembe-yaani shibe tu na tamaa zake, bali aliedelea kusisitiza kuwa Bwana amesema naye kabisa. Chakusikitisha yule binti alimwita kijana huyu ofisini kwake na baada ya kuwa amemnunulia soda huyu kijana asijue anachokiwaza binti huyu; mara binti akafungua kinywa chake na kumwambia kijana akisema, “ Sikupendi na una sura mbaya.”Huyu kijana hakuamini aliyoyasikia. Anasema hakuongea chochote na kama angejua kuwa haya ndio yalikuwa yamejificha kwenye huo wito asinge kwenda ofisini kwake. Kisha yule binti alimpa lift- alimpakia kwenye gari lake mpaka eneo aliloishi kijana huyu. Jakushangaza jamaa huyu aliendelea kudai huyo ndie chaguo lake; mara binti akapata ampendae na sherehe ya kuagwa –send-off ikafika na kufanyika kijana huyu alimwambia Mchungaji wake kuwa huyo binti niwake kabisa na wala ndoa haitafungwa; hayawi hayawi hatimae yakawa siku ya harusi ikafika na yule binti ameolewa na mara ya kufunga ndoa waondoka na mumewe kwenda nchini Marekani lakini pamoja na hayo mtumishi huyu aliendelea kudai kuwa ataachika na atarudi naye atamwoa; chakuchesha baada ya kuona jahazi linazama rafiki yangu huyu akaamua naye kuoa.
Hivyo ana familia yake.
Swali langu napengine na wewe unajiuliza kama mim; Je, huyu aliye sema naye alikuwa ni Mungu kweli? Au ni shetani au dhamiri yake?
SURA YA SABA:
UTAJUAJE KUWA HUYU NDIYE CHAGUO LAKO?
Vipimo vipo vingi vyakujua kuwa huyu ndiye aliye umbwa kwa ajili yako; lakini tuangalie kwa kifupi hivi vifuatavyo:-
[i] Amani ya Kristo ndani yako.
Amani ya Kristo ndani yako ndiyo sauti ya Roho Mtakatifu inayokuthibitishia kuwa upo sehemu sahihi. Filipi 4:7 na Mwanzo 24:56-67-Isaka na Rebeka.
Kama ushirika wako na
Roho Mtakatifu ni mdogo ni vigumu kupambanunua kati ya amni ya kawaida ya mtu
kupata alichokitamani na amani kama sauti ya Roho Mtakatifu inayo
kkuthibitishia kuwa upo salama.
USHUHUDA :
USHUHUDA :
Nikiwa katika moja ya semina ya vijana nikifundisha somo hili katika moja ya Kanisa jijini Dar es salaam; binti mmoja wa Kiganda alinyoosha mkono wakati nafundisha akasema, “Please Pastor let me speak some thing there.” [ Tafadhali Mchungaji naomba niseme kitu hapo ] Nikamruhusu akanza kusema ,”Ni kweli kabisa ulicho kisema Mchungaji, mimi nilimpata mchumba siku tu niliyomkubalia ombi lake kuwa tutaoana nilijikuta na kosa amani moyoni kabisa na nikaanza kumchukia kijana huyu na kila nilipo mwona au alipo nipigia simu nilijikuta napata uchungu; hivyo nikajua huyu sio chaguo langu ika nilazimu kuanza kufanya maombi ya dharula ya kumtoa moyoni kabisa kwani niliogopa kumwambia sikutani huku tayari nimemkubalia. Nilimwomba sana Mungu anitie nguvu na ujasiri mwingi ili nimwambie aachane na mimi atafute mtu mwingine kwani mimi sina amani moyoni. Tangu siku ile nilipo sitisha mahusiano na mawasiliano ya kiuchumba na kijana huyo nilisikia kuwa na amani tele na furaha kuu moyoni; na kwa sasa sina mchumba lakini moyoni mwangu nina amani tele kwani nimekuwa kama mtu aliyetoka gerezani na bado nina mwamini Mungu kunipa mtu nitakaye mpenda nayeye kunipenda, Amen.
Sambamba na hili kijana mmoja yeye alikuwa amekwisha kulipa mpaka mahari lakini akajikuta anakosa amani na akaamua kusitisha zoezi zima kwani ina semekana mpaka ukumbi wa sherehe ya harusi ulikuwa umekwisha kuandaliwa ; pamoja na hayo yote uchumba huo ulikufa na kila mtu akachukua mwelekeo wake au njia yake.
Hivi ndivyo ilivyo usije ukakubali kuolewa au kuoa mtu ambaye huna amani naye moyoni utakiona cha mtemakuni huko ndani ya ndoa; kufa hufi ila cha moto utakipata.
KUMBUKA:
Uchumba sio ndoa ; ni bora kuvunjika kwa uchumba kuliko kuvunjika kwa ndoa. Ukikosa amani juu ya jambo Fulani usitafute baraza au kikao au ushauri wa ndugu na marafiki, leo vijana wana msemo wao husema, “Piga chini, yaani achana naye kabisa.”Kuendelea na mahusiano huku ukiwa umekosa amani ni sawa na kujipeleka au kujiingiza mwenyewe jela au kifungoni. Kitendo cha kukosa amani ni sawa na taa nyekundu inayo ashiria hatari, hivyo achana naye mara moja.
[ii] Hata kushinikiza kufanya tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa.
Hatakuwa na haraka wala papara na hofu ya kukukosa [fear of loss].
KUMBUKA:
Tabia ya Mungu ni utulivu
, yaani amani.
Tabia ya shetani ni vurugu-papara au leo vijana wanasema
[fasta-fasta ] chapuchapu .
Eti utasikia wakisema siwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia, hii ni lugha ya kipepo kabisa achana na mtu kama huyo kwani atakuacha njia panda na kuijeruhi nafsi yako. Mithali 18:14, mara utasikia wengine wana sema tikisa vema kabla ya kutumia [ shake well before use]
ANGALIZO:
Binti uliye okoka usije ukakubali kuonjesha au kufungulia chemichem iliyofungwa [kufanya tendo la ndoa] itakuwa ni doa na utapata wakati mgumu wakuifunga tena hiyo chemchemi.
Usianze mahusiano ya tendo la ndoa [sexaul intercourse] kabla ya au nje ya ndoa. Hii ni ishara ya kuwa msingi wa mahusiano yenu sio upendo bali ni tamaa tu.
Biblia inatoa tahadhali juu ya kutoku ya chochea wala kuyaamusha mapenzi hata yatakapo ona vema yenyewe. Wimbo Ulio bora 4:12, 2:7; 3:5.
KUMBUKA : ukimwamusha
aliye lala utalala wewe mwenyewe.
Pia mapenzi yanafananishwa na chemichem iliyofungwa, [sealed ] siku itakapofunguliwa itaendelea kutamani kufunguliwa kila siku hivyo yawezekana hata utakapo kuwa ndani ya ndoa utaweza kusubua sana- hutaaminika.
Ukisha onja au kuonjesha utaendelea kuonjesha na hapo ndipo sasa mwisho wa uthamani na heshima yako- Mpaka umwendee Bwana Yesu kwa toba ya kweli na kwa maombi ya Rehema.
Tafadhali jitunze, jiheshimu na jithamini ili uimalize safari yako salama na kwa ushindi mkuu.
SURA YA NANE:
MAMBO
YANAYOVUNJA MAHUSIANO [UCHUMBA].
Yapo mambo mengi sana yanayo vunja mahusiano ya wapendanao au ya wachumba baadhi yake ni:-
[i]. Lugha mbaya [chafu] au Maneno ya hovyo unayo yaongea au kuyasema. Kuna watu hujiropokea na huongea lolote linalokuja. Chunga sana mambo yafuatayo:-
Maneno unayoyasema au kuyaongea juu ya umpendaye.
Adui yupo kazini
kuhakikisha anawachafulia usemi ili kuwasambalatisha, kwani akisha wanyang’anya
lugha hamna ujanja kwake. Mwanzo 11:1-9- Mungu anawachufulia usemi.
Maneno yanayo semwa juu ya umpendaye hata kama watasema maneno ya kumponda-yaani kumsema vibaya kama kweli huyu ni chaguo lako hayo maneno hayata kusumbua hata kidogo ndio kwanza mapenzi yata chanua.
Kumbuka yawezekana hao wanao mchambua na kumsema vibaya kumbe nao wana mpigia mahesabu au wanataka mkose wote; hivyo uwe macho kabisa.
[ii]. Mwonekano wako/ haiba.
Hapa ni vizuri kijana kuwa msafi [ smart] kiroho na kimwili; usiwe mchafumchafu-hovyohovyo [rough]. Kumbuka usafi ni sifa na tabia ya Mungu [ mbinguni]
Jifunze kuoga, kufua nguo zako, kupiga mswaki, kunyoa nywele zako sehemu zote zinazotakiwa, kujipaka mafuta na kujipurizia marashi mazuri; sio una mkuta kijana akikupita mbele yako una shika pua kwani anawapa taabu na wakati mgumu kwakuchafua mazingira-yaani hewa [ air pollution]. 1Timo.4:11-12
KUMBUKA:
Hata mtu mchafu hampendi mtu mchafu.
[iii]. Tabia au Haiba ya asili ya mtu:
Tabia ni somo linalo jitegemea kabisa kwani yapo yale makundi manne ya tabia za watu hivyo ni vema kuijua tabia- yaani mwenendo wa maisha ya huyo umpendaye; watu wengi kwakutokuwa na ufahamu wa tabia za wenzi wao wamejikuta hawamalizi safari zao bali huishia njiani. Mfano wa tabia hizi ni – ukimya, uongeaji, uchangamfu,uongo,ugomvi,wizi. Uzinzi, magonjwa ya kurithi, uchonganishi, utembez I [kiguu na njia], udokozi, n.k.
Hivyo tabia kama hizi zisipo shughulikiwa mapema kabla ya kuingia nazo ndani ya ndoa itakuwa ni shida tupu kwenye maisha yako ya ndoa. Ni vizuri kila mmoja akawa wazi kwa mwenzake ili kuyaweka mambo vizuri mapema. Mithali 30:11-14.
[iv]. Ahadi za uongo au zisizotekelezeka:
Kuna vijana hutoa ahadi nzito nzito kwa lengo la kukubalika na huyo amtakaye, na atakapo mkubali kwa sababu ya zile ahadi pengine za kumnunulia gari,nyumba , ndege n.k. na inapotokea kuwa ahadi hizo zimeshindwa kutekelezwa husitisha mchakato mzima wa mahusiano. Kumbuka hapo mwanzo niliongea vizuri katika mambo yakuzingatia katika mahusiano kuwa kijana usithubutu kumtongoza binti bali eleza ukweli wako na hitaji lako na usiogope kabisa kukataliwa. 2Yoh1:9-12 na Yoh. 8:43-44, uongo ni tabia kuu ya shetani. Tazama Mathayo 4:1-11 hasa mstari wa 8 unasema, “ Kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia ,Haya yote nitakupa, ukiniangukia kunisujudia.”
[v ]. Sifa au majivuno:
Tabia ya kujibebesha sifa za uongo ni tabia pacha na ile ya kutoa ahadi za uongo. Leo vijana wana sema, “Kujifanya wa matawi ya juu.” Yaani mtu wa hali ya juu kumbe sio.
Biblia ina onya juu ya kunia makuu kuliko kawaida. Rumi.12:3. Hebu jitahidi kuwa wewe. [ Be your Self ]. Utayafurahia maisha kwani hauigizi na utakuishi kwa uhuru zaidi.
[vi]. Mapenzi [kufanya tendo la ndoa] kabla ya ndoa na michezo ya kimapenzi:
Si jambo zuri hata kidogo tena siyo mpango wa Mungu kuanza kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa, Tendo la ndoa limebarikiwa lifanywe na wana ndoa yaani ndani ya ndoa.
Pia ni hatari kufanya michezo ya kimapenzi kwani ni sawa na kufanya tendo la ndoa. Mfano kunyonyana ndimi, kutomasana [kushikanashikana sehemu za siri na maeneo yenye kuamusha au kuchochoa hisia za tendo la ndoa], kushika matiti, kiuno n.k. Wimbo ulio bora 2:7 na Isaya 57:4-5. Biblia inasema,” ……msiya chochee mapenzi, wala kuyaamsha , Hata yatakapoona vema yenyewe.”Hapa vijana na mabinti wengi wameumizwa kwa kutishiwa kuwa usipo mpa tendo la ndoa atasitisha mahusiano; nimsema hapo mwanzo mtu kama huyo achana naye ni mharibifu kabisa. Na chakushangaza akifanikiwa kufanya tendo la ndoa nawe wengi wana achwa maana amekipata alicho kuwa anakitafuta. Na mara viongozi watakapo jua kuwa umefanya dhambi ya uzinzi huchukua hatua ya kuku adabisha [ kuku-discipline] na wengi hukimbia makanisa kuepuka aibu na fedheha ; hilo halitakusaidia tulia na kaa chini ili kutengeneza ili uwe na ndoa nzuri.
[vii]. Uchumba wa muda mrefu:
Si wote waliokaa kwenye chumba za muda mrefu mahusiano yao yalivunjika bali asilimia kubwa ya chumba hizo ziliishia pabaya sana. Nina shuhuda nyingi za kuonyesha kuwa ni hatari sana kuwa na chumba za muda mrefu; kwani mahusiano yao huvunjika vunjika vipande . Mungu hataki upate hasara kwa kukosa maarifa ;Efeso 4:27 anasema,” wala msimpe ibilisi nafasi” hivyo muda mrefu wa mahusiano wengi hujaribiwa na hata wakaona maamuzi waliyo yafanya si sahihi na waka tafuta wenzi wengine. Mfano wengine hukaa miaka 2,3,4,5, 6, 7, 8, 9, 10,……na kuendelea pengine kwa sababu ya kimasomo, safari za kikazi n.k.
·
Hebu nikuulize swali kama ulijua kuwa huna mpango wa kuoa
nimpaka baada ya miaka 3 au 7 kwa nini ujiingize kwenye mahusiano na kumpotezea
mwenzako muda? Ushauri wewe ni mwanafunzi soma kwanza ukimaliza anza mambo ya
mahusiano.
·
USHUHUDA:
USHUHUDA:
Ndugu yangu mmoja alikuwa na mchumba wake mara akapata nafasi yakwenda kusoma nje ya nchi huko Uholanzi kwa miaka kama miwili na aliporudi alikuta huku nyuma mwenzake amegeuza mtazamo na kumpata mwanaume mwingine aliye mpenda kuliko. Jambo hili lili muumiza sana ndugu yangu aliporudi nchini asijue kinacho endelea; badala ya kutegemea kupokelewa na mpenzi wake kwa furaha kinyume chake akajikuta ana pokelewa na kukataliwa na mtu aliye agana naye kuoana; alikuwa tayari amechukuliwa na mwingine. Kama nilivyo sema mwanzo ukikataliwa mshukuru Mungu kwani amekuponya na tatizo. Sasa ndugu yangu huyu ameoa na ana watoto na wanaishi nje ya nchi kwa sasa; wanafuraha na amani tele.
[viii]. Ukosefu wa mawasiliano:
Mahusiano yoyote hujengwa na kuimarishwa na mawasiliano. Watu husema mawasiliano ni nusu ya kuonana. Kwa hiyo kama kutakuwa na hali ya kupotea na kuvunjika kwa mawasiliano basi kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza mahusiano. Leo wewe ni shahidi tumepotezana na marafiki wengi sana kwa sababu ya kutokuwa na mawasiliano. Hebu rejea kwa rafiki zako wote uliokuwa ukisoma pamoja nao yamkini wengi wao hujui wako wapi na utakuta kuna mipango mliokuwa mkipanga kuifanya wote baada tu ya masomo yenu ; sasa imeyeyuka kwa kukosa mawasiliano n awapo wengine waliokuwa waheahidiana kuoana lakini ndoto hizo zime yeyuka mara tu ya kupoteza mawasiliano.
USHUHUDA :
Kijana mmoja alimpenda binti tuka mwita binti yule tukamketisha chini ili kuisikia kauli yake kama amekubali kuolewa au la; akasema tumpe muda akaombe ili kuthibitisha kama ni Mungu au sio, lakini hakika nilijua hataomba na wala wengi wao wanao sema naenda kuomba huwa; hawa ombi kabisa. Yule kijana akawa anasubiri jibu bila matumaini hasa pale namba ya simu ya binti huyo ilipo acha kupatikana kila alipopigiwa ; hii ilimfanya kijana kusalimu amri nakuanza mchakato mpya na sasa amempata ampendaye na maisha ya ndoa yanaendelea. Hivyo utakubaliana na mimi kuwa mahusianao ni mawasiliano. Amos 3:3 na Mwanzo 11:1-9. Silaha pekee aitumiayo adui ni kukata mawasiliano ili msiwaliane na kujenga nguvu ya pamoja.
[ix]. Usaliti [ betrayal]:
Hiki ni kitendo cha kuvujisha siri au kuwa kinyume na makubaliano-[ ni kuwa adui].
Mara nyingi usalti hutokea au husababishwa na tamaa ya mali na hofu ya maisha hasa pale wapenzi hawa wanapokuwa mbalimbali na kukosa mawasiliano, hivyo adui huingilia kati na kuwagawa hawa wachumba na kuwasambalatisha kabisa. Yoh.6:70.
[x]. Utofauti wa Imani :
Vijana wengi walioko nje ; duniani hutamani sana mabinti walioko ndani yaani waliookoka; hivyo baadhi ya vijana hukubali kuokoka kwa lengo la kumpata binti wa kilokole na akisha mpata ndio mwisho wa mchezo binti anakuwa ameumizwa na hapo mahusiano yao huingia matatani na hata kuvunjika kabisa; Hii ni kwa sababu kijana au binti alikuwa mpagani wakawaida tu. 2Kor.6:14-18- Msifungiwe nira pamoja na wasio amini, kwa jinsi isivyo sawasawa…….hakuna ushirika kati ya giza na nuru.
SURA YA TISA:
MAMBO
YANAYO JENGA UHUSIANO.
-Tumeona mambo kumi ya yanayopelekea kuvunjika kwa mahusiano na kinyume mambo hayo yana jenga mahusiano; pamoja na haya machache yafuatayo:-
[i] Ukweli uadilifu na uaminifu: Yoh.8:31-33 , 1Sam.16:7 na Math.5:37
Biblia insema kweli yenu iwe kweli na siyo yenu iwe siyo; maana yake; ni kusimamia unacho kisema [walking your talk] yaani kumanisha unachosema na kusema unacho maanisha.
KUMBUKA:
Uadilifu unahusika na tabia [moyo] wa mtu;
uadilifu unajengwa na kutenda ,kutekeleza ahadi na kujitoa kikamilifu.
KUMBUKA:
KUMBUKA:
Unapo poteza uadilifu unapoteza uthamani na
ubora wa ujana wako.
[ii]. Mawasiliano: Amos 3:3
[ii]. Mawasiliano: Amos 3:3
Wazee walisema mawasiliano ni nusu ya kukonana, kwa hiyo mahusiano yana jengwa kwa mawasiliano na kama hakuna mawasiliano hakuna mahusiano, maana hamtaweza kutembea njia moja mpaka muwe mmepatana kwanza.
[iii]. Lugha au Maneno mazuri:
Chunga sana unacho kisema mbele ya mwenzi wako mtarajiwa kwani ukiongea unampa nafasi ya kukuthaminisha na kukupima uwezo wako wa ufahamu. Kuna vijana wanajua kuongea vizuri na wengine walopokaji tu ; hivyo kijana fikiri kabla ya kuongea uwapo mbele ya huyo umpendaye
USHUHUDA:
Kijana mmoja alimchumbia binti na kabla binti hajatoa jibu la ndiyo au hapana , kijana akawa ana mshinikiza kutoa jibu huku akiropoka nami nikisika akisema,” Tazama naendelea kukonda tu , wala hunijali mtu unapendwa lakini haupendeki; kama hunipendi na hunitaki niambie mapema kwani mabinti ni wengi sana usinisumbue kwa kukubembeleza bwana.”Huo ni utoto ni kukosa misingi ya mahusiano kama hii. Ukweli binti alimkataa baadae kwani kijana alikuwa akiongea kama kameza kanda [anaongea sana] na binti yeye alikuwa mkimia tu akaamua kukataa kwani aliyaona matokeo ya ndoa yake mapema kabla ya ndoa yenyewe.
USHUHUDA WANGU BINAFSI:
Wakati na majira yalipowadia Mungu kunipa mke wangu kipenzi na chaguo la Mungu kwa ajili ya moyo wangu; nilipomwendea sikuwa na maneno yenye mbwembwe na madowido nilinyoosha maneno wala sikutafuna wala kumumunya mumunya maneno.Nilimwambia wewe ndiwe utakaye kuwa mke wangu na mzazi mwenzangu wa maisha tuzae watoto na kumtumikia Bwana Yesu na hivyo ndivyo ilivyokuwa hata sasa.
[iv]. Uaminifu: 1Kor.4:1-2,Zab.51:6 ,Luka 12:42-48
Mungu ana pendezwa na kweli iliyo moyoni; hivyo hata huyo umpendaye atakapo uona uaminifu wako kwake pendo litakuwa kuu sana. Kuna wanandoa wanaishi maisha ya kuchungana kama kuku mgeni; yaani hawa aminiani hata kidogo. Njia pekee yakumjua kuwa mtu huyu ni mwaninifu ni kumwamini.
KUMBUKA:
Hutaweza kumchunga binadamu kiumbe chenye akilli bali ni Mungu pekee ndiye awezae kumlinda na kumchunga.
[v]Mwonekano mzuri au usafi [smartness]:
Kama nilivyo eleza hapo mwanzo kuwa binti au kijana usijitelekeze mpaka ukawa kero kwa uchafu wa kiroho na kimwili. Jitunze vizuri,vaa vizuri na upendeze vizuri.
Hakuna mtu anayependa kukaa na mtu mchafu.
KUMBUKA :
Hata mtu mchafu na na yeye hampendi mtu mchafu. Hii ni ajabu na inafurahisha kweli
[vi]. Imani moja: Amos 3:3
Mkiwa na imani moja wote, Mungu mmoja,ubatizo mmoja, mbingu, ufamle mmoja zoezi huwa rahisi pengine tu asiwe chaguo lako, siyo ubavu wako.
[viii].Uwezo wa kujitawala au kiasi: Galatia 5:22
Ni jambo la muhimu sana kwa kijana au binti kuweka mipaka katika mahusiano. Ni vema kujua kuweka mipaka; wapi uongee na wapi usiongee. Lakini utakuta vijana hawana breki- mipaka, wanajiachia tu; hebu jaribu kujitawala kwani mwenzako ana kusoma hatua kwa hatua.
SURA YA KUMI:
MAMBO
YA KUZINGATIA ILI KUIMALIZA SAFARI YA MAHUSIANO SALAMA NA KWA USHINDI MKUU:
Yafuatayo yatakuwa ya msaada kama tu yatazingatiwa:-
[i]. Uwe na kiasi [ self control ]- Gal.5:22
Kijana ukiwa na uwezo wa kutawala hisia zako, mazungumzo yako basi utapenya katika safari au mwendo wako wa mahusiano salama.
Weka mipaka katika maeneo yafuatayo:-
1. Achana na Mazungumzo mabaya; Mazungumzo yasiyo na maana yatakayo kupelekea kumkosea Mungu. 1Kor.15:33.kwani, msidanganyike mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
2. Kutokuwa na mazoea yakupitiliza kati ya kijana na binti; Si jambo la busara kwa kijana na binti kufanyia maongezi mafichoni [ gizani ] kama vile mna ibana. Hii inaweza kupelekea ajali ya kuanguka dhambini; kwa kufanya ngono au tendo la ndoa nje ya ndoa.
3. Usijirahisi eti kuonyesha unampenda mwezi wako mtarajiwa.
“Uwe rahisi kuingilika lakini siyo kujirasi yaani wa dezo” [ Be simple but not Cheap]
[ii].Uwe na maono au ndoto: Mithali 29:18
Mtu mwenye maono ana mipango, malengo na mikakati katika mambo yake; hajiendei endei hovyo hovyo. Maono yatakufanya uwe na nidhamu na uwezo wakuweka vipaumbele.
Panga unataka kuishi maisha ya namna gani? Wapi? n.k
KUMBUKA:
Vijana wengi wanao anguka yaani kufanya dhambi ni kwa sababu wapowapo tu hawana maono, hawana mipango wala mikakati wamebweteka tu [ idol]. Hivyo kwa kuwa hawana mipango shetani huwapatia cha kufanya ; mfano kazi ya uzinzi –Mith.6:32. Watu husema akili isiyojishughulisha ni kalakana ya shetani [ idol mind is the work shop of the devil].
[iii]. Jaa Neno na Roho Mtakatifu: Luka4:1-15; Kol.3:16 na Zaburi 119:9-12
Neno la Mungu ni silaha tosha katika kuzipinga hila za shetani ; maana Neno ni upanga mkali ukatao kuwili…..na Roho Mtakatifu atakufundisha na kukuongoza ili usifanye makosa.
[iv]. Kimbia au ondoka maovuni: Mwanzo29:5-23
Mtumishi wa Mungu Yusufu, alichukua hatua ya kukumbia pale alipotakwa kwa nguvu kimapenzi; akakataa na akaamua kukimbia baada ya kukoswa koswa kubakwa na mke wa bwana wake Potifa mke wa Farao.
KUMBUKA:
Usijifanye kuwa wa kiroho kuliko au kupita Neno la Mungu / biblia utaumia. Kulifanya jambo lisilo la kiroho kuwa la kiroho ni kuuficha ukweli uliokusudiwa kujulikana.
Utashangaa kuona kijana na binti si wana ndoa ni wachumba tu anashinda chumbani mwa kijana tena anakaa kitandani na ikibidi hujipumzisha kabisa pamoja na kumpikia chakula; kupika si dhambi ila sio wakati wake subiri ufunge ndoa . Kumbuka, upo mwilini na kijana na binti ni sawa na hasi na chanya kwa kukosa nidhamu ya kuweka mipaka lazima kutatokea kishindo cha mlipuko wa hatari. Hapa hukatazwi kuongea na mwenzako ila unafanyia wapi hayo maongezi. Nini usalama wa mazingira hayo? Jitahidi kufanyia maongezi yenu katika maeneo yalio wazi ili adui asije akapata nafasi ya kuwa maliza. Pia mtakuwa salama dhidi ya wachafuzi na wachongezi.
[v]. Fanya maombi : Luka 18:1-8
Kumbuka uchumba sio ndoa bali ni safari kuelekea kwenye ndoa hivyo unatakiwa kufanya maombi ya ulinzi wa mahusiano yenu kwani adui hata waacha hata kidogo atahakiksha anafanya awezalo ili kuwakwamisha; lakini kama mtadumu katika kumatafuta Mungu na nguvu zake lazima mtafanikiwa tu. Ni sawa na mama aliye mja mzito, asipokuwa macho uja uzito utaharibika na kama akijifungua vizuri haitoshi lazima amuhudumie mtoto mpaka aweze kujitegemea mwenyewe.
KUMBUKA:
Kupokea muujiza ni kitu kingine na kuutunza muujiza huo ni jambo jingine kabisa; tuna pokea vitu vingi lakini havipo leo kwa sababu hatuna ufahamu wa kuvilinda ili vidumu.
Kuwa na kitu
haimaanishi unakimiliki; unaweza kuwa na mchumba na mtu mwingine akaja aka
mmiliki [ kumwoa ]; [ To own does not
mean to possess.] Rejea kwa Adamu hakusimama kwenye nafasi / zamu yake ili
kuilima bustani na kuitunza maana yake ni kuilinda; shetani hakumchelesha alimtoa
bustanini kwa kumkosanisha na Mungu kwa kuto kutii maagizo ya Mungu. Tazama
Mwanzo 2:15-17 na Mwanzo 3:1-24 hasa mst 23.
USHAURI:
Ipo siku utashangaa huyo huyo mpenzi wako umpendaye atakuumiza na hata kusababisha mtikisiko na maumivu mkubwa kwenye moyo/ nafsi yako na hata kukufanya ulie kama mtoto; isikusumbue hata kidogo kama ni chaguo lako toka kwa Mungu lazima vita iwe kali sana kuhakikisha shetani ana pingana na kusudi la Mungu kutimia kwako. Usikate tamaa songa mbele kwa imani huku ukimwomba Mungu siku zote ili kuimaliza safari yenu salama na kwa ushindi mkuu. Ukweli ukiwa vizuri na Mungu shetani hataweza kuwatikisa wala kuwashinda kwani tumehakikishiwa ushindi na Bwana Yesu katika Mathayo 16:18-19 na Warumi 8:31-33.
SURA YA KUMI NA MOJA: MAOMBI:
Baba mtakatifu, Katika Jina La Yesu Kristo Nina kushukuru Kipekee Sana Kwa Kunipa Ufahamu Na Maarifa haya; ninakikaribia kiti chako cha Neema na Rehema ili nipewe Rehema na Neema ya kunisaidia wakati wa mahitaji. Ninaomba toba dhidi ya uovu ,dhambi, makosa, ukaidi na uasi. Nitakase kabisa roho yangu, nafsi yangu na mwili wangu nihifadhiwe pasipo lawama hata siku yakuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Naomba toba juu ya misingi bibovu iliyo nibeba, naomba toba juu ya maisha yangu ya mahusiano yanyooshe mapito yangu; Kwani Ndiwe Unifundishae Ili Nipate Faida Nakushuru Kwa Ajili Ya Mtumishi Wako Uliye Mtumia Ili Kunipa Maarifa Haya Maana Hutaki Niangamie Kwakukosa Maarifa Kama Usemavyo Katika Hosea 4:6 Nami Nitawasaidia Wenzangu Ili Wasije Kuangamizwa Na Adui;Mungu Nisaidie Na Kunitia Nguvu Na Kuniwezesha Kuyafahamu Haya Na Kuyatii Ili Mwisho Wangu Uwe Mzuri Katika Jina La Yesu, Amen.
MWISHO:
Nina imani KUU SANA kuwa somo hili limekuongezea ujuzi,maarifa na
ufahamu wa kutosha kukusaidia katika kuenenda katika mapenzi ya Mungu kwa
kipindi chote cha mahusiano au uchumba wenu. Nawatakia baraka za BWANA na
USHINDI MKUU katika kipindi chenu cha uchumba na hatimaye mkawe na NDOA YENYE
UTUKUFU WA MUNGU, AMEN.
UISHI MILELE- 2KOR. 13:14
MAWASILIANO:
ANUANI YA MWANDISHI:-
PASTOR. SONGWA .MM. KAZI
TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD
GLORY TO GLORY CHRISTIAN CENTRE
GGCC - TAG FOREST KONGOWE
GGCC - TAG FOREST KONGOWE
S.L.P 70983, DSM
Simu: 0757-567 899, 0789-567 899,
Whasap: 0719-968 160.
Blog: lcm2014.blogspot.com
Email: ptrsongwak@gmail.com
songwak@yahoo.com